Tuliowahi kuteswa na marejesho ya mkopo tukutane hapa

Wanawake ndo wanaongoza kuchukua mikopo ya hovyo isiyo na kichwa wala miguu.

Na hela huioni.
Mbaya zaidi asilimia kubwa ya wanawake wanachukua mikopo bila kuwa na source ya kueleweka ya kipato

Sasa unategemea atalipaje huyo
 

Hata mimi nilianza na mkopo wa milioni 3, ikapanda hadi 5 nikapandisha hadi 7 nikaja nikakopa 10 ila sasa hivi kwenye hii 14 biashara zimechange kidogo mwaka huu ila natumaini tutamalizana vizuri ila miezi 7 iliyobaki ni mingi
 
Futa hii comment haraka sana..... Uta tapeliwa mda c mrefu

Sent from my M2010J19SI using JamiiForums mobile app
 
Pole mkuu kwa msiba tujitahid kukata Bima za msiba NMB Wana hi huduma ya mkono wa pole .....Kuna kifurushi Cha 500
Elezea vizuri ili watu tujue na tuelewebbroo
 
Na kwa sisi tunaokopa sehemu ya kazi tusemaje?
Yaani unajipangia mwenyewe mwezi huu nisikatwe mpaka mwezi ujao.
 
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]

#MaendeleoHayanaChama
 
Mimi nilikopa milioni 8 ada na meals. Nikanunua kiwanja 3m. Nyingine matumizi kidogo na ada. Kile kiwanja nilichonunua miaka 12 nyuma leo thamani yake ni 50m.
HESLB nawalipa kila mwezi hela yao 30,000.

Asante sirikali.
Muongo ww
 
hii mikopo kausha damu balaa sana mam yangu alichukua pesa kidogotu kama laki tatu hivi kila siku analipa 5 elfu amekauka apa na mkopo hauishi anafanya kulipa faini tu mkopo upo pale pale Ni huzuni kwa kweli nimeuza mpaka kitanda kumsaidia
Mwambie aache, hawawezi kumshtaki sababu wengi hawana vibali maalum
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Usikope hela kuanzisha biashara. Aiseee usithubutu mkuu
-Usikope kuanzisha biashara
-Usikope kujenga

Nyinyi hivi vitu mnafanya kwa pesa ipi?

Tatizo mnashauri kwa jumla,nachojua sio kila mmoja ataishi bila kukopa labda huo ushauri wenu mnashauriana wafanyabiashara, mtumishi asipokopa ili kujenga akaibe? Maana vimishahara vyenyewe uchwara
 
Sasa wewe mtumishi KOPA alafu kaanzishe biashara usiyoijua. Kwanza na utumishi wako utaisimamia saa ngapi? Labda ukae na wataalamu wakuelekeze
 
Maza alikosea kukupiga hukuwa na kosa, alitakiwa kulipa tu hilo deni
 
Watumishi wengi wao kuto kujenga ni uzembe wao tu kwasababu watumishi wengi wa Serikali upata kazi wakiwa vijana wadogo kwaiyo miaka mingi wana kubwa free hawa majukumu na pesa zao uishia kwenye starehe tu, mfano kijana ana miaka 24 kapata kazi ya ualimu ndani ya miaka 5 utakuta hana kiwanja na haja fanya lolote zaidi ya kuonga na kulewa bas
 
Binafsi huwa nakopa hiyo mnaita mkopo umiza au kausha damu,napenda hiyo kwa sababu haina muda wa kukamilisha malipo tofauti na hiyo mingine.

Ila tuu huwa nakopa sio zaidi ya 1M kujazia tuu,uzuri unakopa kwa mtu..

Mwisho sipendi mikopo hata kidogo nilishazoea saving,ukiona nimekopa ujue Nina uhakika wa kurudisha hiyo Pesa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…