Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

hahahaaa!! zungushaaaa, wape bia haoooo!!! wanywe mpaka waombe poa!! kampuni kubwa hiiiiiiii!!!, bill inakuja 70,000/= mfukoni una 50,000/= unachukua pikipiki fasta huku wadau unawaacha wanakula mvinyo, unaenda kuvuta 200,000/= ili imalize kila kitu[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] mnahama viwanja huku group linakufuata nyuma kila MTU na bebi wake unawanywesha wewe!!!
Unachosema Ni kweli mkuu.Kwa upande wangu pombe ndo kikwazo kikubwa cha mafanikio yangu.Hua naweza kuamua kuacha pombe hata miezi 3, cha kushangaza naweza kosa Hadi nauli ya dala dala!![emoji849][emoji849]Cha kushangaza nikirudi kwenye kinywaji pesa napata Ila haifanyi lolote zaidi ya anasa[emoji848][emoji848]
 
Kwa mara ya kwanza kudraw hela ya Forex 2 Million, kwa akili zangu those days iyo hela sio rahisi kuisha.

Niliwahi lipia mhudumu mmoja alikuwa off duty nauli ya Tax usiku saa 7 aje anichanganyie cocktails eti siwezi kulala bila iyo kitu.

Ilikuwa ukinikuta nimetulia bar hata kama sikujui na umenizidi umri utasikia, "mbona unanikosea adabu, weita mpige huyu na bia anazotaka" hapo niko na John walker red label.

Mamaaaee ile hela hata Boksa sikununua.
😂😂😂😂😂😂😂
 
Duuh kumbe mimi sijachezea pesa nyingi mimi nilikamata 65m. Sinywi pombe zipu nilifungua kidogo tu wala haikuzidi laki3.
Mzigo ulikata ndani ya miezi 4 tu chali. Nilikutana na watu sio sahihi katika biashara wakafuja mtaji. (Fundisho)
😂😂😂😂😂😂 daaah
 
Ukipigika kuna wakati hata vumbi linakupausha, ila ukiwanazo bwana hata vumbi linakuogopa..

Ulishazoea kuwa na confidence, maana mfuko ukiwa vizuri binadamu hata confidence anakuwa nayo....sasa ukipigika dah hata ile confidence inapotea na muda wote unakuwa na hasira..

Tumuombe sana Mungu alinde vipato vyetu, Tumuombe sana Mungu atubariki tuwe na vipato vizuri..
Kupigika ni noma sana mkuu,kuna muda unahisi kama dunia nzima inakuzomea.
 
Ni kweli..hata sisi nyumbani mama alipokua ana maisha safi ndugu walikua hawakauki nyumbani..wengine hata hatuwajui sasa hivi hali mbaya mno nyumbani hatuna ndugu anayekuja hata kugonga hodi.
Ndio wanadamu walivyo boss....pambaneni nafasi nyingine itakuja tu na hao ndugu watawatafuta tu.
 
Back
Top Bottom