Tumbo kuunguruma

Tumbo kuunguruma

Mara nyingi tumbo langu huunguruma kama vile mtu anajamba,wakati mwingine nipo na watu basi ninaibu,hii inasababishwa na nini?
Zingatia ulaji, yaweza kuwa.....
  • Unakula kwa mama lishe vyombo sio visafi. Mama lishe wengi mpaka abadili maji ya kuoshea vyombo ni janga halaf vyombo hawakaushi. Jaribu kuzingatia hili.
  • Unakula hovyo vyakula visivyokidhi viwango vya kuiva na hata pengine vina virutubishi vya kuongeza wingi kama hamira
  • Haunawi mikono sawasawa
  • Una minyoo,
  • Unamaliza kula na muda huo unakunywa maji ya baridi au matunda.
Jaribu kufanya marekebisho. Maumivu yakiendelea, Nitafute PM nikupe tiba. Msiseme kwanini usitoe hapa, sitaki kutoa hapa mimi sio dokta wa JF
 
Aache kula viporo vyote ikiwemo mikate, keki na maandazi ya Azam na wazalishaji wengine. Maana mikate ni viporo.

Ni wanadamu wachache hawali viporo, inategemea vimetunzwaje na vinaandaliwaje vikitakiwa kuliwa tena.

Mfano, Hotel zote hadi za hadhi ya nyota 5, wanalisha watu viporo.
Punguza kula viporo maana vinasababisha Gesi
 
Mara nyingi tumbo langu huunguruma kama vile mtu anajamba,wakati mwingine nipo na watu basi ninaibu,hii inasababishwa na nini?
Mkuu; kama hakuna maumivu yoyote au kuharisha:
Fahamu kwamba tumbo kwa ujumla wake (Stomach & Intestines)siku zote na muda wote hujigeuza-geuza (Peristaltic movements) na katika mwondoko wake huo hutokea wakati mwingine hewa ambayo ni kitu cha kawaida sana tumboni yaweza kuminywa au kusukumwa kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine(Hiyo ni tofauti kabisa na kujamba) na hewa hiyo iliyominywa (pressurized stomach gas) hutoa mlio humo ndani ya tumbo au utumbo mwembamba. Hilo lisikupe shida ni kitu cha kawaida sana esp. unapokuwa na njaa. Unaweza kupunguza hiyo hali lakini kamwe mtu hawezi kuiondoa isiwepo kabisa. Ni kitu cha kimaumbile. Unaweza kupunguza hali hiyo kwa kunywa club soda au huku Umasaini ndani-ndani huwa tunakunywa maji yenye magadi. Maji yenye Magadi ni alkaline.
Lakini hali kama inakusumbua zaidi waone Wataalam wa Afya wataweza kukupa mwongozo zaidi.
 
Hii kitu nakumbuka iliwahi nitesa sana nikiwa collee.
The easiest way ya kuitibu ni kunywa a glass or 2 of water right after kuamka asubuh.
Kuna science hapo kati ya acid inayotengenezwa mdomoni while you sleep kukwenda kuua ma bakteria tumbon if you drink water after you wake up.
Haijawahi nisumbua tena
Binafsi hua naamka saa tisa usiku kunywa maji hivi inaweza kua alarm ya tatizo lolote la kiafya?

OSEFUKANY
 
ni stage katika kujitafuta kiuchumi ndugu nakumbuka hilo lilinikuta kabla sijaoa na kuwa na familia
ile kipindi cha kigetogeto wala sishangai
 
Back
Top Bottom