spm96
New Member
- Jun 14, 2023
- 1
- 2
Mabadiliko na mageuzi ya kiutendaji yanayowekwa na kusimamia utawala bora katika kutoa huduma sehemu mbalimbali ni wazi zinaboresha uwezo na ufanisi wa utelekezaji mzuri katika kutoa huduma husika katika ngazi tofauti kwa namna bora na kiyapekee.
Miongoni mwa huduma muhimu zenye uhitaji mkubwa ni huduma za afya kwasababu inatazamwa kama makusudio ya msingi katika maisha ya mwanadamu yanayohitaji uangalizi wa hali zote hivyo inachukuliwa kuwa huduma yenye madhumuni ya kufikia malengo yanayotarajiwa.
Kwa hakika afya ni tunu ya thamani na ghali kwa mwanadamu,kutengemaa kwake kunamuwezesha kuyatekeleza vyema majukumu yake na kukengeuka kwake hudhoofisha harakati zake za kila siku.Mafungamano na matokeo chanya au hasi ya hali ya mwanadamu yanamchango mkubwa wa utambuzi binafsi,mazingira yanayomzunguka na wataalamu wa afya katika kutekeleza wajibu wao wa kitaalamu na kitaalama.
Ukweli usiofichika sekta ya afya inauhitaji wa mabadiliko ya kiutendaji yatayoleta tija na ufanisi mkubwa wa utekelezaji katika utoaji huduma kuanzia ngazi za chini mpaka juu,bila kubeza maendeleo na juhudi zilizopo na zilizofanyika katika sekta hii kwa nyakati tofauti.
Mabadiliko haya yanaumuhimu wa kuzingatia pande kuu tatu kwa kuanza na wasimamizi wakuu ikijumuisha viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia kwa ujumla sekta hii nyeti nchini,wakifuatiwa na watoa huduma katika kada tofauti pamoja na wahudumiwaji. Dhana ya mabadiliko yenye kuleta ufanisi mzuri kiutendaji yatabaki kwa pande zote kuwa tayari katika kuyakubali na kuyakabili mabadiliko na kwa maana hio hiki ni kigezo tosha cha kiutendaji wenye tija.
Miongoni mwa hatua za mwanzoni kuelekea katika mabadiliko haya ni kuuchambua na kuurekebisha mfumo mzima wa afya. Haina maana ya kuchambua na kurekebisha upya kila kitu,bali kutazama mambo ya msingi yenye tija yanayolenga maslahi ya wanufaika wa huduma za afya.
Jukumu la wasimamizi wakuu linalowakilishwa na serikali kwa ujumla wake kupitia Wizara ya Afya ni kupitia muundo na mpangilio wa mfumo wa afya kwa kuziangalia upya sera na kanuni zetu zinazotupa mwanga katika kusimamia huduma za afya nchini. Kufanikisha hili kwa weledi na ufanisi mzuri kwa kushirikiana na wadau pamoja na mashirika tofauti yanayohusika katika masuala ya afya kuangalia na kujiridhisha sera na kanuni hizi kuwa rafiki na zenye maslahi mapana kwa wote na sehemu zote.
Hivyohivyo zijumuishe mlolongo mzima katika mfumo wa afya kwa kuanza na watunga sera,wasimamizi,watoa huduma na wapokea huduma ili kila mmoja katika nafasi yake ajue lipi jukumu lake na analotakiwa kufanya bila kusahau ziweze kumhukumu kila mmoja bila upendeleo pindi wanapokwenda kinyume.
Kimsingi sera na kanuni ni zenye kutungwa kila siku lakini uhitaji wa watu makini,wazalendo waliyotayari kwenda na mabadiliko na kubadilika katika kuzisimamia,kufuatilia na kuzitekeleza kwa uaminifu mkubwa ni jambo linalohitaji kuzingatiwa.
Ni muhimu kuzingatia namna gani huduma za afya zinavyopangwa kwa kuwafikia walengwa kila sehemu kwa kuzingatia na kuboresha ufikiaji rahisi na wa haraka,sambamba na hilo kuweka vipaumbele kwa huduma za dharura zinazohitajika kuwa karibu. Hivyohivyo kuangaliwe huduma zinazopaswa kutolewa bila malipo katika hatua za awali kama vile huduma za mama na mtoto,chanjo,elimu ya afya,afya ya mazingira na mengineyo.
Kadhalika mahitajio ya kimapinduzi ya kiteknologia za afya,nguvu kazi kwa kuchagua waliokuwa na sifa katika kutelekeza majukumu yao,vifaa tiba,madawa pamoja na rasilimali zingine za afya ni jambo la msingi na la kuzingatiwa katika kuchochea mabadiliko ya huduma bora.Ni muhimu kuboresha mifumo mizuri na miundombinu rafiki ya rufaa katika vituo vya karibu na tegemezi kwa watumiaji.
Pamoja na hayo ni muhimu sana kuzingatia majukumu ya utafiti na mafunzo yaliyofanywa,yanayoendelea kufanywa na watafiti wetu na mashirika mengine ya afya kwa kutazama mustakabli wa mfumo wa afya katika nchi yetu.
Kuwa tayari kuboresha maslahi ya wahudumu wetu pamoja na kuwapa motisha na moyo katika kuendelea kuihudumia jamii kwa ustadi na weledi. Si hivyo tu pia kuwa tayari kupokea maoni,ushauri na changamoto zinazojotokeza katika sekta hii kwa lengo la kujifunza,kutekeleza na kuboresha zaidi palipokuwa na shida.
Watoa huduma ni watu muhimu katika kulisongesha gurudumu hili kwa mchango wao mkubwa wa kuyatekeleza majukumu yao kila siku.Pamoja na juhudi hizo kubwa wanazozifanya,miongoni mwa mambo makuu yanayowasukuma watu kujadili sekta ya afya na kuhitaji mabadiliko ya kiutendaji ni kutokana na uzembe na huduma duni.Malalamiko haya yanatokea sehemu zote katika hospitali za umma na binafsi na sababu kuu ni usimamizi mbovu usiozingatia na kuangalia utendaji wa watoa huduma jambo linalopelekea huduma mbovu na uzembe wa marakwamara.
Daima ubobezi mzuri na huduma bora zenye kuzingatia miiko na maadaili ya kazi katika utoaji wa huduma za afya pamoja na usimamizi mzuri wa kiutendaji ni jambo la msingi lenye kuchochea uaminifu na kumiminika wa wahudumiwaji sehemu fulani. Usimamizi madhubuti,uwepo na upatikanaji wa vifaa vya kisasa,wahudumu wa kutosha ni jambo lenye kuchochea mabadiliko ya kiutendaji na kihuduma, ukosefu wa hivyo huepelekea huduma duni na utendaji mbovu.
Wahudumiwaji na wapokezi wa huduma za afya ndio wahusika wakuu na ni kipimo kizuri cha kupima namna gani huduma zinatolewa na kufikishwa kwao. Matarajio ya kundi hili wakiwa kama watumiaji wa huduma za afya wanapenda huduma bora zinazokidhi mahitaji ya watu kwa nyakati na muda tofauti,kuwa na vituo vya afya karibu kwa huduma za dharura,kuwa na mfumo rafiki wa udhamini wa mambo ya afya au kuwa na gharama zinazo vumilika katika kupata huduma za afya. Maboresho ya sehemu hizi yatapunguza kwa kiasi kikubwa malalamiko yanayojitokeza kila siku.
Hivyohivyo yapasa wapewa huduma kuwa wasikivu,wavumilivu wenye kufata ushauri na maelekezo mbalimbali yanayotolewa na wataalamu wa afya kulingana na afya zao katika kuziboresha na wawe wenye afya njema.
Matumaini yetu ni kuzijali afya zetu kwa kuzingatia yale yanayotugusa katika huduma mbalimbali za afya, hivyo ni muhimu sana mabadiliko haya yazingatie pande tatu ili kuleta taswira nzuri ya mabadiliko katika utendaji,bila kusahau usimamizi na uongozi madhubuti hasa kwa wasimamizi wakuu na wahudumu wa afya.

Upvote
2