Tulivyowaza tukiwa watoto

Tulivyowaza tukiwa watoto

Faru dume

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2012
Posts
471
Reaction score
116
Poleni wananzengo,

Si vibaya kukumbuka nyakati zilizopita pindi tukiwa watoto wadogo ukiachana na maswali ya kidadisi kama vile "Eti mama mimi nimetoka wapi?"

Je ulishawahi kuwaza nini kipindi cha utoto wako ukaja gundua sio kweli ulivyokuwa ukihisi?

Mfano mimi nilijua watu wazima hawaendi haja kubwa (chooni).

Je, wewe?

Karibuni.
 
1~ Mi nilijua eti dereva anayeendesha gari kubwa hawezi kupigwa na dereva anayeendesha gari ndogo ikitokea wamepigana.

2~ Nilijua eti unaposikiliza redio basi unaweza kumsemesha mtangazaji na akakusikia.

3~ Nilijua eti zile ngurumo za radi wakati mvua inanyesha au kabla ya mvua kunyesha basi Mungu anahesabu mapipa ya maji.

4~ Nilijua eti ukiweka sindano-rungu kwenye reli basi treni ikipita inaanguka.

5~ Nilikuwaga nadhani eti kama kwa mfano nchi na nchi zimeangukia kwenye machafuko yanayopelekea vita basi ilikuwa unachorwa mstari katikati, upande huu wanasema wanajeshi wa nchi A na upande wa pili wanajeshi wa nchi B, halafu inapigwa filimbi risasi zinaanza kuunguruma [emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi nilijua umeme ukikatika na gari hazimbei
 
1.Nakumbuka baada ya kusikia ile ngoma ya jdee MAWAZO kuna mstari ansema"mawazo kila mtu ana mawazo akulala ukiamka unawaza..."

Sasa nikawa nawaza haya mawazo ni nini hiki kitu

2.sikutaka dada yangu aolewe na mkulima,ila leo mimi ni mkulima nataka dada zenu wanikubalie.

3.Nikifika miaka 18 nitakuwa mtu tofauti sana.
 
Acha channel E, manayoangalizia miziki siku hizi.

Channel ambayo zamani pekee ndio ilikua inaonyesha mieleka, channel tulio wajulia kina John cena
Dah ukiniambia etv ya south unanikumbusha decoder ya strong ilikuwa kama inazingua kuonesha kwako kuna namba fulani unaingiza basi etv inaanza kuonesha
images (21).jpeg
 
1~ Mi nilijua eti dereva anayeendesha gari kubwa hawezi kupigwa na dereva anayeendesha gari ndogo ikitokea wamepigana.

2~ Nilijua eti unaposikiliza redio basi unaweza kumsemesha mtangazaji na akakusikia.

3~ Nilijua eti zile ngurumo za radi wakati mvua inanyesha au kabla ya mvua kunyesha basi Mungu anahesabu mapipa ya maji.

4~ Nilijua eti ukiweka sindano-rungu kwenye reli basi treni ikipita inaanguka.

5~ Nilikuwaga nadhani eti kama kwa mfano nchi na nchi zimeangukia kwenye machafuko yanayopelekea vita basi ilikuwa unachorwa mstari katikati, upande huu wanasema wanajeshi wa nchi A na upande wa pili wanajeshi wa nchi B, halafu inapigwa filimbi risasi zinaanza kuunguruma [emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
Dah hii namba 5 imenichekesha sana
 
Nimecheka sana aisee.

1. Nilijua gari zina jinsia. Yaani nikiona FIAT nilikuwa naona ni Dume na nikiona Bus aina ya Leyland najua ni jike [emoji3][emoji3][emoji3]

2. Nilijua pipi zinapandwa na kuota. Nimewahi kupanda pipi aka peremende na kumwagilia maji. Baada ya siku kama 5 hivi nikaona haioti ikabidi nifukue pale nikakuta kitu kilisha yeyuka [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
3. Nilijua kila chombo unaweza kupikia. Kuna siku niliweka maharage ya kupasha asubuhi kwenye kikombe cha plastic matokeo kiliyeyuka na maharage yote [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Kuna mengi sana.
Huu uzi ni mzuri sana kwa kuondoa stress
 
Kama kuna kitu kimewahinisumbua utotoni basi ni kifo cha baba wa taifa (Nyerere). Maana ilikuwa kila mtu namuuliza ni nani huyo mpk watu wanalia na kila mtu anaenda uwanja wa taifa, ilinichukuwa muda sana kuelewa kuhusu nyerere kwa kweli
 
Kwavile madereva pikipiki huvaa sweta/jaket kubwa nkajua basi ndo mabosi kuliko wa gari walivyo hivyo lazima uwe na boda ili uwe na hela nyingi
Nilijua gari ndogo kama teksi haiwezi kuanguka
Nilikuwa nikinyatia chakula na kuingiza mkono kwenye chungu huku nikijua sionekani wala hakuna atakayejua wakt wa asbhi wakati nawahi shule kumbe nimeshaacha alama
 
Back
Top Bottom