Tumbo kubwa..nilipunguze vipi? kwa njia ya vyakula lakini

Tumbo kubwa..nilipunguze vipi? kwa njia ya vyakula lakini

Mie tumbo langu naona limeshindikana
Asbh nafanya mazoezi kwa muda wa robo saa, naruka kamba na jogging, kabla sijatoka nakunywa maji ya moto yaliyochanganywa na asali. Nakunywa chai kama kawaida, mchana sili chakula ila nakunywa maji glass 6 hadi 8. Jioni nikirudi nakunywa tena maji ya moto yaliyochanganywa na asali. Uck nakula potion ndogo sana ya chakula na matunda kwa wingi lakini ndo naona tumbo linazidi. silipendi sijui hata nifanye, mazoezi ya situps yalinishinda

For how long ymefanya hivyo?
 
Kila ukiamka alfajiri kabla ya kufanya kitu tumia glass 1 ya maji moto ukiwa umekamulia Limao 1 na asali kijiko 1. Ukiweza unaweza kuweka pilipili manga kidogo.

Kinachotokea ni kuwa mchanganyiko huo unaongeza body metabolism kwa kiasi kikubwa sana japo utakuwa hujui na as a result process hiyo ina burn fat nyingi sana. Unaweza fanya hivyo na usiku kabla ya kulala na hata mchana.

Tumia sana salads za rangi na hasa matango na parachichi nk. Hivi tunaita high thermic foood. Ni vyakula ambavyo vikiingia tumboni digestive process inachukua calories za ziada na hivyo ku-burn fats.

Mafanikio Na Afya Njema itakupa details zaidi

You are right mkuu.

There is no shortcuts guys...
Total lifestyle changes is all that you need..

Use calories count kama waweza it helps..

Calories intake < Calories outtake..

Kwa njia hii ukiweka na zoezi kidogo utajipenda...kikubwa ni kuapply hivi vitu...
1.Commitment
2. Consistent
3. Patience.
 
kuna wakati nilifanya a month mfululizo nikaona halipungui nikaacha, ila nimeanza tena nina three wks tangu nimeanza tena

Endelea tu maana sio process ya muda mfupi... give it a minimum of three months..
 
Kwa sasa inaonekana hauko commited...mazoezi yanahitaji commitment na displine ya kufa mtu. Mm nachofanya naamka saa 11 kamili naingia gym saa 12 kasoro robo napiga aerobics au cardio classes mpaka saa moja kamili then naoga naingia ofisini saa 2 kasoro robo. Kwa nn nafanya mazoezi asubuhi ukifanya mazoezi asubuhi you burn storage.... ukifanya jioni una burn ulichokula asubuhi na mchana then unakula tena unalala. So asubuhi ni safi sana hasa kwa anayetaka kupungua sio kuweka misuli/body builder. Jumamosi na jumapili naamka saa 12 kamili nakimbia km 7. Na kunywa maji lita 3 kila siku.

safi sanaaa...
huyo aliye katika avatar ni wewe ee! tehe
 
Duuh,mi nazuia kitambi kisije,nifanye nini.maana kama kutembea kwa miguu na tembea sana,maji nakunywa sana,pombe sinywi.mchana siliii kabisa,nakunywa maji tu,ila usiku nakula

wewe mwenzangu lolz
inashauriwa kula mchana kwa kuwa chakula kitaweza kusagika kwa urahisi, usiku kimeo..
nimeuliza wadau hapa mchana wanategemea hivyo vyakula vya kitaa sijapata jibu, to me kutokula mchana sioni tabu kabisa.. as usiku najua naweza kuchagua hata nile nini coz niko nyumbani. Bado natafakari..
 
Nile vyakula gani ili tumbo langu lipungue yaani lirudie hali ya u flat kama zamani

mazoezi huwa najaribu lakini nashindwa kuendelea nayo kiukweli

msaada juu ya hili maana linanikera sana wakati mwingine

Usipate shida kulipunguza mkuu maana kama una smart phone kazi yake ni kufutia simu baada ya kuzungumza kwa muda.
 
Nitajitahidi mamii, manake ni balaa, nguo zingine hazikai kabisa
Na maswali sasa, vipi tayari? mara hongera tunasubiri kulea, ni nini naudhika basi tu

Endelea tu maana sio process ya muda mfupi... give it a minimum of three months..
 
kwa wewe usiopata muda wa mazoezi waweza kujikita zaidi na diet.Kuna usemi wa kidactari unasema.EATING IS VITAL,EXERCISE IS IMPORTANT.
 
hayo maswali yanaushi..basi tu
Nitajitahidi mamii, manake ni balaa, nguo zingine hazikai kabisa
Na maswali sasa, vipi tayari? mara hongera tunasubiri kulea, ni nini naudhika basi tu
 
  • Thanks
Reactions: ram
Bila ya mazoezi especially ya kukimbia then, hakuna njia nyingine. Na usije ukajaribu kujinyima kula. Hilo ni kosa ambalo watu wengi wamekuwa wakulifanya na kuishia kudhoofika na matokeo yake unakaribisha magonjwa
 
Nitajitahidi mamii, manake ni balaa, nguo zingine hazikai kabisa
Na maswali sasa, vipi tayari? mara hongera tunasubiri kulea, ni nini naudhika basi tu

Hahahaaa.. kazana ma'am.. kikubwa ni kujitahidi kukikataa then kila kitu kitakua rahisi kuliko unavyodhani..
Mi siku hizi nimezoea.. asubuhi lazima nifanye mazoezi..then Maji ya uvuguvugu yenye asali.Limao na mdalasini.. wanga na mafuta nimeshapumzika muda wa mwezi sasa...
Kitambi byebyee... no supplement wala nini...
Am really happy now..ukiniangalia utapenda.
 
  • Thanks
Reactions: ram
Bila ya mazoezi especially ya kukimbia then, hakuna njia nyingine. Na usije ukajaribu kujinyima kula. Hilo ni kosa ambalo watu wengi wamekuwa wakulifanya na kuishia kudhoofika na matokeo yake unakaribisha magonjwa

Kwenye diet hutakiwi uskip any meal.. unatakiwa ule at least milo minne kwa siku but in small portion.. portion kubwa iwe ni fruits and veggies..

Pia drink water at least 8glasses per day.
 
Dah, hongera sana, nakutamanije, ngoja nijitahidi, mie nakunywa maji ya moto na asali tu so niongeze na limao?
Dozi ya mdalasini na limao niliifanya sana but haikusaidia kitu nikaachana nayo

Hahahaaa.. kazana ma'am.. kikubwa ni kujitahidi kukikataa then kila kitu kitakua rahisi kuliko unavyodhani..
Mi siku hizi nimezoea.. asubuhi lazima nifanye mazoezi..then Maji ya uvuguvugu yenye asali.Limao na mdalasini.. wanga na mafuta nimeshapumzika muda wa mwezi sasa...
Kitambi byebyee... no supplement wala nini...
Am really happy now..ukiniangalia utapenda.
 
ulaji nahisi
okey
kama alivyoshauri mdau mmoja hapo juu. Haya mambo yanahitaji kujitoa, kuvumilia na pia kubadili mfumo wa maisha (hasa katika ulaji). Bila ya hivyo unaweza kupungua kutokana na mazoezi, dawa au namna unavyokula.. ukirudi normal life weight inarudi kwa kasi ya ajabu. Best option ni kutafuta long lasting solution nayo ni kufanya mazoezi na kuwa makini na ulaji wetu.
 
Back
Top Bottom