Mtoto halali na hela
JF-Expert Member
- Aug 10, 2012
- 52,160
- 48,974
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sawa mkuuHapana msiondoke bado tuna vitu vingi vya kujifunza kutoka kwenu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Duh ulienjoy sana mkuu maana kipindi tunasoma hakuna jambo lilikuwa linafurahisha kama kulipiwa nauli au kusamehewa usilipe.Nilishaacha mkuu.
Hata sikuwa maarufu sema ni vile vijana wengi ambao nilisoma nao waliachana na shule baada ya kumaliza darasa la saba wengine waliacha secondary wakaingia kwenye ukondacta na udereva wa daladala sasa nilikuwa nikipanda hawanidai wenyewe nauli[emoji23][emoji23][emoji23]. Hata siku nikiwa nayo hawapokei[emoji23][emoji23][emoji23]
The Hate U Give, Little Infants F's Everyone.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Kama nakuona mkuuNakumbuka mwaka 2002 bado niko primary nilitumia hadi pesa ya nauli baada ya kuzidiwa na kiu ya haja kwa uzembe wa kuendekeza kucheza mpira jua likiwa kali kabisa....
Aisee nilitembea siku ile kutoka Mjini na nilipofika maeneo ya kurasini kiu ilinibana tena ikabidi nigonge nyumba za watu kuomba msaada wa maji...
Nilitembea siku ile mpaka nikataka hadi kulia na nilijutia kwanini nilitumia nauli. Tangu siku hyo ikawa nikitoka shule sitaki story na mtu nakimbilia stand kupanda gari.
Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee ilikuwa balaaaaNilitembea kutoka kinondoni mkwajuni hadi ununio na kurudi na sio mara moja acha tu ..staki kukumbuka kabisaaa
Sent using Jamii Forums mobile app
Taifa to Mbagala 10kms[emoji848][emoji848][emoji848]Hahahaha usinikumbushe kuna siku ilipigwa game ya SIMBA NA YANGA... basi natoka taifa ile sina hata buku nkaanza upiga wa mguu hadi mbagala...
Sent using Jamii Forums mobile app
Duh! Aisee, inabidi kwenye nyuzi zetu ili kuchangia muanze na shikamoo kwa mtoa mada[emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787]94 nina aka 4 [emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Ilikuwa ni shida mkuu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Kama nakuona mkuu
Sent using Jamii Forums mobile app
We ulivyosoma umeona swali?
Hapo ni sawa na kutoka kilapula mpka Tanga mjini, duh pole sana japo ilikwishapita.Ilikua mwaka 2006 wakati nasoma Tosamaganga Boys, Nilitembea kwa miguu kutoka Iringa Mjini mpaka shuleni Tosa,
Ilikua hivi, kila jumamosi ya mwisho wa mwezi tulikua tunaruhusiwa kutoka nje ya eneo la shule bila ruhusa, kwa kipindi hiko familia yangu ilikua inaishi Iringa Mjini ila kulikua na taarifa za kuhama hama kutokana na Mkwawa Sekondari kuvunjwa ili kiwe chuo (Familia yangu ilikua inaishi pale, Baba yangu alikua Mwalimu pale). Basi mie nikasema ngoja niende Nyumbani nikaangalie nini kinaendelea, nikachukua buku langu na nauli ilikua mia tano tu kutoka Tosa hadi Iringa Mjini, nikalipa ile mia tano nauli wakati wa kwenda nikabaki na mia tano nyingine. Nikafika Iringa Mjini moja kwa moja nikakanyaga hadi Mkwawa kwa mguu maana kuna kama kilomita tatu kutoka Irnga mpaka Mkwawa, nafika nyumbani nakuta peupeee, Familia haipo, nikauliza kwa majirani wakasema wameondoka jana tu kuelekea Morogoro ambapo ndiko Baba alikohamishiwa, da nilipagawa na hapo njaa inauma vibaya. Nikasema sio mbaya hii mia tano ntakula chakula halafu kwenda Tosa ntajikakamua kwenda kwa miguu.
Saa tisa za mchana ndio nikaanza safari ya kuuchapa kwa mguu mpaka Tosa kwa kupitia njia ya Kalenga, sio mchezo maana kuna kama kilomita 22 ,
Nilitembea vibaya mno hadi nikahisi naanguka, Saa 12 na nusu jioni ndio nikaibgia Tosa moja kwa moja nikapitiliza kwenye ugali (sumu).
Kesho yake nilikuaja kuamka saa 6 mchana hata uji sikunywa.
SIO MCHEZO
Sent using Jamii Forums mobile app