Tuliowahi kuteswa na marejesho ya mkopo tukutane hapa

Tuliowahi kuteswa na marejesho ya mkopo tukutane hapa

Ilikuwa mwaka 2011 mwezi wa 7 mara yangu ya kwanza kuchukua mkopo benki, Tsh 3m. Ule mkopo niliufanyia biashara vizuri na nikarejesha bila changamoto kubwa ndani ya miezi 6. Wale maafisa mikopo wakafurahia na kunishauri nichukue mwingine wa Tsh 5m. Nikafikiria na baada ya mwezi nikachukua mkopo mwingine. Ikawa kama bahati wakati nachukua mkopo nikawa nimepata tenda ya kushona uniform za shule flani. Nikaona hili ni dili zuri na kwa bahati wateja wangu wakanilipa pesa za advance zaidi ya 90%. Kilichofuata nikaamua nitafute mafundi wazuri Nairobi wanishonee uniform zote. HAPA NDO BALAA LILIPOANZA. Niliingia choo cha kike. Mkenya niliyempa kazi kumbe ni mshenzi mno... kadhulumu watu wengi sana. Ni kweli ofisi anayo na mafundi anao ila kwa bahati mbaya huwa hatimizi makubaliano. Ujinga mwingine niliofanya ni kumlipa karibu hela zake zote.

Hadi shule zinafunguliwa Januari sikuwa nimepeleka nguo yoyote kwa mteja. Basi presha ikaanza kutoka kwa mteja wangu ambaye pia alikuwa anawashiwa moto na wanafunzi + wazazi. Baada ya kusumbuana na mzabuni wangu nikaona isiwe ishu nichukue hela za kwenye biashara yangu niliyoombea mkopo wa 5m ili kupambana na tatizo ambalo lilikuwa limefikia pabaya. Kwa maana nitafute fundi mwingine nitengenezee kwake huku nikiendelea kupambana na huyu wa mwanzo. Changamoto iliyojitokeza tena ikawa kwa muda ule wauza uniform wengine wana kazi zingine nyingi na bei zao zimeshaenda juu. Gharama za nauli nenda rudi Ars - Nrb nazo zikawa zinanipiga kama ngoma.

Hadi kuja kufanikiwa kupeleka nguo angalau kwa 70% tayari kiuchumi nilishayumba hivyo marejesho yakawa yanasuasua. Ninachokumbuka ule mkopo niliotakiwa niwe nimemaliza kulipa kabla hata ya August nilimaliza December kwa mafaini kibao huku nikiwa nimefilisika. Wale maafisa mikopo walijua kuniwashia moto.

Pamoja na yote hayo nilijipanga upya na baada ya miaka kama mitatu nilirudi tena benki na kuchukua mkopo. Ninamshukuru Mungu kwamba ninakopesheka na ninaendelea kuchukua mkopo. Somo kubwa ni kwamba usichukue mkopo kuanzisha biashara.
Mikopo,mhhhh.
Nilikopa Saccos moja nikanunua shamba,nikijua mshahara utanisaidia kurejesha chap,duuuu.
Mshahara ukaanza kusuasua,marejesho yakaanza kusumbua.
Mhh,muda wa kulipa ukaisha,daaaaa.saccos wakaanza kunifatilia,acheni wazeee!!
Mungu akanisaidia nikafanya juu chini nikamaliza Deni ,yaani furaha niliyoipata kwa kumaliza deni Ni kubwa Sana.
 
Na sisi tunaodhamini wakopaji tukutane wapi??????
Hili nalo balaa linginee.
Nilimdhamini mfanyakazi mwenzangu kuchukua mkopo kidogo tuu,Mara jamaa akashindwa kurejesha kwa mwezi km ilivyotakiwa

Gafla nikaambiwa inabidi nianze kumlipia ,yaani nikalipa marejesho mwezi mmoja,ikabidi nifanye maarifa boss amkate juu kwa juu Deni likalipwa Ila Mimi nikiwa mhanga,acha tuuu.
Sitakuwa mwepesi kumdhamini mtu tena
 
Hahaahah
Mimi nilikua afisa wa mikopo kwenye microfinance moja ivi nikaacha nikaingia mtaani kwenye biashara nilichofanyiwa na mikopo sina hamu, alikuja afisa mikopo juzi kunishauri nikakope kwao nimeishia kumtolea panga
Kausha damu
Usiombe uchukue mkopo wa KAUSHA DAMU...wanakupa leo kesho unaanza marejesho mfululizo mpaka utapomaliza kina mama wamekauka huko mitaani sio poa
 
Kuna ka benki kamoja mkopo wake hauishi kabisa.
Ukimaliza deni wanakuja tulisahau kukata faida.
Ukimaliza wanakuja tena, tulisahau kukata bima
Ukimaliza wanakuja tena, tulisahau kukata kapacity charge
Ukimaliza wanakuja tena, mahesabu ya kwanza yalikosewa.

Ukimaliza deni huambiwi umemaliza, baada ya miezi mitatu wanakuja tena yaani madeni yake hayaishi.

Jamani mimi sijataja jina la benki yoyote, walio yakuta wanaijua.

Nimeacha kabisa kukopa tena benki.
kama sio letshgo sijui
walifanya upuuzi huu kwa mke wangu nikawapandia hewani siku hiyo wakatuma statement ya bank ya marejesho ikaonekana deni limeisha walikuwa wanafanya uhuni
 
Back
Top Bottom