Tulitumia zaidi ya Tsh. Bilioni 7 kurekodi Royal Tour, tumeingiza kiasi gani mpaka sasa?

Tulitumia zaidi ya Tsh. Bilioni 7 kurekodi Royal Tour, tumeingiza kiasi gani mpaka sasa?

Black Butterfly

Senior Member
Joined
Aug 31, 2022
Posts
130
Reaction score
368
Ukiangalia gharama kubwa za maisha zinavyozidi kuwatesa wananchi, kila kitu kimepanda bei kuanzia chakula, mafuta, vifaa vya ujenzi ndio kabisaaaa. Kuna wakati najiuliza tulitumia zaidi ya Tsh. Bilioni 7 kwaajili ya kushoot filamu ya Royal Tour ili iweje sasa? zimerudi gharama kiasi gani mpaka sasa?

Kwanza ni Watanzania wangapi mpaka sasa wamefanikiwa kuiona hiyo filamu? nna uhakika hata 1000 hawafiki, sasa hebu fikiria kitu cha kwetu wenyewe hatujakiona mpaka leo. What was the reason ya kushoot? tuna TV zetu hapa Bongo lakini hazina kibali cha kuionesha kwa Watanzania, ukitaka kuiangalia inabidi ulipie sio chini ya Tsh. 30,000.

Mambo ya ajabu sana yaani maudhui yametoka nchini kwetu lakini ili kuyaona inabidi sisi wenye nayo tuyalipie na bado tuliwalipa waliokuja kuyachukua. Wajinga ni sisi.

Haya turudi kwenye fadia zilizopatikana kwenye hiyo ROYO TUA, mpaka sasa zimejenga madara mangapi? au ndio tumefeli tumeamua kuchukua TOZO ndio ziendeshe nchi?

Nina hasira wacha nikanywe maji. SMH
 
Ukiangalia gharama kubwa za maisha zinavyozidi kuwatesa wananchi, kila kitu kimepanda bei kuanzia chakula, mafuta, vifaa vya ujenzi ndio kabisaaaa. Kuna wakati najiuliza tulitumia zaidi ...
Mambo ya ajabu sana yaani maudhui yametoka nchini kwetu lakini ili kuyaona inabidi sisi wenye nayo tuyalipie na bado tuliwalipa waliokuja kuyachukua. Wajinga ni sisi.🥲[emoji57]
 
Hujui royal tour ilikuwa inaficha kitu gani kipite? Kila tukio lazima liwe na lengo mkiwa busy kufatilia huo upuuzi nyuma ya pazia kuna yanayo endelea

Huyu mzee ana dhambi kumfanya bibi wa watu afanye kazi za waziri
 
Dark days
Hujui royal tour ilikuwa inaficha kitu gani kipite? Kila tukio lazima liwe na lengo mkiwa busy kufatilia huo upuuzi nyuma ya pazia kuna yanayo endelea

Huyu mzee ana dhambi kumfanya bibi wa watu afanye kazi za waziri
 
Swali lako halina mantiki kabisa. Aliyekuambia lengo ni kurudisha gharama ndani ya miezi sita ni nani? Hata hivyo, husikii taarifa za kufurika kwa watalii huko kaskazini na Zanzibar?

Je wafanyabiashara katika sekta ya utalii hawafaidiki? Hujaona namna waongoza watalii walivyo busy back to back?

Isitoshe, si watu kama wewe waliokuwa wakilalamika kuwa hatutangazi utalii ipasavyo na badala yake Kenya wanatumia fursa?

Ulitaka kifanyike nini ili uridhike? Binadamu ni kiumbe wa ajabu sana yaani. Hajui alitakalo, kazi kulalama tu.
 
Ccm hakuna jambo walilowahi kulifanya na wakafanikiwa labda uwizi wa kura kipindi cha uchaguzi
 
Ukiangalia gharama kubwa za maisha zinavyozidi kuwatesa wananchi, kila kitu kimepanda bei kuanzia chakula, mafuta, vifaa vya ujenzi ndio kabisaaaa...
Uliishaambiwa hizo pesa hazikuwa za kwetu. Za kwetu ni zile zitakazopatikana kwa watalii wengi kuja Tanzania baada ya kuiona ROHO TUA! Halafu, Watanzania hatuoneshwi kwasababu hatuna tabia ya kutalii! Ahahahahah!!!!!!
 
Tatizo ni sera mbovu za Ujamaa zilizoletwa na Nyerere zinakwamisha uchumi. Hata watalii milioni wakija, hali ya uchumi haitabadilika sana kwa sababu kuna mfumo mbovu.
 
Swali lako halina mantiki kabisa. Aliyekuambia lengo ni kurudisha gharama ndani ya miezi sita ni nani? Hata hivyo, husikii taarifa za kufurika kwa watalii huko kaskazini na Zanzibar...
Husikii tarifa za kufurika watalii?

Ndo nini we kiazi aka mlamba asali?
 
Back
Top Bottom