Tulipofika: mbegu ya chuki inapandwa, umma unachezeshwa, na hatari ina tengenezwa, hatua za haraka zichukuliwe!

Rijali jandoni

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2018
Posts
2,174
Reaction score
2,265
Yanayo andikwa huko mitandaoni, binafsi nabaki katika mawazo kutokana na kuwa muumini wa Tanzania yenye upendo, amani na utulivu, lakini yalio pelekea yote haya kwa vijana ni chuki ilio jengwa kidogo na kisha kukomaa kutokana na vitendo ama matukio yalio kosa majibu, hili la sasa (upandikizaji wa chuki, na umma kulishwa taarifa zisizo thibitishwa hasa kwenda vyombo vya usalama) ni hatari zaidi na linaweza kosa utatuzi wa haraka?

Hili linajengwa kwa kasi sana, lisipo pata hatua za utatuzi wa haraka kuna uwezekano wa vijana kuanzisha vikundi na kisha kuzaa ugaidi, japo sijatambua vitakuwa na mlengo gani?, pili wananchi wanaweza kuchochewa na kisha kuhitaji majeshi ama taasisi za nchi za magharibi kuingilia kati, hii ni hatari na nimeisikia lina zungumzwa

Hili la pili sina nia ya kupinga fikra wala mawazo ya watu nimeona mtandaoni mtu au watu ana shauri kama inawezekana serikali iingie makubaliano na taifa moja la magharibi kutuliza hali, hili ni sawa kweli wakuu? Tukiangalia wananchi waliingia barabarani wakiwa na imani ya kulindwa kwa namna moja walipewa hilo, lakini likaja swala la wao kuuliwa, kisha taarifa tofauti zilisambaa zikihusisha viongozi wa taasisi kutokuwezesha waandamanaji walicho hitaji, sasa imefika hatua taasisi moja inataka ipewe lawama haijafanya kazi kama ilivyo kuwa mategemeo ya watu

Wasiwasi wangu ni baada ya haya yote, namna gani itatumika kutuliza jamii na watu wa kawaida?, hawa vijana wakirudi kuna uwezekano wakafanya mambo nnje ya utaratibu tulio zoea , chuki inayo jengwa kwenda vyombo vya usalama sio ya kupuuzwa, kwa namna fulani watu wana aminishwa taasisi na vyombo vya usalama havipo kwa ajili ya wananchi, wanawaza vijana wapate ama kupatiwa vifaa vya kujilinda ili kukabliana na wanao wazuia hii ni hatari kubwa sana. Upendo urudi sijui ni kwa namna gani ila tuna hitaji utaratibu usio na athari kwa pande zote na ikiwezekana hotuba ya kuliponya Taifa iwepo, sio baada ya miezi huu mbuyu usikomae wakuu, hapo mbele utakuwa mkubwa ila iwepo namna nzuri ya kuliendea jambo

Nimekaa na watu mataifa karibia yote Afrika,naweza thibitisha kwa kusema, hakuna watu hatari na wenye roho ya visasi kama watanzania, hawaoneshi hasira kama mataifa mengine, ila wanaweka vinyongo bila ya kulalamika lakini siku wakitoa ya moyoni huwa wanajenga na chuki ya moja kwa moja ni wagumu kusamehe, ninalo omba hawa vijana kwa wazee wasije chukia hizi taasisi sijui tutakuwa katika hali gani?

Mungu Ibariki Tanzania
 
Jeshi la police linavyozidi kukaa kimya ndio linamalizia chembe ya Imani ndogo iliyobakia
Linatakiwa kutoka hadharani na kukiri ukweli huu sio wakati wa sisi kudanganyana tena
 
Too late, Lazima walipe kwa ukatili waliofanya.
Tuombe upendo na utulivu mkuu, likitokea jingine sidhani kama litakuwa zuri, ama katika hali kama ya sasa

We might be late ila hekima itumike, hekima ni uwezo wa kuweka usawa kwa pande zote mbili, anae ona yupo sahihi akaweza msikiliza mwingine na kwanini limetokea, na atakae dhani ana makosa akaweza kuelewa na kuwa sehemu ya utatuzi

Hekima na uelewa unahitajika kwa sasa, ni ngumu kupambana na governing power, ikitumika nguvu yenye mlingano sijui itakuaje!
 
Tuombe upendo na utulivu mkuu, likitokea jingine sidhani kama litakuwa zuri, ama katika hali kama ya sasa

We might be late ila hekima itumike, hekima ni uwezo wa kuweka usawa kwa pande zote mbili, anae ona yupo sahihi akaweza msikiliza mwingine na kwanini limetokea, na atakae dhani ana makosa akaweza kuelewa na kuwa sehemu ya utatuzi

Hekima na uelewa unahitajika kwa sasa, ni ngumu kupambana na governaing power, ikitumika nguvu yenye mlingano sijui itakuaje!
Tunakoelekea pasipo busara kutumika, wananchi wengi watakuwa wana bear arms kwa rate isiyotarajiwa.
 
Wamesema waliokufa sio Watanzania
Hili ni zito mkuu, hekima itumike, nadhani watu wamepoteza ndugu aidha walikuwa wananchi au maafisa wa vyombo vya usalama kikubwa upendo,hekima na faraja ndio inayo hitajika
 
Tunakoelekea pasipo busara kutumika, wananchi wengi watakuwa wana bear arms kwa rate isiyotarajiwa.

Kabisa mkuu, japo hatujitaji kufika huku wengi wanapo fikiria wanamchi kumiliki hivyo vifaa, swali ni kwamba what next kama kila kitu kitakaa sawa na jamii ina hivyo vifaa?

Ingewekwa elimu ya kwamba ukiachana na maswala ya uchumi na mfumo wa kimaisha basi amani ni kitu kinacho ainisha ama kufanya utambuzi wa jamii ilio endelea na yenye ustaarabu

Na ukija hapo basi utaweza tambua sote tunahitaji kufika katika uelewa mmoja
 
Tuombe upendo na utulivu mkuu, likitokea jingine sidhani kama litakuwa zuri, ama katika hali kama ya sasa

We might be late ila hekima itumike, hekima ni uwezo wa kuweka usawa kwa pande zote mbili, anae ona yupo sahihi akaweza msikiliza mwingine na kwanini limetokea, na atakae dhani ana makosa akaweza kuelewa na kuwa sehemu ya utatuzi

Hekima na uelewa unahitajika kwa sasa, ni ngumu kupambana na governaing power, ikitumika nguvu yenye mlingano sijui itakuaje!

..we are already late.

..Polisi wetu wamefundishwa kuwachukia na kuwafanyia ukatili viongozi na wafuasi wa chama fulani cha upinzani.

..maelekezo ya kuchukia viongozi na wafuasi wa chama fulani cha upinzani pia yameelekezwa kwa waendesha mashtaka wa serikali, na baadhi ya mahakimu na majaji.

..kama taifa sijui tunakwenda wapi. Haiwezekani baadhi ya Watanzania wachukuliwe kama raia wa daraja la nne katika nchi yake.
 
Kitu kisicho eleweka na kinaweza chukuliwa kawaida kuna traits yaani tabia huzaliwa ama kuanzishwa na kisha kusambazwa kupitia mazingira

Mfano watu walio zaliwa kwenye hali ya vita na maandamano hizo genes huwa zina badilika na kisha kuathiri vizazi vinavyo fuata

Kwa namna hii ukikaa kwa jicho la miaka kumi ijayo mpaka ishirini inawezekana tukawa tuna anzisha ama kutengeneza kizazi chenye kiburi na roho ya kisasi kuliko vyote Afrika

Kwanini tabia ilio kuwa domant kupitia chembe hai tunaiweka juu na ianze tawala fikra na hisia zetu

Ndio maana kuna baadhi ya nchi migomo vita na maandamano haviishi

Hili ni zito sana!!!
 
..we are already late.

..Polisi wetu wamefundishwa kuwachukia na kuwafanyia ukatili viongozi na wafuasi wa chama fulani cha upinzani.

..maelekezo ya kuchukia viongozi na wafuasi wa chama fulani cha upinzani pia yameelekezwa kwa waendesha mashtaka wa serikali, na baadhi ya mahakimu na majaji.

..kama taifa sijui tunakwenda wapi. Haiwezekani baadhi ya Watanzania wachukuliwe kama raia wa daraja la nne katika nchi yake.
May be, but we still have time to solve it brother, chuki na kila kitu ulichogusia inawezekana kuondoka taratibu kikubwa ni namna taarifa na maagizo yanayo tolewa ndio hubadili hali

Hili huenda likawa first call tukizubaa ikaja second hali itakuwa mbaya kwa watu

Kama ni chuki basi pande mbili taru ama nne zikae na kuangalia taratibu za kuweka mambo sawa

Hii itaweza fanya watu wakashindwa hata kusalimu ama kuona viongozi na mambo yakawa magumu zaidi
 
Kabisa mkuu, japo hatujitaji kufika huku wengi wanapo fikiria wanamchi kumiliki hivyo vifaa, swali ni kwamba what next kama kila kitu kitakaa sawa na jamii ina hivyo vifaa?

Ingewekwa elimu ya kwamba ukiachana na maswala ya uchumi na mfumo wa kimaisha basi amani ni kitu kinacho ainisha ama kufanya utambuzi wa jamii ilio endelea na yenye ustaarabu

Na ukija hapo basi utaweza tambua sote tunahitaji kufika katika uelewa mmoja
Unafikiri kwanini nchi kama Marekani wanaipambania sana ile Second ammendment?
 
Kwa upande wao wanaona hilo likipita itasaidia kwenye ulinzi binafsi lakini angalia kariba na tabia, kama likipita hali itakuaje mkuu?, watazikana sana

Kwa sasa wananchi wana jaziba, kinacho hitajika hili jambo litulizwe kwa hekima, au hata hii wengi hawataki mkuu?
 
Hapana kwa sisi tunaoamini kwenye Agano la Kale, imani yetu ni kwamba waliosababisha hayo mauaji nayo yawapasa kuonja utamu wa kuuliwa na wengine. Baada ya wao kuonja joto ndipo mnaweza kukaa vizuri kwa heshima na kuzungumza.
 
Okay hili ni zito, kama namna ndio hii then hekima ndio inayo hitajika kwa sasa mkuu
 
Watawala wa nchi hii hawana hekima, usifanye hilo kosa la kutumia hekima unapo deal na mtu mwenye akili za kinguruwe maana utaishia kuchafuliwa kila sehemu. Kumbuka nguruwe ana uwezo wa kula watoto wake kama ambavyo wanasiasa wa tanzania walivyoua wananchi kuanzia tarehe 30.
 
May be, but we still have time to solve it brother, chuki na kila kitu ulichogusia inawezekana kuondoka taratibu kikubwa ni namna taarifa na maagizo yanayo tolewa ndio hubadili hali

Hili huenda likawa first call tukizubaa ikaja second hali itakuwa mbaya kwa watu

Kama ni chuki basi pande mbili taru ama nne zikae na kuangalia taratibu za kuweka mambo sawa

Hii itaweza fanya watu wakashindwa hata kusalimu ama kuona viongozi na mambo yakawa magumu zaidi

..hili tatizo limekolea huu ni takriban mwaka wa 10. kwa maoni yangu inawezekana tumeshachelewa.

..Na kibaya zaidi hakuna mtu yeyote katika nafasi za kimamlaka anayefikiria kubadili muelekeo.
 
Yanayo andikwa huko mitandaoni, binafsi nabaki katika mawazo kutokana na kuwa muumini wa Tanzania yenye upendo, amani na utulivu, lakini yalio pelekea yote haya kwa vijana ni chuki ilio jengwa kidogo na kisha kukomaa kutokana na vitendo ama matukio yalio kosa majibu, hili la sasa (upandikizaji wa chuki, na umma kulishwa taarifa zisizo thibitishwa hasa kwenda vyombo vya usalama) ni hatari zaidi na linaweza kosa utatuzi wa haraka?

Hili linajengwa kwa kasi sana, lisipo pata hatua za utatuzi wa haraka kuna uwezekano wa vijana kuanzisha vikundi na kisha kuzaa ugaidi, japo sijatambua vitakuwa na mlengo gani?, pili wananchi wanaweza kuchochewa na kisha kuhitaji majeshi ama taasisi za nchi za magharibi kuingilia kati, hii ni hatari na nimeisikia lina zungumzwa

Hili la pili sina nia ya kupinga fikra wala mawazo ya watu nimeona mtandaoni mtu au watu ana shauri kama inawezekana serikali iingie makubaliano na taifa moja la magharibi kutuliza hali, hili ni sawa kweli wakuu? Tukiangalia wananchi waliingia barabarani wakiwa na imani ya kulindwa kwa namna moja walipewa hilo, lakini likaja swala la wao kuuliwa, kisha taarifa tofauti zilisambaa zikihusisha viongozi wa taasisi kutokuwezesha waandamanaji walicho hitaji, sasa imefika hatua taasisi moja inataka ipewe lawama haijafanya kazi kama ilivyo kuwa mategemeo ya watu

Wasiwasi wangu ni baada ya haya yote, namna gani itatumika kutuliza jamii na watu wa kawaida?, hawa vijana wakirudi kuna uwezekano wakafanya mambo nnje ya utaratibu tulio zoea , chuki inayo jengwa kwenda vyombo vya usalama sio ya kupuuzwa, kwa namna fulani watu wana aminishwa taasisi na vyombo vya usalama havipo kwa ajili ya wananchi, wanawaza vijana wapate ama kupatiwa vifaa vya kujilinda ili kukabliana na wanao wazuia hii ni hatari kubwa sana. Upendo urudi sijui ni kwa namna gani ila tuna hitaji utaratibu usio na athari kwa pande zote na ikiwezekana hotuba ya kuliponya Taifa iwepo, sio baada ya miezi huu mbuyu usikomae wakuu, hapo mbele utakuwa mkubwa ila iwepo namna nzuri ya kuliendea jambo

Nimekaa na watu mataifa karibia yote Afrika,naweza thibitisha kwa kusema, hakuna watu hatari na wenye roho ya visasi kama watanzania, hawaoneshi hasira kama mataifa mengine, ila wanaweka vinyongo bila ya kulalamika lakini siku wakitoa ya moyoni huwa wanajenga na chuki ya moja kwa moja ni wagumu kusamehe, ninalo omba hawa vijana kwa wazee wasije chukia hizi taasisi sijui tutakuwa katika hali gani?

Mungu Ibariki Tanzania
Polisi na Rais wao wa kuchaji kwa solar wamesema ni raia wa kigeni, kwa hiyo tulia wacha kimuhemuhe
 
Back
Top Bottom