Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Usiwalaumu watu kwa matatizo Yako.

Kila mtu ana matatizo anayoyapa kipaumbele.
 
Dah watu wahonga aisee..mi nilihonga afu ishirin naiwaza hadi leo
 

Si ungekopa kwingine pia ukute alikuwa hana
 

Mbongo akipata pesa anachanganyikiwa anakuwa na machawa kibao wnaamfilisi
 
We acha tu bei uwa inacheza vibaya sana.Nimekuelewa vizuri
 
Nine share nyuma experience yangu nyuma

Leo Nimekutana na experience hii ya bilionea nigeria aliefilisika karibu kupoteza 80% ya assets

Femi otedola ni billionea wa Nigeria ambaye alipata ukwasi mkubwa sana kwenye mafuta , aliweza shikilia soko zima la nigeria kwenyemafuta

Ghafla mwaka 2008 aliweza kuagiza tani nyingi za mafuta za thamani ya dola milioni 800 zaidi

Ghafla bei ya mafita ikashuka kutokana na uchumi kuanguka

Ghaflaakaingia kwenye matatizoya kuuza mafuta kwa hasara ya 80% zaidi

Kumbuka alikopa hela bank kwa pesa za kimarekani

Alipata hasara ,akaingia deni $1,200,000,000 kutokana na deni halisi, kushuka kwa thamani yanaira na riba

Alitamanikujiua lakini akaamuakuanza upya


Aliamuakuuza malizake karibu zote

Alikuwa largest shareholder wa banks akauza share zote

Alikuwa na flats 196 appartment akauza zote pamojana mali nyingi


Lakini hakikata tamaa akaanza upya

Leohii karudi kwenye chati kama bilionea wa dola


Waweza fuatilia video kwa kufuata link hio


 
Asante Sana mkuu,Hadi SASA nakula msoto nakazi nimehamishwa kwenda eneo ambalo sio la kupata pesa naishi Kwa kibangaaiza Tu nakibarua chenyewe nikichungu ,huuu Uzi umenifariji Sana Sana Sana Tu.
Uko wapi now kikazi
 
Aisee haya maarifa wengi hatuna. Ila tunajifunza humu JF.
Mungu akubariki sana Bwana Kobello
 
Nakumbuka 2018 wakati bado nilkuwa o-level niliweza kubana pesa kuifikia kiasi cha laki 7 ni kapata wazo la kuwekeza ktk kilimo cha mihogo wilayani mkuranga kata ya hoyoyo kijiji cha hoyoyo. Bahati mbaya mvua ikawa adimu jua kali mbegu yote ikauka nikaweka nyngne pia nayo hvohvo nikakata tamaa kutokana na ckuwa na pesa nyngne na istoshe nilkuwa naingia kidato cha nne ambapo nilitakiwa kuspend much time kweny masomo. Nakumbuka iyo siku nilrudi nyumbani nimechanganyikiwa nililia sana nikaona kama mkosi. Mungu c Athuman nilipokea kiasi cha shilingi million moja na laki tatu kweny bank account yangu. Sikuamini nikaacha week ipite hatimae mwezi hamna mtu aliyenitafuta, nilifatilia bank kama Kuna miss deposits nikaambiwa hamna tatzo nikatoa pesa zote nikanunua kiwanja Alhamdulillah machungu yalifutika
 
Bora wewe 70 mimi kuna mtu nimemfungulia salon na niko mwenyewe kwanza na check upepo week nzima imeingia tsh 2500 hahahah saloon ina week 2. Na hlo eneo salon ni mimi tu
Biashara ni imani..fanye utafiti pia kujua nini hasa tatizo.

#MaendeleoHayanaChama
 
2011, nilianza biashara ya kuuza milango na anko na muuzaji akawa mdogo wangu.

Biashara ilienda hadi tulafikisha mtaji wa mil 20. Kuingia kwa Magufuri kukaleta majanga.

Ikawa ngumu kupata vibali.
Tulashauriana na anko tukapata njemba moja ikasema itatupa leseni ya uvunaji. Tukalipa mil 5, zikaenda hadi leo.

Nikamwambia anko tununue mashamba tupande miti itakuja kutusaidia. Anko akagoma.

Watu watatu tuliowakabidhi mzigo na tulikuwa tunawapata wanarejesha, wakafilisika na familia zao zikaparaganyika, nyumba zao zikauzwa na bank.

Sasa sisi tutalipwaje? Pesa ikapotea as simple as that. Mpaka sasa tunawadai hela nyingi watu halafu sisi hatuna hata senti.
 
Hela za urithi hazina hasara.
Nilizitumbuaaaa.
KATIKA MAISHA HAKUNA KITU KIZURI KAMA KWENDA KU WITHDRAW ATM.
Mwezi wa tatu mwaka jana nikapewa mil 8 za mirathi. Nikawaza nifanyie nini? Wazo langu la kwanza, ninunue shamba porini, nifuge mbuzi na kondooo. Nikaenda minada ya mbuzi na kondooo, nikakuta hali siyo nzuri. Yaani vitoto vinauzwa kwa bei ya mbuzi na kondoo waliokomaa.

Jamaa yangu akanishauri tuchonge mitumbwi na kununua nyavu. Mwanzoni nikapewa tu hela, nikaongeza mtaji.

Nashtuka naambiwa nyavu za 2mil zimeibiwa. Hadi sasa nimebaki na mitumbwi yenye rangi ya tanganyika tu
 
Ule wimbo wa Selina selina, uongo wako selina
 
Mmh aisee bhasi ilikuwa kama zariii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…