Haujamjibu ipasavyo, na kama scenario yako ya kutoa mayai mawili ingekuwa ndivyo ilivyo basi kungekuw na prevalence kubwa sana ya mapacha (fraternal). Kimsingi yai linatoka moja, na ovaries zinapevusha mayai kwa kubadilishana. Kuna wakati inaweza kutokea kila ovary ikapevusha yai na hapo yanaweza kushuka mawili na uwezekano mkubwa ni kutunga mimba mapacha.
Kwa suala lake, kwanza atueleze, kama baada ya tendo la ndoa mpenzi wake aliingia hedhi tarehe ngapi mwezi huo wa nne na baada ya hapo amemiss periods ngapi? Maana kama ilikuwa April, tunategemea sometime in May arudi hedhi, na June pia arudi hedhi (normally). kwa hiyo kama amemiss hedhi ya June, na ya May alipata, then mimba ilitungwa at least one week baada ya hedhi ya May, so kama hawakukutana May inawezekana mdada alikutana na mtu mwingine. Mbona haya yanaweza kutokea? Kuna rafiki yangu 'aliuziwa' mimba ambaye kwa mahesabu ya lini walikutana mara ya mwisho na mpenzi wake, mtoto alipaswa kuzaliwa njiti wa miezi saba, cha ajabu alizaliwa full term. Jamaa alishashtuka akamwambia ampeleke kwa Baba yake wa kweli.
Ila hapa tuna-speculate tu maana hatujui mambo ambayo walifanya wahusika, labda tupate details zaidi.