Tuliowahi kuwa na chawa tukutane hapa

Tuliowahi kuwa na chawa tukutane hapa

sio chawa za ukubwani chawa za utotoni, haikumaanisha uchafu la hasha ilikuwa ni hali ya kawaida iliyowatokea watoto wengi tulio ishi vijijini. na je Kunguni kitandani na mvua ikinyesha nyumba ina vuja visehem sehem sasa ikivuja kitandani ndio mnahama kabisa na je kulalia godoro la sufi kwenye kitanda kilicho sukwa cha miti au ulienda kwa babu yako akakuachia kitanda mjukuu yeye akatandika majani chini ili ninyi mlale. wote wa mjini hawana experience hii umeme ukikatika wanalalamika ni kweli walizaliwa nao na wakakua nao sisi huwa hatuhangaiki wakikata tunaona kawaida kwanza ndio tunaona matumizi yanapungua sana.
Nyumba inavuja unategeshea sufuria ya kupikia ugali! Umeme unakatika wewe wala shida hamna unawasha mshumaa wako!
 
kunguni ni noma yule msela anajua kula na kipofu ....akiona unafurukuta tu anatuliza ball yaani anakuwa ameshajua kuwa amekupa vitu hivyo anasubiria tena upate usingizi ili aendeleze mechi
Hahahah msela mavi sana kunguni
 
kunguni ni noma yule msela anajua kula na kipofu ....akiona unafurukuta tu anatuliza ball yaani anakuwa ameshajua kuwa amekupa vitu hivyo anasubiria tena upate usingizi ili aendeleze mechi
afadhali kumbe unawajua kunguni kwa undani zaidi lol bigup ntakurushia vocha mwanangu uko vizuri
 
Hebu weka picha
b2dc70a5ca6f5f3bc47dafd2a562f97e.jpg
 
Back
Top Bottom