Tulipofika: mbegu ya chuki inapandwa, umma unachezeshwa, na hatari ina tengenezwa, hatua za haraka zichukuliwe!

Yanayo andikwa huko mitandaoni, binafsi nabaki katika mawazo kutokana na kuwa muumini wa Tanzania yenye upendo, amani na utulivu, lakini yalio pelekea yote haya kwa vijana ni chuki ilio jengwa kidogo na kisha kukomaa kutokana na vitendo ama matukio yalio kosa majibu, hili la sasa (upandikizaji wa chuki, na umma kulishwa taarifa zisizo thibitishwa hasa kwenda vyombo vya usalama) ni hatari zaidi na linaweza kosa utatuzi wa haraka?

Hili linajengwa kwa kasi sana, lisipo pata hatua za utatuzi wa haraka kuna uwezekano wa vijana kuanzisha vikundi na kisha kuzaa ugaidi, japo sijatambua vitakuwa na mlengo gani?, pili wananchi wanaweza kuchochewa na kisha kuhitaji majeshi ama taasisi za nchi za magharibi kuingilia kati, hii ni hatari na nimeisikia lina zungumzwa

Hili la pili sina nia ya kupinga fikra wala mawazo ya watu nimeona mtandaoni mtu au watu ana shauri kama inawezekana serikali iingie makubaliano na taifa moja la magharibi kutuliza hali, hili ni sawa kweli wakuu? Tukiangalia wananchi waliingia barabarani wakiwa na imani ya kulindwa kwa namna moja walipewa hilo, lakini likaja swala la wao kuuliwa, kisha taarifa tofauti zilisambaa zikihusisha viongozi wa taasisi kutokuwezesha waandamanaji walicho hitaji, sasa imefika hatua taasisi moja inataka ipewe lawama haijafanya kazi kama ilivyo kuwa mategemeo ya watu

Wasiwasi wangu ni baada ya haya yote, namna gani itatumika kutuliza jamii na watu wa kawaida?, hawa vijana wakirudi kuna uwezekano wakafanya mambo nnje ya utaratibu tulio zoea , chuki inayo jengwa kwenda vyombo vya usalama sio ya kupuuzwa, kwa namna fulani watu wana aminishwa taasisi na vyombo vya usalama havipo kwa ajili ya wananchi, wanawaza vijana wapate ama kupatiwa vifaa vya kujilinda ili kukabliana na wanao wazuia hii ni hatari kubwa sana. Upendo urudi sijui ni kwa namna gani ila tuna hitaji utaratibu usio na athari kwa pande zote na ikiwezekana hotuba ya kuliponya Taifa iwepo, sio baada ya miezi huu mbuyu usikomae wakuu, hapo mbele utakuwa mkubwa ila iwepo namna nzuri ya kuliendea jambo

Nimekaa na watu mataifa karibia yote Afrika,naweza thibitisha kwa kusema, hakuna watu hatari na wenye roho ya visasi kama watanzania, hawaoneshi hasira kama mataifa mengine, ila wanaweka vinyongo bila ya kulalamika lakini siku wakitoa ya moyoni huwa wanajenga na chuki ya moja kwa moja ni wagumu kusamehe, ninalo omba hawa vijana kwa wazee wasije chukia hizi taasisi sijui tutakuwa katika hali gani?

Mungu Ibariki Tanzania
Kaka yangu ametekwa na hadi leo hajulikani alipo,baba yangu kabomolewa nyumba bila fidia kisa eneo alilojenga kapewa mwekezaji,mdogo wangu kapigwa risasi juzi kapoteza maisha na mwili hadi leo hatujapewa,TRA wamekuja kunikadiria kodi kwenye biashara yangu haiendani na uhalisia wa mtaji wangu.....upendo kwa nchi yangu nitautoa wapi wakati serikali yenyewe hainipendi?

Ni mfano tu lakini.
 
..hili tatizo limekolea huu ni takriban mwaka wa 10. kwa maoni yangu inawezekana tumeshachelewa.

..Na kibaya zaidi hakuna mtu yeyote katika nafasi za kimamlaka anayefikiria kubadili muelekeo.
Then is too dangerous, Tanzania ni nchi ya kimkakati sana, ipo eneo ambalo ni zuri sio kiuchumi tuu hata kiulinzi Tanzania is the gate to south and north of Africa

Mkubwa omba Mungu raia wasipandikizwe chuki na wengine wa karibu
 
Polisi na Rais wao wa kuchaji kwa solar wamesema ni raia wa kigeni, kwa hiyo tulia wacha kimuhemuhe
Okay huu sio ushabiki mkuu, hiki jambo likizidi huu mwaka ni hatari zaidi ya tunavyo ona kwa sasa, amani ni ya muhimu, lakini kabla ya hayo yote toba ifanyike kwanza

Taifa linahitaji uponyaji, ulishawahi sikia mioyo ya watu ni mizito basi ndio sasa, sio kwa upande wa wananchi tuu, hata wenye dhamana nao wanauzito uleule

Omba hekima itawale nchi ipone na kutulia ila ukisema haya sisi tupo mkuu
 
Yanayo andikwa huko mitandaoni, binafsi nabaki katika mawazo kutokana na kuwa muumini wa Tanzania yenye upendo, amani na utulivu, lakini yalio pelekea yote haya kwa vijana ni chuki ilio jengwa kidogo na kisha kukomaa kutokana na vitendo ama matukio yalio kosa majibu, hili la sasa (upandikizaji wa chuki, na umma kulishwa taarifa zisizo thibitishwa hasa kwenda vyombo vya usalama) ni hatari zaidi na linaweza kosa utatuzi wa haraka?

Hili linajengwa kwa kasi sana, lisipo pata hatua za utatuzi wa haraka kuna uwezekano wa vijana kuanzisha vikundi na kisha kuzaa ugaidi, japo sijatambua vitakuwa na mlengo gani?, pili wananchi wanaweza kuchochewa na kisha kuhitaji majeshi ama taasisi za nchi za magharibi kuingilia kati, hii ni hatari na nimeisikia lina zungumzwa

Hili la pili sina nia ya kupinga fikra wala mawazo ya watu nimeona mtandaoni mtu au watu ana shauri kama inawezekana serikali iingie makubaliano na taifa moja la magharibi kutuliza hali, hili ni sawa kweli wakuu? Tukiangalia wananchi waliingia barabarani wakiwa na imani ya kulindwa kwa namna moja walipewa hilo, lakini likaja swala la wao kuuliwa, kisha taarifa tofauti zilisambaa zikihusisha viongozi wa taasisi kutokuwezesha waandamanaji walicho hitaji, sasa imefika hatua taasisi moja inataka ipewe lawama haijafanya kazi kama ilivyo kuwa mategemeo ya watu

Wasiwasi wangu ni baada ya haya yote, namna gani itatumika kutuliza jamii na watu wa kawaida?, hawa vijana wakirudi kuna uwezekano wakafanya mambo nnje ya utaratibu tulio zoea , chuki inayo jengwa kwenda vyombo vya usalama sio ya kupuuzwa, kwa namna fulani watu wana aminishwa taasisi na vyombo vya usalama havipo kwa ajili ya wananchi, wanawaza vijana wapate ama kupatiwa vifaa vya kujilinda ili kukabliana na wanao wazuia hii ni hatari kubwa sana. Upendo urudi sijui ni kwa namna gani ila tuna hitaji utaratibu usio na athari kwa pande zote na ikiwezekana hotuba ya kuliponya Taifa iwepo, sio baada ya miezi huu mbuyu usikomae wakuu, hapo mbele utakuwa mkubwa ila iwepo namna nzuri ya kuliendea jambo

Nimekaa na watu mataifa karibia yote Afrika,naweza thibitisha kwa kusema, hakuna watu hatari na wenye roho ya visasi kama watanzania, hawaoneshi hasira kama mataifa mengine, ila wanaweka vinyongo bila ya kulalamika lakini siku wakitoa ya moyoni huwa wanajenga na chuki ya moja kwa moja ni wagumu kusamehe, ninalo omba hawa vijana kwa wazee wasije chukia hizi taasisi sijui tutakuwa katika hali gani?

Mungu Ibariki Tanzania
Kama ni ushauri tu,kila aina yaushauri umetolewana kufika kwa wanaohusika,,ila kwamazoea yaliyojengeka kwamba Watanzania ni wapole na hawawezi kufanya lolote sijui kama hata huu ushauri wako mzuri utapata nafasi.Kwani wapo watakao sema niushauri tu na sii lazima ufuatwe.Ila kwa manufaa ya nani hilo ni jambolingine.
 
Ni kweli mkuu naimani wenye nafasi za karibu huwa wanasoma, na kupita huku ndani huenda na wao wanafikiria kama tunayo andika, kikubwa tunaomba upendo na amani iwepo mkuu pamoja na mengine
 
Hivyo vinahengwa tena kwa dhati kupitia utashi wa kisiasa,ila shida inakuja pale utashi wakisiasa unapokosekana.
 
Back
Top Bottom