Tuliowahi kuteswa na marejesho ya mkopo tukutane hapa

Dah! Nakumbuka mwaka flani niliwahi kuchukua mkopo kwa hawa jamaa ambao Bond unaweka gari.. aisee sitakaa nisahau, Jamaa wanajua kudai na marejesho yao ni tofauti na makubaliano ya Awali. Ukishindwa kurudisha ndani ya mwezi tu wanakuja kuchukua gari lako ambalo wanakuwa wameshabadilisha Jina.

Aisee hata uwe na shida kiasi gani ndugu yangu usikae ukaenda kwa wale jamaa wa Mkopo kwa dhamana ya Gari
 
Kwa hiyo unataka kugaiwa pesa za baba ako?
 
Mkopo sio zawadi hakikaa
 
 

Attachments

  • 3416317A-E97F-46A5-B0CC-8E62464A2AF4.jpeg
    108.1 KB · Views: 37
Dadangu anafosi nimwandikie barua ya mkopo,
Anakopea kiwanja cha urithi,hii ni mali yetu mimi na yeye....hii pesa nina wasiwasi hatarudisha.
Naandika kesho kuepuka lawama ila najua ili deni nitalipa mimi dadeki.
Una uhakika kuwa hatarudisha lkn unakubali akope.
Mkuu kama upo karibu na Milembe Hospitali, pale Kuna wataalamu wa maradhi yako.
 
Riba yao ikoje??
 
Fanya yote ila usikope ASA
Hahahaa kuna dada nilijiroga nikamchukulia mkopo ASA, ndio mara yangu ya kwanza rejesho moja tuu akasafiri hajarudi mpaka leo na simu inapatikana ila huwa hapokei namba yoyote.

Nilimchukulia 600,000 mwezi wa 5 juzi kati mwezi wa 10 ndio nimemaliza kulipa sina hamu,rejesho ni 28000 kwa wiki ila ukikumbuka unamlipia mtu roho inachafuka. Afisa mikopo ananiuliza lini unachukua tena mkopo huwa namjibu nitakuja tuu hajui maumivu niliyonayo mpaka akiba niliwaachia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi watumishi wa serikali wakikopa wakiacha kazi kabla mkopo kuisha huwa wanatafutwa?

Na kama hawatafutwi na hulipa hela zao?

Na kama wanatafutwa je huwa wanauza mali zao kufidia madeni?
 
ASA ni nini?
 
Hivi watumishi wa serikali wakikopa wakiacha kazi kabla mkopo kuisha huwa wanatafutwa?

Na kama hawatafutwi na hulipa hela zao?

Na kama wanatafutwa je huwa wanauza mali zao kufidia madeni?
Vip unataka uache kaz ukimbie na mkopo? [emoji3]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…