Tuliowahi kusafiri na magari ya magazeti tukutane hapa

Tuliowahi kusafiri na magari ya magazeti tukutane hapa

Bosi hivi ulishapanda haya magari ukaangalia ukaaji au unajisemea hakuna mtu anafunga mkanda wala nini,Ni kweli iko cku kila mtu atatangulia ila tuache kupanda vitu hatarishi
Sijawahi ila ninachoamini ni kwamba Mungu alishapanga kila kitu , na siku ya kufa hutowaza tena kwamba huu usafiri ni hatarishi. Utapanda na ahadi itatimia
 
hao madereva wako vizuri maana hata ajali zao haziskiki so wako saafi kabisa,
dereva wa basi toka s wanga mpaka dar,au kyela dar hawa nao si mchezo wanasukuma zile mashine ile ni safari mama km hujawahi pita hiyo njia jaribu,maana kuna vipande hapo kati ni tambarare tu sasa ndo unaona ufundi wa dereva km una roho ndogo utashuka
Ajali utazisikiaje wkt wenyewe ndo wandishi wa habari?
 
hao madereva wako vizuri maana hata ajali zao haziskiki so wako saafi kabisa,
dereva wa basi toka s wanga mpaka dar,au kyela dar hawa nao si mchezo wanasukuma zile mashine ile ni safari mama km hujawahi pita hiyo njia jaribu,maana kuna vipande hapo kati ni tambarare tu sasa ndo unaona ufundi wa dereva km una roho ndogo utashuka
Mkuu si naskia bus zimefungwa speed governor mwisho 80kph... Au jamaa uwa wanapitiliza hio speed?
 
IT usijaribu kupanda kama una moyo mdogo unaweza kuomba ushushwe uendelee kutembea na miguu

Magari ya magazet kwa IT yanasubiri sana
hapana gari za magazeti ni noma kuliko it..... it zinatofautiana na madereva wanatofautiana.....pia it ni risk sana madereva wengi ni lafu hawako makini wengi siyo wazoefu... wale wa magazeti ni proffesional wanakimbia lkn wako makini sana
 
nakumbuka safari moja ya chuga nilikuwa na CELICA GT 4 ya 3s-GTE saa 6.30 usiku naanza safari nipo sheli ya BP kibaha njuweni hotel ikaja gari ya magazeti ilikuwa ni hiece super custom zile za 1KZ dereva akaniambia dogo naona full tank usiku huu safari ndefu nn nikamwambia hujakosea akasema wapi nikamwambia kaskazini akasema tupo road moja kijana tutembee

bwana weee mashine yangu ilikuwa top end ni 260 kph lakin inabidi niseme wale jamaa huwa barabaran wanajitoa mhangaa nilijua nitawapoteza road ila kila nikikanyaga hawa hapa... ikabidi ilifika wakati nikawaacha wao watangulie mbele japo gari yangu ilikuwa ina top end kubwa kuliko yao ila ujasiri nilikosa
 
Back
Top Bottom