Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Huwez
mipango inakuwepo mingi tuu,hela zikishakaa mkononi matumizi ndo yanatawala,kwa maswali uliokua unamuuliza ni wazi mzee alikua hajitambui,hukusima kwenye nafasi yako,yawezkana matapeli (matumizi yasio rasmi)yalimtafuta wewe mwerevu (mipango ya maendeleo)ukajifungia na alikua muwazi kwako 100%
Huwez kumtafuta sana mtu mwenye hela, atakuona nuksi, ndo maana jamaa Ali mute kwanza,na Mzee alipopata chench akasepa, hela ndo IPO ivyo.
 
poleni wakuu shida yote ni iblisi anayotupelekea kufilisika maana ukiwa tu na hela ya Maana kitu cha kwanza akili inakutuma badaya kushauriana Na iblisi ni pombe na umalaya. na ukiingia huo mtego huchomeki kabisa.
 
Ukimuona ndugu yako au rafik yako kapata pesa anakuomba ushauri ingia JF tafuta huu uzi mpe ausome wote

Akimaliza halafu akatumia pesa vibaya huyo kaumbwa awe maskini tu

Huu uzi wange uaattach hpo juu tuwe tunarudia rudia kuusoma ni fundisho kwa sisi vijana

Kma una mtoto anza kumzoesha kumpa pocket money awe anapanga matumizi mwenyew ya wiki nzima hata kama yuko day mpe hela ajipangie anunue nini atumie sh ngap kwa siku itamsadia baadae kuwa na ni mtu mweny kupangilia matumiz yake

Nashukuru Mungu sina wenge la pesa sana ila bado sijashika nyingi bado naendelea kujifunza kwa pesa nilizopata mpk saiv bdo sjatumia vibaya sana

Sijawah kufilisika maana sijawah kushika pesa za kusema nimefilisika
 
Uko sahihi kabisa mkuu tangu nijiunge jf huu Uzi umenifanya nijifunze vtu vngi sana nakujiona sipo peke yngu niliye anguka ktk kutafta maisha pia kwa sku ya Leo nimecheka sana mana kuna haya mambo pombe na mademu ni mambo ya muda mfupi lakini majuto yake adi mauti.

Ila kilimo hakijawai kumwacha mtu salama, mm ufuta uliniangusha Mara 3 nikanyoosha mikono juu. Ila kikubwa kutokata tamaa.
 
Uzi mzuri sana huu. Vijana wote muusome mara kadhaa. Jambo la kwanza kabisa na muhimu kuliko yote ni NIDHAMU yako wewe binafsi ndani ya moyo wako. Unapopata pesa (ya halali), kwanza kabisa toa zaka au sadaka yoyote ya shukrani kwa Mungu. Ukifanya hivyo, unakuwa umeanza hatua ya kwanza ya kujijengea nidhamu ya nafsi yako.

Hatua ya pili:- Ziache hizo pesa benki kwa muda fulani (miezi kadhaa) UJIFANYE KAMA HUJAZIPATA. Hilo ni JAMBO GUMU (amini usiamini). Ni vigumu sana mtu kupata pesa nyingi kwa ghafla na kuacha kujionyesha. Ukishaweza kuwa na nidhamu ya kuendelea na maisha yako kama zamani wakati ulikuwa huna pesa, utakuwa umeshashinda kwa sehemu kubwa uwezo wa kuha kufilisika kirahisi.

Jambo la tatu ni kujaribu kwa nguvu zote KUZIMA MSUKUMO WA KUTAKA KUTAJIRIKA HARAKA. Nashauri ukipata pesa yoyote, usijaribu kuwekeza zaidi ya theluthi moja ya pesa hizo. Yaani ukipata milioni kumi na mbili, fikiria biashara unayoweza kufanya ambayo mtaji wake hauzidi milioni nne. Ng'ang'ana na hiyo biashara weee...Ukishaona inalipa, ndipo uongeze mtaji wake au uanze ya aina ingine ambayo nayo haizidi milioni nne. Kumbuka:- Kamwe USIANZE CHOCHOTE BILA KUKIFANYIA UPEMBUZI MKUBWA KABISA KWANZA. Unaweza ukalima na ukapata mazao mengi lakini kama huna soko la uhakika tayari umeanguka.

Unaweza kuanza biashara (k.m. duka au saluni n.k.) ambayo kwa kawaida inalipa vizuri lakini ukawa huna watendakazi wazuri au biashara haipo mahali penye wateja wengi wa biashara hiyo. Ni afadhali utafute fremu ya biashara yako uwe unalipa laki sita kwa mwezi mahali ambapo kuna wateja wengi kuliko kutafuta fremu ya laki tatu mahali ambapo wateja ni wa kubahatisha. Ni afadhali "umtoe"mfanyakazi bora uliyemwona mahali umlipe ghali ahudumie wateja wako vizuri kuliko utafute tu "wa kuokoteza" Ndio maana nimesema unatakiwa kufanya "upembuzi" wa kina kabla ya kuanza biashara. Lakini mwisho wa siku, jambo muhimu kuliko yote yanayomfanya mtu asifilisike ni NIDHAMU.

Watu wote duniani ambao waliwahi kupata pesa nyingi lakini zikaisha fasta walifilisiwa na TAMAA ZAO (yaani kukosa nidhamu). Kutaka fahari ndio kumefilisi wengi. Ukiwa baa unanunulia wote ili wakuone "unazo za kumwaga" Fahari ya kumchukua kila demu mzuri anayekatiza mbele yako, kuvaa mavazi ya ghali sana uonekane wewe ni bora zaidi n.k. Mimi binafsi nilishapata nyingi tu zikaisha- Nilikuwa nataka kutajirika haraka nikawekeza zote. Mtaji wote ukakata. Ni kama vile kuna "shetani fulani" anakufanya usishituke haraka- unakuja kutambua wakati zimebakia milioni mbili kwenye milioni hamsini ulizokuwa nazo.

Mimi nilipozinduka ndipo nikajiuliza ni wapi nilikosea. Nilipojua, nikajirekebisha. Sikukata tamaa nilianza tena kuanzia hatua ya kwanza lakini safari hii nikawa mjanja sikufanya tena kosa. Usisahau kamwe !!! Wanawake "wadangaji" wanajua "kunusa" ukiwa na pesa ni ajabu !! Waogope kama ebola !!
 
Back
Top Bottom