Tulizeni presha Simba SC na Yanga SC hawajaanza kukutana leo

Tulizeni presha Simba SC na Yanga SC hawajaanza kukutana leo

sisi tunazungumzia viwango vya wachezaji,wenzetu wanaangalia historia na mazali
 
Yanga anakufa hii mechi.
Mechi za dabi hazitabiriki lakini kwa hii mechi Yanga atafungwa.

1)Simba wanapata apdates zote za ndani(nyeti) za Yanga kuelekea hii mechi.
2)Mpaka sasa Yanga sio wamoja kuanzia viongozi,wachezaji mpaka mashabiki.kuna viongozi upande wa gsm na wa Msolwa,kuna wachezaji wazawa wanaowatuhumu wachezaji wageni kupendelewa.
3)Simba hii mpaka sasa imeshacheza mechi za CAF zilizokua na presha kubwa na wakawa watulivu na wakafanya vizuri.
4) Kwa mchezaji mmoja mmoja Simba wapo vizuri kuliko wapinzani wao.

Mwisho mpira ni dakika 90,kuna matokeo matatu,kushinda kufungwa na kudraw.
Rage akiwaambia nyie ni mbumbumbu huwa mnabisha, unasema simba inawachezaji bora zaidi, kwa nini mechi mbili za mwisho mlipata draw moja, tena kwa shida na kupoteza game moja? au ni kiliwasibu? Kuanzia game hizo mshasajili mchezaji mpya??

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
... unasema simba inawachezaji bora zaidi, kwa nini mechi mbili za mwisho mlipata draw moja, tena kwa shida na kupoteza game moja?
Hii nayo ni hoja? Kwamba timu bora inapimwa kwa kushinda mechi zote, au inapimwa kwa timu moja? Kwa nini uchague mechi mbili za mwisho, kwa nini usiseme mechi tano za mwisho? Timu bora inapimwa kwa kupata matokeo yenye wastani mzuri kutoka katika vilabu bora. Katika ligi ya bara, kwa sasa Simba ni timu bora kwa kuwa ina wastani mzuri wa matokeo katika mechi ilizocheza. Katika Ligi ya Mabingwa wa Afrika, Simba pia ni timu bora katika msimu huu kwa kuwa ina wastani mzuri wa matokeo katika mechi ilizocheza. Sasa sijajua wewe unaipima timu kwa kutumia vigezo vipi, eti kutoa sare mbili za mwisho na Yanga! Kwani Simba ikitoa sare na Yanga, si maana yake pia Yanga imetoa sare na Simba? Au unamaanisha Simba ilistahili kuwa inashinda!?
 
Baada ya mechi jutiandae taarifa za misiba. Kuna watu lazima watakufa kwa presha,hizi timu buana!
 
Game yangu kubwa leo Barcelona vs Atletico Madrid, hao uto hawanisumbui akili kabisa.
 
Back
Top Bottom