Mwaka 2011 soko kuu mwanza nikiwa ninauza nafaka zikiwemo karanga, njugu, choroko,dengu,ufuta,ulezi,uwele,mtama,maharage na kunde.
Kamtaji kalivyokuwa nikawa naendea karanga tabora tani kadhaa nauza jumla. Nilipata pesa kwa njia hiyo. Basi kufkia December karanga zikawa chache Sokoni hivyo mwenye nazo alipiga pesa balaa.
January 2012 nikaingia poli kusaka karanga mpya ili niwahi bei sokoni. Basi nikapata kama gunia 30 (tani 3). Kufkisha Sokoni ziligombaniwa kama nyama. Nikaona pesa si hii apa. Nikazoa msingi wote around kama 22.8m. ili nikapige mkupuo mmoja nije nitulie.
Kuleta mzigo nafika Sokoni nakutana na fuso 6 zinashusha mzigo. Sasa kila mmoja ashajua ni dil acha bei ishuke. Nilijikuta karanga nimezinunua 2300 natakiwa niziuze 1600. Sasa nilipoharibu nikapiga mzigo stoo kwamba bei ikikaa sawa nitauza duh! Kumbe mzigo si haujakauka vizuri, nilikaa kama wiki nafungua stoo nakuta mzigo wote umevunda... Duh!