Mwanzon mwa miaka ya 70s ndio niliingia mjini kutoka kijijini kabisa huko mkoani, Elimu niliyokuwa nayo ni ya darasa ya VII na sikuwa na mtaji au chochote cha maana kinibebe nilipofika town zaidi ya kuwa na misuli imara iliyotokana na jembe la bush na ujasiri niliotoka nao kijijin.
katika harakati za maisha nikapata mtu alienipa idea ya kujiunga na mfunzo ya ufundi na kweli nikaanza mafunzo. Baada ya kumaliza mafunzo nikaingia mtaani kufanya kazi za hapa na pale kwa kujiajiri na baadae nashukuru Mungu kupitia fani yangu ya ufundi milango ilifunguka na hadi kumiliki nyumba ya kwanza nikiwa na miaka sio zaidi ya 30(yaani kijana haswa huku nikiwa na usafiri wangu wa gari pendwa miaka ya 80s).
Niliendelea na shughuli zangu za ufundi kwa kipindi chote na ndio ulikuwa msingi wa kuendesha familia yangu kwa kusomesha watoto shule nzuri, kuhudumia mama(wife) na bata za mjini[emoji482]. Miaka ilisonga nikapata nyumba ya pili na kubadili magari hadi kufikia gari zaidi ya 4 zilizopita mkononi mwangu(kuzimiliki) . Ilipofika mwanzoni mwa miaka ya 2000 nikapata ushawishi wa kujiingiza kwenye shughuli za ukandarasi( contractor), ofcoz niliipenda hii na mwanzo hela niliiona, nikaingia mazima na balah likaja baada ya kupata kazi/tender ya sio chini ya 350Milioni, hapa ikumbukwe sikuwa na mtaji pia Serikali kama mjuavyo kidogo kunakuwaga na ucheleweshwaji wa malipo.
Hivyo sasa ikabidi niingie kwenye mikopo ya mtaani tena kwa hawa jamaa hata wasio kuwa authorized kufanya kazi za ukopeshaji, kiukweli lengo lilikuwa nikope nikimbize site(tender) kisha malipo yakitoka nirudishe deni, ila hawa mabwana ni kama waliniloga maana mikopo ilikuwa na riba kali tena za hovyo ikifika hatua malipo niliyotegemea hayatoshelezi tena kulipa madeni niliyo nayo, hapa nilipoteza nyumba, gari yote kufidia madeni hadi ikafika hatua na kampuni ikafa kabisa nikawa sina kazi yoyote huku nikiwa na madeni yanayozidi milion30 na hayana kichwa wala miguu, niliishi kwa kujicha kama digidigi mtaani, hapa niliona dharau za wazi wazi kwa wale nilidhani ni wema kwangu before. Nashukuru Mungu nilihama eneo husika na kuanza maisha eneo jingine na milango mipya ikafunguka na maisha yanasonga hadi sasa.
Somo nililopata ni usivamie biashara/tenda kubwa ikiwa bado hujajiimarisha mtaji wako kisa tu unaona bajeti ya tenda digits zinakuvutia, lakini pia hii isikufanye uache kuchangamkia fursa mpya kila mara zinapo jitokeza