Tuliowahi kuteswa na marejesho ya mkopo tukutane hapa

Mzee wenu anawadanganya,kwanza wanafacitate malipo ni NSSF/PSSSF hazina Nazi yao ni kutoa hela tu.hata kama mstaafu hajahakikiwa hela wanamuingizia kama kawaida.
 

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]aisee hatari
 
Aisee. Kama naiyona familia yake inayo pitia kwa sasa,[emoji26]
 
Mara nyingi huwa wanakopa Hela kwenda kwenye mitikasi iliyo riski sana. Mfano madini.
 
hii mikopo kausha damu balaa sana mam yangu alichukua pesa kidogotu kama laki tatu hivi kila siku analipa 5 elfu amekauka apa na mkopo hauishi anafanya kulipa faini tu mkopo upo pale pale Ni huzuni kwa kweli nimeuza mpaka kitanda kumsaidia
 
daah mkopo ulinifanya niwe mpangaji kutoka kuwa baba mwenye nyumba

mkopo ulinifanya nitembee barabarani nikiwa naongea peke yangu bila kusahau hasira zisizokwisha kwa watu wakaribu
Mikopo Ni nyoko Moja matata.Kuna dada alikuwa ananisimulia jinsi nyumba Yao ilipigwa mnada na mikopo chechefu mama Yao alikopeaga..

Sasa Ni wapangaji na mama ana kisukari huyo dada Hana kazininayoeleweka na ana familia Hana mume..

Alikuwa kaingia kingi baada Kupigwa mistari Sasa nilipanga nimpe 15,000 tuu baada ya jumla Ila alivyonisimulia msala nikamwambia wazi kwamba nakusaidia kwa50,000 baada ya hapo Nika block na namba..

Binafsi huwa naogopa mikopo na kama nitakopa Basi mkopo usizidi nusu ya kiwango changu Cha mapato kwa mwezi na hata kukopesha naogopa maana uwezekano wa kulipwa Ni mdogo Sana.
 
Jamani mie nina emergency nimetoka kufiwa na Dada yangu asubuhi ya Leo,Nina shida ya mkopo wa Shilingi laki 3 kwa dhamana laptop yenye thamani ya 1.8M. Nitarajesha pesa hiyo kabla ya tarehe 25 ya mwezi huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…