Tuliowahi kuteswa na marejesho ya mkopo tukutane hapa

Tuliowahi kuteswa na marejesho ya mkopo tukutane hapa

Aisee hii mikopo iko nzuri na mibaya, nilishawai kuchukuwa M10 za mkopo hapo sikujua namna ya kurejesha maana ilikuwa haraka haraka siku yule jamaa ananipa utaratibu wa kurejesha niliishiwa nguvu, maana nilitakiwa nilipe jumla ya M16 kwa miezi sita, cha kustaajabu hela yote niliijengea, nyumba nikaiuza nikageuka mpangaji kwenye hiyo nyumba, alienunua hiyo nyumba nae akanipa notisi niachie nyumba yake.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Andika tujifunze mwanawane

Kifupi nikopa NMB 10ml nialipa marjesho kama 6 biashara ikaanza kuyumba.aisee nilihangaika huku na huko nyumba isiuzwe bila mafanikio.mwisho niliongea na marafiki zangu wanimlizie deni then mambo yakiwa mazuri niwarejeshee wao badala ya benk,hivyo nilipigwa tough kama 4ml nikaokoa nyumba yangu..sasa deni limehamia kwa washkaji ndo mziki upo hapo.Mungu nisaidie
 
Pole sana. Mikopo nyoko
 
Karibuni MABENA FINANCIAL SERVICES TUPO NCHI NZIMA KILA WILAYA MKOPO CHAP RIBA 20% dhamana Ni vitu vya ndani
Duh riba 20%, tax 30%, bima, matozo etc hivi inawekana vipi kufanya biashara kwa kutumia pesa ya mkopo bongo? unaweza kufikiri ufisadi na rushwa ndio vinatufanya tuwe masikini na biashara zishindikane kumbe huku napo ni worse kuliko maelezo, kwa riba kama hizi, tax na matozo nchi itaendelea kuwa maskini kwa muda mrefu sana
 
Nina ndugu yangu anafanya buashara ya nguo, alifanikiwa kupata hela kidogo akajenga nyumba kali ya kisasa na usafir binafs, badae akaja kuyumba kuchumi nadhani alijusahau akatumia mpaka mtaji kwenye ujenzi.

Sasa akaenda kukopa milion 50 bank aongeze mtaji wa biashara,kwenye biashara ikakatika yote ile hela aisee alitaka kuchizi.

Deni lilibaki kama mil 17 na muda wa kurejehesha ulibaki mchache sana yaan alikonda kiufup alifirisika kabsa hata buku akawa hana. Alikata tamaa akisubiri nyumba iuzwe.

Bahati nzuri kuna jamaa yake mmoja alikua anampaga mzigo walikutana akamuelezea hali ilivyo yule jamaa wakaenda nae Bank akamlipia yote ndo ikawa bahati ya kutouziwa nyumba.
 
Aisee hii mikopo iko nzuri na mibaya, nilishawai kuchukuwa M10 za mkopo hapo sikujua namna ya kurejesha maana ilikuwa haraka haraka siku yule jamaa ananipa utaratibu wa kurejesha niliishiwa nguvu, maana nilitakiwa nilipe jumla ya M16 kwa miezi sita, cha kustaajabu hela yote niliijengea, nyumba nikaiuza nikageuka mpangaji kwenye hiyo nyumba, alienunua hiyo nyumba nae akanipa notisi niachie nyumba yake.
[emoji1787][emoji23]
 
Afisa mikopo wa .......... Microfinance. Wewe zingua rejesho nije nikuchafulie pande nne za nyumba yako
IMG_20221129_200750.jpg
 
Kuna kikampuni hapo dodoma kinakopesha kwa dhamana ya kiwanja, chombo cha moto, ama nyumba, muhimu uwe mmiriki halali, watafute hao, uwapige hela, ukishindwa kurudisha wanachukua chako kinakuwa chao, unakuwa kama umeuza mali na kupata pesa...THE DEAL DONE, hivyo ndivyo maharamia tulifanya biashara bila kuhangaika na wateja[emoji16][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Umenipa akili wanaitwaje??
 
Ilikuwa mwaka 2011 mwezi wa 7 mara yangu ya kwanza kuchukua mkopo benki, Tsh 3m. Ule mkopo niliufanyia biashara vizuri na nikarejesha bila changamoto kubwa ndani ya miezi 6. Wale maafisa mikopo wakafurahia na kunishauri nichukue mwingine wa Tsh 5m. Nikafikiria na baada ya mwezi nikachukua mkopo mwingine. Ikawa kama bahati wakati nachukua mkopo nikawa nimepata tenda ya kushona uniform za shule flani. Nikaona hili ni dili zuri na kwa bahati wateja wangu wakanilipa pesa za advance zaidi ya 90%. Kilichofuata nikaamua nitafute mafundi wazuri Nairobi wanishonee uniform zote. HAPA NDO BALAA LILIPOANZA. Niliingia choo cha kike. Mkenya niliyempa kazi kumbe ni mshenzi mno... kadhulumu watu wengi sana. Ni kweli ofisi anayo na mafundi anao ila kwa bahati mbaya huwa hatimizi makubaliano. Ujinga mwingine niliofanya ni kumlipa karibu hela zake zote.

Hadi shule zinafunguliwa Januari sikuwa nimepeleka nguo yoyote kwa mteja. Basi presha ikaanza kutoka kwa mteja wangu ambaye pia alikuwa anawashiwa moto na wanafunzi + wazazi. Baada ya kusumbuana na mzabuni wangu nikaona isiwe ishu nichukue hela za kwenye biashara yangu niliyoombea mkopo wa 5m ili kupambana na tatizo ambalo lilikuwa limefikia pabaya. Kwa maana nitafute fundi mwingine nitengenezee kwake huku nikiendelea kupambana na huyu wa mwanzo. Changamoto iliyojitokeza tena ikawa kwa muda ule wauza uniform wengine wana kazi zingine nyingi na bei zao zimeshaenda juu. Gharama za nauli nenda rudi Ars - Nrb nazo zikawa zinanipiga kama ngoma.

Hadi kuja kufanikiwa kupeleka nguo angalau kwa 70% tayari kiuchumi nilishayumba hivyo marejesho yakawa yanasuasua. Ninachokumbuka ule mkopo niliotakiwa niwe nimemaliza kulipa kabla hata ya August nilimaliza December kwa mafaini kibao huku nikiwa nimefilisika. Wale maafisa mikopo walijua kuniwashia moto.

Pamoja na yote hayo nilijipanga upya na baada ya miaka kama mitatu nilirudi tena benki na kuchukua mkopo. Ninamshukuru Mungu kwamba ninakopesheka na ninaendelea kuchukua mkopo. Somo kubwa ni kwamba usichukue mkopo kuanzisha biashara.
😂😂😂Ety unakopesheka.
 
Nina ndugu yangu anafanya buashara ya nguo, alifanikiwa kupata hela kidogo akajenga nyumba kali ya kisasa na usafir binafs, badae akaja kuyumba kuchumi nadhani alijusahau akatumia mpaka mtaji kwenye ujenzi.

Sasa akaenda kukopa milion 50 bank aongeze mtaji wa biashara,kwenye biashara ikakatika yote ile hela aisee alitaka kuchizi.

Deni lilibaki kama mil 17 na muda wa kurejehesha ulibaki mchache sana yaan alikonda kiufup alifirisika kabsa hata buku akawa hana. Alikata tamaa akisubiri nyumba iuzwe.

Bahati nzuri kuna jamaa yake mmoja alikua anampaga mzigo walikutana akamuelezea hali ilivyo yule jamaa wakaenda nae Bank akamlipia yote ndo ikawa bahati ya kutouziwa nyumba.
Kuishi na watu vizuri inasaidia sana. Huwezi kosa hata mmoja wa kukuokoa
 
Back
Top Bottom