Tuliowahi kuteswa na marejesho ya mkopo tukutane hapa

Tuliowahi kuteswa na marejesho ya mkopo tukutane hapa

Dadangu anafosi nimwandikie barua ya mkopo,
Anakopea kiwanja cha urithi,hii ni mali yetu mimi na yeye....hii pesa nina wasiwasi hatarudisha.
Naandika kesho kuepuka lawama ila najua ili deni nitalipa mimi dadeki.
Afadhali umejua mapema hivo umejipanga ili hata huko mbeleni wala hutonung'unika kwakuwa ulishaona mbele.
 
Mimi mkopo ulichonifanya sitokaa nikope milele mpk naingia kaburin
Nitaridhika na ninachopata
Bora sahiz nasave hela naiona aisee
Mkopo ulikuwa unifirisi kabisa
Ila afsa mkopo ni mbwa hawana huruma
Rejesho mil 5.8 kwa mwez halaf sikuwa mzoefu wa mikopo hata kunishaur nisogeze mbele mkopo ilo marejesho yapungue wakashindwa wakaniacha nakufa na tai shingon mbwa wale sitowasahau kamwe
Rejesho 5.8m kwa mwezi nadhani mi mngenizika kabisa.
 
Ilikuwa mwaka 2011 mwezi wa 7 mara yangu ya kwanza kuchukua mkopo benki, Tsh 3m. Ule mkopo niliufanyia biashara vizuri na nikarejesha bila changamoto kubwa ndani ya miezi 6. Wale maafisa mikopo wakafurahia na kunishauri nichukue mwingine wa Tsh 5m. Nikafikiria na baada ya mwezi nikachukua mkopo mwingine. Ikawa kama bahati wakati nachukua mkopo nikawa nimepata tenda ya kushona uniform za shule flani. Nikaona hili ni dili zuri na kwa bahati wateja wangu wakanilipa pesa za advance zaidi ya 90%. Kilichofuata nikaamua nitafute mafundi wazuri Nairobi wanishonee uniform zote. HAPA NDO BALAA LILIPOANZA. Niliingia choo cha kike. Mkenya niliyempa kazi kumbe ni mshenzi mno... kadhulumu watu wengi sana. Ni kweli ofisi anayo na mafundi anao ila kwa bahati mbaya huwa hatimizi makubaliano. Ujinga mwingine niliofanya ni kumlipa karibu hela zake zote.

Hadi shule zinafunguliwa Januari sikuwa nimepeleka nguo yoyote kwa mteja. Basi presha ikaanza kutoka kwa mteja wangu ambaye pia alikuwa anawashiwa moto na wanafunzi + wazazi. Baada ya kusumbuana na mzabuni wangu nikaona isiwe ishu nichukue hela za kwenye biashara yangu niliyoombea mkopo wa 5m ili kupambana na tatizo ambalo lilikuwa limefikia pabaya. Kwa maana nitafute fundi mwingine nitengenezee kwake huku nikiendelea kupambana na huyu wa mwanzo. Changamoto iliyojitokeza tena ikawa kwa muda ule wauza uniform wengine wana kazi zingine nyingi na bei zao zimeshaenda juu. Gharama za nauli nenda rudi Ars - Nrb nazo zikawa zinanipiga kama ngoma.

Hadi kuja kufanikiwa kupeleka nguo angalau kwa 70% tayari kiuchumi nilishayumba hivyo marejesho yakawa yanasuasua. Ninachokumbuka ule mkopo niliotakiwa niwe nimemaliza kulipa kabla hata ya August nilimaliza December kwa mafaini kibao huku nikiwa nimefilisika. Wale maafisa mikopo walijua kuniwashia moto.

Pamoja na yote hayo nilijipanga upya na baada ya miaka kama mitatu nilirudi tena benki na kuchukua mkopo. Ninamshukuru Mungu kwamba ninakopesheka na ninaendelea kuchukua mkopo. Somo kubwa ni kwamba usichukue mkopo kuanzisha biashara.
Funzo lingine usichukue mkopo kusolve ishu zako binafsi[emoji1787][emoji1787] hi nitakuja kuleta ushuhuda
 
Aisee hii mikopo iko nzuri na mibaya, nilishawai kuchukuwa M10 za mkopo hapo sikujua namna ya kurejesha maana ilikuwa haraka haraka siku yule jamaa ananipa utaratibu wa kurejesha niliishiwa nguvu, maana nilitakiwa nilipe jumla ya M16 kwa miezi sita, cha kustaajabu hela yote niliijengea, nyumba nikaiuza nikageuka mpangaji kwenye hiyo nyumba, alienunua hiyo nyumba nae akanipa notisi niachie nyumba yake.
Inachekesha[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kuna kikampuni hapo dodoma kinakopesha kwa dhamana ya kiwanja, chombo cha moto, ama nyumba, muhimu uwe mmiriki halali, watafute hao, uwapige hela, ukishindwa kurudisha wanachukua chako kinakuwa chao, unakuwa kama umeuza mali na kupata pesa...THE DEAL DONE, hivyo ndivyo maharamia tulifanya biashara bila kuhangaika na wateja[emoji16][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Niliuza laptop kwa mazingira haya haya[emoji3][emoji3][emoji3] kipindi nipo chuo
 
Pole sana mzee ulijipiga bomu mwenyewe.....Just imagine umenunua kiwanja umeanza ujenzi,nyumba yako inakamilika halafu ghafla unageuka mpangaji kwenye nyumba uliyoisotea kuijenga halafu mwisho wa siku unatimuliwa kwenye nyumba yako.
Daah inachoma kama pasi hii mzee [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Inachekesh pia[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mkuu UGM BIN CHAMPION ni Kampuni gani hiyo ya DODOMA na Ofisi zao zipo wapi??naomba direction au contact zao
Imarika, jengo la haloteli, opposite na nyerere square barabara ya kutokea NMB kwenda ilipokuwa maisha Club.

Au kama unakijua kibarabara ambacho machinga walikuwa wanamwaga nguo za mtumba kuuza jioni nyerere square.

Kampuni ya Kina Frank mtei na mkewe nadhani.
 
On the otherside of the story: Kwa wakopeshaji, Kuna shost anaishi huko uswahilini kazi yake kukopesha wamama. Sasa kuna muda anaumwa sana ukimuuliza anasema wakopaji wanamloga asahau madeni 😅😅😅😅😅

Akaanza kwenda kwa mganga na yeye kujiweka fit, Mwisho ameolewa na mganga siku hizi na biashara yake ya kukopesha anaendelea nayo.
 
Hili nalo balaa linginee.
Nilimdhamini mfanyakazi mwenzangu kuchukua mkopo kidogo tuu,Mara jamaa akashindwa kurejesha kwa mwezi km ilivyotakiwa

Gafla nikaambiwa inabidi nianze kumlipia ,yaani nikalipa marejesho mwezi mmoja,ikabidi nifanye maarifa boss amkate juu kwa juu Deni likalipwa Ila Mimi nikiwa mhanga,acha tuuu.
Sitakuwa mwepesi kumdhamini mtu tena
Me haya mambo namdhamini mama yangu tu...... Nje ya hapo asante kwa kushiriki
 
Back
Top Bottom