Watanzania huwa tuna asili ya kuwapenda sana viongozi wetu japo baadhi huutumia upendo huu vibaya kwa kujinufaisha wao binafsi. Viongozi watupende kwanza hasa sisi wananchi wa hali ya chini (wanyonge), wavae viatu vyetu kama alivyokuwa anafanya Hayati JPM, wahangaike kuhakikisha hali ya maisha inakuwa nafuu hasa kwa watu wa hali ya chini, watangulize uzalendo katika suala la kusaini mikataba juu ya raslimali za nchi yetu kwa kuhakikisha inawanufaisha Watanzania wote n.k. Hapo, upendo wetu kwa nchi yetu na viongozi wetu akiwemo Rais, utakuja "automatically".