Little Angel
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 1,212
- 373
Mie tumbo langu naona limeshindikana
Asbh nafanya mazoezi kwa muda wa robo saa, naruka kamba na jogging, kabla sijatoka nakunywa maji ya moto yaliyochanganywa na asali. Nakunywa chai kama kawaida, mchana sili chakula ila nakunywa maji glass 6 hadi 8. Jioni nikirudi nakunywa tena maji ya moto yaliyochanganywa na asali. Uck nakula potion ndogo sana ya chakula na matunda kwa wingi lakini ndo naona tumbo linazidi. silipendi sijui hata nifanye, mazoezi ya situps yalinishinda
Kila ukiamka alfajiri kabla ya kufanya kitu tumia glass 1 ya maji moto ukiwa umekamulia Limao 1 na asali kijiko 1. Ukiweza unaweza kuweka pilipili manga kidogo.
Kinachotokea ni kuwa mchanganyiko huo unaongeza body metabolism kwa kiasi kikubwa sana japo utakuwa hujui na as a result process hiyo ina burn fat nyingi sana. Unaweza fanya hivyo na usiku kabla ya kulala na hata mchana.
Tumia sana salads za rangi na hasa matango na parachichi nk. Hivi tunaita high thermic foood. Ni vyakula ambavyo vikiingia tumboni digestive process inachukua calories za ziada na hivyo ku-burn fats.
Mafanikio Na Afya Njema itakupa details zaidi
For how long ymefanya hivyo?
kuna wakati nilifanya a month mfululizo nikaona halipungui nikaacha, ila nimeanza tena nina three wks tangu nimeanza tena
mie nilikua flat tumboni mpaka nilikua naulizwa kama hua nakula..saiv..aarrgghhh..hata sare za utawani hazikai poa yani
Kwa sasa inaonekana hauko commited...mazoezi yanahitaji commitment na displine ya kufa mtu. Mm nachofanya naamka saa 11 kamili naingia gym saa 12 kasoro robo napiga aerobics au cardio classes mpaka saa moja kamili then naoga naingia ofisini saa 2 kasoro robo. Kwa nn nafanya mazoezi asubuhi ukifanya mazoezi asubuhi you burn storage.... ukifanya jioni una burn ulichokula asubuhi na mchana then unakula tena unalala. So asubuhi ni safi sana hasa kwa anayetaka kupungua sio kuweka misuli/body builder. Jumamosi na jumapili naamka saa 12 kamili nakimbia km 7. Na kunywa maji lita 3 kila siku.
Duuh,mi nazuia kitambi kisije,nifanye nini.maana kama kutembea kwa miguu na tembea sana,maji nakunywa sana,pombe sinywi.mchana siliii kabisa,nakunywa maji tu,ila usiku nakula
Nile vyakula gani ili tumbo langu lipungue yaani lirudie hali ya u flat kama zamani
mazoezi huwa najaribu lakini nashindwa kuendelea nayo kiukweli
msaada juu ya hili maana linanikera sana wakati mwingine
Endelea tu maana sio process ya muda mfupi... give it a minimum of three months..
Usipate shida kulipunguza mkuu maana kama una smart phone kazi yake ni kufutia simu baada ya kuzungumza kwa muda.
Nitajitahidi mamii, manake ni balaa, nguo zingine hazikai kabisa
Na maswali sasa, vipi tayari? mara hongera tunasubiri kulea, ni nini naudhika basi tu
ulaji nahisi
Bila ya mazoezi especially ya kukimbia then, hakuna njia nyingine. Na usije ukajaribu kujinyima kula. Hilo ni kosa ambalo watu wengi wamekuwa wakulifanya na kuishia kudhoofika na matokeo yake unakaribisha magonjwa
Hahahaaa.. kazana ma'am.. kikubwa ni kujitahidi kukikataa then kila kitu kitakua rahisi kuliko unavyodhani..
Mi siku hizi nimezoea.. asubuhi lazima nifanye mazoezi..then Maji ya uvuguvugu yenye asali.Limao na mdalasini.. wanga na mafuta nimeshapumzika muda wa mwezi sasa...
Kitambi byebyee... no supplement wala nini...
Am really happy now..ukiniangalia utapenda.
okeyulaji nahisi