Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Nitatoa uzi mdaa sio mferu niliingia dsm kizembe na mtaji Wa 2 million baada tu ya Ku graduate, after 2 weeks sikua hata na mia mbovu na mzee kipindi ananipa huo mtaji alinipa husia kwa masaa 7 na kunambia tusijuane tena so pambana. Na Mimi baada ya mtaji kuisha hata sikurudi nyumbani 😁😁 kilichoniokoa ni ajira serikalini walitangaza nikaotea.
Wosia wa masaa 7 😂😂😂😂😂😂
 
Mwaka 2020 ni mwaka ulio nipiga mpaka leo sijatengamaa ile corona ile dah kwangu naonaga ni mwaka wa shetani kwangu.
Kuna ndugu yangu alikua anafanya kazi zanzibar, kwa siku alikua analipwa 35 na hayo matips hadi laki anaipata kikawaida kabisa kila akienda kazini, ilikua kwenye ma hotel haya ya kitalii.

Hii corona ilivyoingia zanzibar walikua very strictly kidogo, na wazungu wakaisha kabisa.

Mwamba alifilisika kiasi kwamba akarudi hapa dar akawa dereva bodaboda mpaka leo hajasimama tena. Kila ukiongea nae anailaumu sana hio corona.
 
Yote ni kushika pesa mikono yako haijazoea kushika

Mfano umezoea kuwa na laki to laki tatu ndo unaweza ibalance then unakuja shika milion kumi mara nyingi sana itaisha ikibaki laki ndo unapata akili

Nakumbuka nikiwa bado chuo sikuwa nimewah shika laki tano kasoro yangu kwa mkoa ule ambao bajet ya mtoto wa kiume milo mitatu ni 2500 kwa siku

Nikapiga zali moja nikapata 480k asee nilibadilika pesa mfukoni zipo nikabadil milo ..et siwezi kula wali nyama mkavu bila soda 😁 wakati mwanzo wali marage tupu daaa ..ile pesa sijui iliishaje
Very true🙌🏾
 
Mimi hapa nishapata wazo,

UONGOZI WA JF,AU YEYOTE ANAYEWEZA AFANYE KUPRINT UZI HUU KTK NAKALA NGUMU.KILA PAGE 1 YA HUMU NA KULE INAKUWA NI KURASA MOJA AU ZAIDI.MWISHO ZINAPATIKANA KURASA ZAIDI YA 100 NA KINAKUWA NI KITABU KAMILI(JINA LINABAKI KAMA KICHWA CHA UZI KILIVYO)
TAFADHALI FANYENI KITU KWA AJILI YA VIJANA WAJAO!
@Maxence melo
 
Nikiwa chuo nilipataga mkopo, lakini kukawa na hitilafu Fulani boom wakawa hawaniingizii. Nikaendea kufuatilia. Kufikia mwaka wa pili wa masomo wakaniingizia maboom yote at once ambayo sikuwa napewa. Mama yangu! Mwisho wangu wa kushika pesa ndefu ilikuwa ni laki moja, Sasa akaunti ikasoma milioni 2 kama na laki nane hivi. Ilikuwa mtu akilia shida kidogo tu nachomoa hata elfu50 Nampa.

Mwaka wa pili wa masomo haukuisha pesa zikapukutika zote. Nikawa kama kuku tu, lilikuwa fundisho kubwa sana na majuto sana. Nilipomaliza chuo nikawa na adabu sana na pesa.
 
Mimi ndio ngedere kabisa nilifanya kazi kwenye kampuni ya gas ndani ya miaka mi3 nilipata kama milion 10 nikanunua pikipiki ya kutembelea nikawa kazi yangu kuwafata mademu na kwenda kula bata beach demu nikimpata mtandaon hata awe anakaa Kibaha namfata na pikipiki kiukwel sikuamini kama ile hela ingekuja kuisha nilikuwa naiona nyingi sana kumbuka mii nmetokea familia ya kimasikin hivi nnavyoandika hapa nmerudi naishi home kwa baba na mama sina hata mia mfukoni
Tinder, badoo na hi5 zinawangamiza vijana
 
Nikiwa chuo nilipataga mkopo, lakini kukawa na hitilafu Fulani boom wakawa hawaniingizii. Nikaendea kufuatilia. Kufikia mwaka wa pili wa masomo wakaniingizia maboom yote at once ambayo sikuwa napewa. Mama yangu! Mwisho wangu wa kushika pesa ndefu ilikuwa ni laki moja, Sasa akaunti ikasoma milioni 2 kama na laki nane hivi. Ilikuwa mtu akilia shida kidogo tu nachomoa hata elfu50 Nampa. Mwaka wa pili wa masomo haukuisha pesa zikapukutika zote. Nikawa kama kuku tu, lilikuwa fundisho kubwa sana na majuto sana. Nilipomaliza chuo nikawa na adabu sana na pesa.
Your best teacher is your last mistake...mimi niliajiriwa mgodi x take home ilikuwa 760k ilikuwa wazee wakinipiga vizinga kutoa 100k ni kawaida sana mara paap! kibarua kikazima kama mshumaa savings sikufanya aisee hao hao ndo wakwanza kusema "hata akiba alikuwa hajiwekei"..ila now nimekuwa mgumu sana kutoa pesa kizembe maisha ya kitaa yamenifunza aisee

NB: "THE WORST OF NOT HAVING MONEY IS HAVING IT AND LOSING IT"
 
Nitatoa uzi mdaa sio mferu niliingia dsm kizembe na mtaji Wa 2 million baada tu ya Ku graduate, after 2 weeks sikua hata na mia mbovu na mzee kipindi ananipa huo mtaji alinipa husia kwa masaa 7 na kunambia tusijuane tena so pambana. Na Mimi baada ya mtaji kuisha hata sikurudi nyumbani 😁😁 kilichoniokoa ni ajira serikalini walitangaza nikaotea.
Pole sana Mkuu eti baada ya 2 weeks huna ht Mia mbovu 😆😆
 
Kuna ndugu yangu alikua anafanya kazi zanzibar, kwa siku alikua analipwa 35 na hayo matips hadi laki anaipata kikawaida kabisa kila akienda kazini, ilikua kwenye ma hotel haya ya kitalii.

Hii corona ilivyoingia zanzibar walikua very strictly kidogo, na wazungu wakaisha kabisa.

Mwamba alifilisika kiasi kwamba akarudi hapa dar akawa dereva bodaboda mpaka leo hajasimama tena. Kila ukiongea nae anailaumu sana hio corona.
Huyo hajafilisika alikua mzembe na mwizi tu.
Kazi ya hoteli kupata laki kwa siku sio tipu ni wizi tu humo.
Sasa angejiandaa vizuri mtaani hata bila kuilaumu corona ingefika siku kazi angefukuzwa.
 
Mkuu nimefukuzwa kazini kwa madai ya utoro maana nilipata issue moja,emergency nikaomba ruhusa nikanyimwa ikabidi nisepe hivo hivo,hasa kupata barua ya termination hawataki kunipa.
Hivyo na nssf yangu ngumu kupata

Mkuu kama una vielelezo vyote kawashtaki labour usiogope mkuu utapata haki yako.
 
Back
Top Bottom