Swali lako halina mantiki kabisa. Aliyekuambia lengo ni kurudisha gharama ndani ya miezi sita ni nani? Hata hivyo, husikii taarifa za kufurika kwa watalii huko kaskazini na Zanzibar?
Je wafanyabiashara katika sekta ya utalii hawafaidiki? Hujaona namna waongoza watalii walivyo busy back to back?
Isitoshe, si watu kama wewe waliokuwa wakilalamika kuwa hatutangazi utalii ipasavyo na badala yake Kenya wanatumia fursa?
Ulitaka kifanyike nini ili uridhike? Binadamu ni kiumbe wa ajabu sana yaani. Hajui alitakalo, kazi kulalama tu.