Tuliowahi kutembea kwa sababu ya kukosa nauli tukutane hapa

Duh ulienjoy sana mkuu maana kipindi tunasoma hakuna jambo lilikuwa linafurahisha kama kulipiwa nauli au kusamehewa usilipe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Kama nakuona mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aiseee mi nimetembea sana sana, ,halafu bora utembee njia za ndani ndani kuliko main road. Unachoka zaidi, mana magari yanapita unayaona yaleeee
 
Ilikua mwaka 2006 wakati nasoma Tosamaganga Boys, Nilitembea kwa miguu kutoka Iringa Mjini mpaka shuleni Tosa,

Ilikua hivi, kila jumamosi ya mwisho wa mwezi tulikua tunaruhusiwa kutoka nje ya eneo la shule bila ruhusa, kwa kipindi hiko familia yangu ilikua inaishi Iringa Mjini ila kulikua na taarifa za kuhama hama kutokana na Mkwawa Sekondari kuvunjwa ili kiwe chuo (Familia yangu ilikua inaishi pale, Baba yangu alikua Mwalimu pale). Basi mie nikasema ngoja niende Nyumbani nikaangalie nini kinaendelea, nikachukua buku langu na nauli ilikua mia tano tu kutoka Tosa hadi Iringa Mjini, nikalipa ile mia tano nauli wakati wa kwenda nikabaki na mia tano nyingine. Nikafika Iringa Mjini moja kwa moja nikakanyaga hadi Mkwawa kwa mguu maana kuna kama kilomita tatu kutoka Irnga mpaka Mkwawa, nafika nyumbani nakuta peupeee, Familia haipo, nikauliza kwa majirani wakasema wameondoka jana tu kuelekea Morogoro ambapo ndiko Baba alikohamishiwa, da nilipagawa na hapo njaa inauma vibaya. Nikasema sio mbaya hii mia tano ntakula chakula halafu kwenda Tosa ntajikakamua kwenda kwa miguu.
Saa tisa za mchana ndio nikaanza safari ya kuuchapa kwa mguu mpaka Tosa kwa kupitia njia ya Kalenga, sio mchezo maana kuna kama kilomita 22 ,
Nilitembea vibaya mno hadi nikahisi naanguka, Saa 12 na nusu jioni ndio nikaibgia Tosa moja kwa moja nikapitiliza kwenye ugali (sumu).
Kesho yake nilikuaja kuamka saa 6 mchana hata uji sikunywa.
SIO MCHEZO

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tulikuwa na mshkaji wangu,tupo mitaa ya kilombero na mishe mishe,sasa bhana ujanja ujanja nikapiga had nauli jamaa hana kitu,tulitembea kuanzia frence corner hadi kidemi(ngalimi), tunajipa moyo kishenzi eti ni mazoezi kumbe hatuna nauli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mdogo wangu mmoja mtembezi sana, ukitoka nae kwenda kutembea basi ''mnatembea' kweli kweli.. Amenipigisha sana ruti za soko matola-ilemi-mwakibete mbeya na route za sua main campus-jordan university moro. Hafai kabisa kuongozana nae
 
Hapo ni sawa na kutoka kilapula mpka Tanga mjini, duh pole sana japo ilikwishapita.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…