Tuliowahi kuteswa na marejesho ya mkopo tukutane hapa

Dadangu anafosi nimwandikie barua ya mkopo,
Anakopea kiwanja cha urithi,hii ni mali yetu mimi na yeye....hii pesa nina wasiwasi hatarudisha.
Naandika kesho kuepuka lawama ila najua ili deni nitalipa mimi dadeki.
Afadhali umejua mapema hivo umejipanga ili hata huko mbeleni wala hutonung'unika kwakuwa ulishaona mbele.
 
Rejesho 5.8m kwa mwezi nadhani mi mngenizika kabisa.
 
Funzo lingine usichukue mkopo kusolve ishu zako binafsi[emoji1787][emoji1787] hi nitakuja kuleta ushuhuda
 
Inachekesha[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Niliuza laptop kwa mazingira haya haya[emoji3][emoji3][emoji3] kipindi nipo chuo
 
Inachekesh pia[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mkuu UGM BIN CHAMPION ni Kampuni gani hiyo ya DODOMA na Ofisi zao zipo wapi??naomba direction au contact zao
Imarika, jengo la haloteli, opposite na nyerere square barabara ya kutokea NMB kwenda ilipokuwa maisha Club.

Au kama unakijua kibarabara ambacho machinga walikuwa wanamwaga nguo za mtumba kuuza jioni nyerere square.

Kampuni ya Kina Frank mtei na mkewe nadhani.
 
On the otherside of the story: Kwa wakopeshaji, Kuna shost anaishi huko uswahilini kazi yake kukopesha wamama. Sasa kuna muda anaumwa sana ukimuuliza anasema wakopaji wanamloga asahau madeni πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…

Akaanza kwenda kwa mganga na yeye kujiweka fit, Mwisho ameolewa na mganga siku hizi na biashara yake ya kukopesha anaendelea nayo.
 
Me haya mambo namdhamini mama yangu tu...... Nje ya hapo asante kwa kushiriki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…