Hatuwezi kuijenga nchi hii ikafanikiwa na aina ya wana siasa hawa tulionao. Kamwe hatutaweza! Wamezidi kutuongopea.Wadanganyika munatakiwa kuunda jumuiya za kutetea jamii, na kushughulikia maslahi ya jamii.Kama kungelikuwa na jumuiya za namna hii, ni rahisi kuandaa maandamano kupinga maamuzi kama haya bungeni.
Aidha kwa wanasiasa kwangu mimi nawaona kama ni too theoretical na waongo mara nyingi.Pengine hii inakuja na kuwa mimi ni science boy, hivyo kila kitu nataka practical approaches...and not bla bla bla...
Kama wadanganyika mnasubiri bunge lifanye kitu, naona kama hatufiki....itisheni maandamano!!
Wale "wapiganaji" wako wapi? Mbona wamekuwa kimya?
msiumie sana jamani.. katika siasa.. you win some, you lose some.. and some hurt more too!! But as long as you have another day to fight.. pick yourself up, jipanguse vumbi na machozi, futa makamasi.. inua kichwa na mabega yako.. angalia mbele.. move!!!
sasa najua kwanini Watanzania tunaburuzwa; hatujui kupigana migogoro ya kisiasa. Tunachanga watu wanazoungumza kwa uchungu na hasira na mapambano ya kuangusha watu kisiasa. Sasa watu wasipozungumza tunavyotarajia tunaamini hawapigani tena.
hahaha unatishika na nini tena
in one week.. karibu thread tatu za mwanakijiji.. mnaanza kunitisha.. MODs please..
....Si wote wasemao bwana bwana..........!!
ni sawa kabisa....makala nzuri sana...tatizo haya yoote yatawezekana humu mijini tu...wananchi ambao ndio wapiga kura walio wengi wapo vijijini.....hawajui chochote kinachoendelea kuhusu mageuzi ya kifikra yanayoongelewa humu....nakwambia ni ngumu sana.....kwa mfano ,mimi shughuli zangu huwa zinahusiana na kuzunguka ma wilayani na vijijini...we acha kabisa....BADO NI NDOTO KUWABADILI WATU KIFIKRA NA KIMTAZAMO....yaani kwa jinsi ilivyo hao wanaoitwa mafisadi karibu wooote wanakubalika huko majimboni mwao.,tena hata kwenye nyumba za ibada.....naona iko kazi...nahisi kwa mwaka huu stori ni ile ile....kama kuna kaugumu basi kwa vyovyote vile ,kanuni a na b zitatumika kama kawaida...
Nakubaliana nawe kabisa!wengi humu wanafikiri mabadiliko yataletwa na kuandika makala kwenye magazeti na kwenye mitandao!Kwa watanzania bado sana!mie pia nazunguka vijijini kwenye wapiga kura wengi hakuna umeme wala Tv ,magazeti yanaishi mijini tu!njia ya kuwafikia hao ni mikutano ya hadhara tuuu!
Wengi wana radio lakini zinatumia battery na anapata TBC tu au radio za mikoani nyingi ni mziki tu!