Tuliowahi kuteswa na marejesho ya mkopo tukutane hapa

Tuliowahi kuteswa na marejesho ya mkopo tukutane hapa

Mkuu mimi Mzazi wangu kakopa pesa Banki lakini kwa marejesho ya banki kukata kwenye pensheni yake sasa pensheni yake Azina hawaja muingizia benki miezi 4 imefika sasa Afisa mikopo wa Banki ana tusumbua sisi watoto tumpeleke mzee wetu Azina akahakikiwe, Mimi nimekataa simpeleke kwasababu pesa alivyokopa haja tugaiya kaitumia peke yake, sasa hatujui afisa mikopo wa benki atazipataje pesa zaidi ya Milioni 10

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
Mzee wenu anawadanganya,kwanza wanafacitate malipo ni NSSF/PSSSF hazina Nazi yao ni kutoa hela tu.hata kama mstaafu hajahakikiwa hela wanamuingizia kama kawaida.
 
On the otherside of the story: Kwa wakopeshaji, Kuna shost anaishi huko uswahilini kazi yake kukopesha wamama. Sasa kuna muda anaumwa sana ukimuuliza anasema wakopaji wanamloga asahau madeni [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]

Akaanza kwenda kwa mganga na yeye kujiweka fit, Mwisho ameolewa na mganga siku hizi na biashara yake ya kukopesha anaendelea nayo.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]aisee hatari
 
Haya sasa nawapa kisa
Huyu mzee wa makamo (around 49 au 50 hivi) alikuwa moja ya wenye maduka makubwa sana ya vitu vya ndani jumla na reja reja. Aliwekeza kwenye majengo akawa na nyumba za wapangaji na yake ya kuishi. Kifupi milioni 20 hadi 40 hivi za mzunguko wa biashara tu zilikuwa hakosi bado mishe zingine za kumuingizia hela.
Huku na huku sijui alipata pepo gani lilomtuma aende benk kukopa tumilion kadhaa dhamana zikiwa mali zake iliwemo duka, na nyuma zake zote (hazipungui 3 au 4 hivi).
Baada ya mkopo mambo yakaenda ndivyo sivyo watu wa benk wanataka Chao.
Akawa anakopa watu ili akimbizane na kasi ya bank....
Harakati zote hizi zikagonga mwamba mali zake zikapigwa mnada.
Kukwepa aibu akakimbilia shinyanga akaanza biashara ya kuuza mchele wa reja reja kwa kupewa kamtaji kadogo na mama yake mzazi baada ya kuuza shamba lake huko killage (kijijini).
Muda wote akawa mtu wa mawazo hadi akili zikachanganya akafariki..lakini hadi anafariki anaongelea mali zake na utajiri wake ulioteketea...

Kwa hiyo wandugu mikopo ni mizuri lakini ikikugeuka utaomba poo
Aisee. Kama naiyona familia yake inayo pitia kwa sasa,[emoji26]
 
Mara nyingi huwa wanakopa Hela kwenda kwenye mitikasi iliyo riski sana. Mfano madini.
 
hii mikopo kausha damu balaa sana mam yangu alichukua pesa kidogotu kama laki tatu hivi kila siku analipa 5 elfu amekauka apa na mkopo hauishi anafanya kulipa faini tu mkopo upo pale pale Ni huzuni kwa kweli nimeuza mpaka kitanda kumsaidia
 
daah mkopo ulinifanya niwe mpangaji kutoka kuwa baba mwenye nyumba

mkopo ulinifanya nitembee barabarani nikiwa naongea peke yangu bila kusahau hasira zisizokwisha kwa watu wakaribu
Mikopo Ni nyoko Moja matata.Kuna dada alikuwa ananisimulia jinsi nyumba Yao ilipigwa mnada na mikopo chechefu mama Yao alikopeaga..

Sasa Ni wapangaji na mama ana kisukari huyo dada Hana kazininayoeleweka na ana familia Hana mume..

Alikuwa kaingia kingi baada Kupigwa mistari Sasa nilipanga nimpe 15,000 tuu baada ya jumla Ila alivyonisimulia msala nikamwambia wazi kwamba nakusaidia kwa50,000 baada ya hapo Nika block na namba..

Binafsi huwa naogopa mikopo na kama nitakopa Basi mkopo usizidi nusu ya kiwango changu Cha mapato kwa mwezi na hata kukopesha naogopa maana uwezekano wa kulipwa Ni mdogo Sana.
 
Jamani mie nina emergency nimetoka kufiwa na Dada yangu asubuhi ya Leo,Nina shida ya mkopo wa Shilingi laki 3 kwa dhamana laptop yenye thamani ya 1.8M. Nitarajesha pesa hiyo kabla ya tarehe 25 ya mwezi huu.
 
Back
Top Bottom