Nakumbuka nilikosa bus za tunduma zinazokwenda dar pale mbeya nanenane
Basi ilibid nisogee adi uyole nikakuta hizo gari za magazet ndio zinataka kurud dar, sasa kuna fundi viatu ndio alinilengesha na nikiiangalia hzo gari yan naona kama ananitania hiv, yan gar hii nitoboe dar ila nikasema haina shda
Safar ikaanza saa 8 kamil mchana ilipigwa gia za kibabe na matrafk weng wanajuana nao so hazina kusimamishwa hzo, iv mnajua gia za kibabe,??? ikabd niwajurulshe ndugu jamaa na marafik wenye mioyo migum kwamba nipo safarin lakn gar ya magazet lolote litakalo tokea wakubaliane na matokeo
Tunafika maeneo ya kibaha kuna mzee alikua karibu yangu ananiambia apo wamepunguza speed, uwakute wanapeleka mzigo
Dar ubungo sheli tunaingia saa 3:30 usku, waliopanda bus saa 12 asubuhi waliniacha masaa mawil iv
Na nilipiga calculation zangu, saa 1 asubuh magazet yanasomwa mbeya sasa jiulize uku dar yanavyotoka saa 6 usiku yanaenda speed gan??
Niliapa hiz gar sipand tena ata nikikutwa na umaut ntaacha wosia huo