Tulivyoachana aliniambia mtoto siyo wa kwangu, ameachwa tena anataka nimrudie

Tulivyoachana aliniambia mtoto siyo wa kwangu, ameachwa tena anataka nimrudie

Akili Unazo!

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2009
Posts
3,930
Reaction score
4,912
TULIVYOACHANA ALINIAMBIA MTOTO SIYO WA KWANGU, AMEACHWA TENA ANATAKA NIMRUDIE.

Dunia hii hawa Wanawake wamekuwa Vichaaa siyo Bure.... kaka nimekwama najitaji ushauli naomba nisaidie.

"Nilikuwa na mpenzi wangu nilikuwa naishi nae ingawa tulikuwa bado hatujaoana ila tulikuwa tunaishi pamoja kama mke na mume na wazazi wake na wa kwangu walilijua hilo..... mahusiano yetu hayakwenda bure tulibahatika kupata mtoto wetu wa kiume.

Kiukweli nilikuwa nampenda sana mpenzi wangu, yani sanaa ingawa yeye alikuwa bado hajawa tayari kuwa mke ndiyo maana alikuwa hataki nimuoe mapema.

Miezi 8 baadae baada ya mtoto kuzaliwa, nilimfumania na mwanaume mwingine wakiwa faragha, badala aniombe msamaha alinitukana sana mbele ya umati wa watu na kusema hata mtoto siyo wa kwangu, ni kihelehele changu tu cha kuhudumia....

Niliumia sana yani ile kauli inaniuma mpaka leo ukizingatia nimelea tangu wiki ya kwanza hadi kujifungua, mtoto hakufanana na mimi ila sikujali maana mtoto anaweza kufanana na mama yake tu kwahiyo sikuwaza sana, kutokana na kauli zile niliumia sana nikaja kumuacha.

Sasa siku za hivi karibuni ananisumbua eti nisamehe ni shetani alimuingia, mara ulikuwa ni utoto mtoto ni wangu, na ameniambia kule pia kaachika, nifanyaje kaka?
 
NIPO KWENYE MAHUSIANO NA MWANAMKE ALIYENIZIDI UMRI,NAMPENDA LAKINI ANAYONIFANYIA NIMECHOKA.

Dunia haina Jambo Jema hata kama litokeeje- Oneni haya maswahibu , mimi nipo kwenye mahusiano ya kimapenzi na mwanamke aliyenizidi umri, amenizidi miaka 25 ni mama mtu mzima haswa lakini kwakuwa tunapendana na ana pesa ya kutosha niliona bora nitulie nae maana mabinti wa siku hizi ni stress tupu.

Nampenda sana huyu mwanamke, namfulia nguo mpaka za ndani, nimekuwa zaidi ya mpenzi, yeye hunipa pesa za kutosha yani milioni mbili milioni tatu siyo shida zake....shida ni kwamba ana wivu sana, yani hataki nitoke peke yangu, ananifungia ndani sana
😭
😭
mwanzoni nilivumilia lakini sasa nimechoka siwezi tena kama ni pesa bora ziwe, lakini sasa naogopa nitatokaje?

Maana hajanikosea na hii kunifungia ndani yeye anaona kawaida, anasem ananitunza.

Mbona heka heka Acha tu tuendelee kusubiria Makarani
 
MUME WANGU ANANIZALISHA MFULULIZO KILA MWAKA, NIMECHOKAAA
Duniani Vioja haviishi sasa hata hili kweli , jamani naomba ushauli nifanyaje maana nashindwa kuamua chochote
😭
😭
kaka mwaka 2006 niliolewa na msomali mmoja hivi hapa Mombasa Kenya.... yuko na pesa za kutosha hatuna shida sawa lakini tangu anioe amekuwa ni mtu wa kunizalisha kila mwaka, niliolewa 2006 lakini mpaka sasa nina watoto 8, na nina miaka 38.

Imefika wakati watoto hata hawajulikani yupi mkubwa yupi mdogo
😭
😭
sasa hivi nimemkimbia nalala kwenye chumba cha watoto, alivyoona hivyo ameacha kulala nyumbani, mala anachelewa kurudi...

Mimi nimeshachoka jamani imefika mda sina nguvu kutokana na kuzaa mfululizo, eti jamani nifanyaje? Nakosa uamuzi maana nikienda kulala chumbani hataki tutumie kinga, matokeo yake mtoto hata hajakuwa vizuri mimba nyingine inaingia, nawapenda watoto ila hii imekuwa too much naomba unisaidie nifanyaje

Wanawake wanataka nini Jamani wazae shida wasizalishwe shida ..............

CHAI
 
NIMERUDI KUTAFUTA MAISHA NIMEKUTA MKE WANGU WA NDOA ANA UJAUZITO WA MWANAUME MWINGINE.
" Mwaka jana mwezi wa tano nilipata dharula ya kazi nje ya nchi, nilienda Dubai kwa kazi ya mkataba wa mwaka mmoja, kwakua ulikuwa mkataba wa pesa nyingi niliamua kwenda kufanya kazi hiyo ili nikirudi pesa zinisaidie kumalizia nyumba yangu....... nikamuaga mke wangu na watoto wangu wawili, kwa amani kabisa tukawa tunawasiliana hata nilipokuwa kule Dubai simu zilikuwa hazikati.
Nilikuwa natuma pesa kila wiki laki moja na wakati mwingine natuma zaidi ili mke wangu asiwe na tamaa ya pesa akakwapuliwa na njemba za mjini....lakini pamoja na kujitahidi matokeo yake nimeambulia aibu.
Mwezi wa pili aliacha kunipigia simu kabisa, hata nikimtafuta alikuwa hapatikani, nikamtafuta rafiki yangu aangalie familia kama wako salama, rafiki yangu akaniambia mke wako ni mjamzito na ana mtu wanaishi pamoja nyumbani kwako
Niliumia sana, mwezi wa sita nilipomaliza mkataba wangu nikarudi nyumbani Tanzania na nilichokikuta ni aibuu!! nimedhalilika jamani sijui ntawaeleza nini watoto wangu,
Sijui nichukue maamuzi gani kwa huyu mwanamke, amekimbilia kwa dada,yake lakini nina hasira naye hakuna mfano
 
Pole sana maana hapo Bado kubeba mimba tu ila stage zote za mke bora umezipitia.
 
MUME WANGU ANANIZALISHA MFULULIZO KILA MWAKA, NIMECHOKAAA
Duniani Vioja haviishi sasa hata hili kweli , jamani naomba ushauli nifanyaje maana nashindwa kuamua chochote
[emoji24]
[emoji24]
kaka mwaka 2006 niliolewa na msomali mmoja hivi hapa Mombasa Kenya.... yuko na pesa za kutosha hatuna shida sawa lakini tangu anioe amekuwa ni mtu wa kunizalisha kila mwaka, niliolewa 2006 lakini mpaka sasa nina watoto 8, na nina miaka 38.

Imefika wakati watoto hata hawajulikani yupi mkubwa yupi mdogo
[emoji24]
[emoji24]
sasa hivi nimemkimbia nalala kwenye chumba cha watoto, alivyoona hivyo ameacha kulala nyumbani, mala anachelewa kurudi...

Mimi nimeshachoka jamani imefika mda sina nguvu kutokana na kuzaa mfululizo, eti jamani nifanyaje? Nakosa uamuzi maana nikienda kulala chumbani hataki tutumie kinga, matokeo yake mtoto hata hajakuwa vizuri mimba nyingine inaingia, nawapenda watoto ila hii imekuwa too much naomba unisaidie nifanyaje

Wanawake wanataka nini Jamani wazae shida wasizalishwe shida ..............
[emoji24]
[emoji24]

Tukiachana na kukuzalisha vipi wewe unaweza kutoa mchango gani wa kiuchumi kwenye familia?
Au unaweza kuchangia nini kwenye uendeshaji wa familia na maendeleo yake kiujumla?
 
Back
Top Bottom