Tumbo linawaka moto kama kuna maji ya kuunguza yanamwagwa tumbo

Tumbo linawaka moto kama kuna maji ya kuunguza yanamwagwa tumbo

Naombeni msaada naungua tumbo, mbavu zinauma yaan sina raha, mgongo unauma vichomi kwenye mbavu na wakati mwingine kifuani
Pole sana mkuu.

Inabidi kwenda hospitali lakini kabla hujaanza safari tumia app yetu ya Afya Mingle kuchat na madaktari na wataalamu wengine wa afya watakupa namna ya kudeal na tatizo lako kitaalam zaidi.

Bofya Afya Mingle - Apps on Google Play
 
Wahi hospitali mkuu, Don't waste time in Social media.
Namsikitikia sana jamaa,siyo kwamba hospital hataki kwenda shida anaenda na hela gani?

Matibabu Tanzania ni gharama sana kwa maskini sisi huishia kuomba ushauri kama hivi mitandaoni tukisubiri labda kuna atakeyeandika dawa fulani tukanunue dukani tutumie tusubiri matokeo.
 
Matibabu nigharama kila sehemu, acha awahi hawez kosa pesa yakupima
 
Namsikitikia sana jamaa,siyo kwamba hospital hataki kwenda shida anaenda na hela gani?

Matibabu Tanzania ni gharama sana kwa maskini sisi huishia kuomba ushauri kama hivi mitandaoni tukisubiri labda kuna atakeyeandika dawa fulani tukanunue dukani tutumie tusubiri matokeo.
Hajaeleza hali yake kwamba hana fedha au ni Masikini - Sasa wewe umejuaje hilo?
 
Hajaeleza hali yake kwamba hana fedha au ni Masikini - Sasa wewe umejuaje hilo?
Rudi pale juu mkuu msome katikati ya mistari then njoo uniambie (ktk mazingira ya kawaida tu) kwa namna alivyoandika kwa uchungu angekuwa na uhakika wa kwenda hospital kumuona specialist fulani pamoja na kupata vipimo sahihi angekuwa anasubiri comments za wadau hapa zimpe matibabu?

Mimi naishi mtaani nayajua mazingira humo mahospitalini nimezunguka sana hakuingiliki kiwepesi wepesi labda uwe na mafua maradhi serious kama hivi ujipange hasa.
 
Naombeni msaada naungua tumbo, mbavu zinauma yaan sina raha, mgongo unauma vichomi kwenye mbavu na wakati mwingine kifuani
Mkuu hizo ni dalili za ugonjwa wa vidonda vya tumbo ama gesi(gastris), jaribu dawa inaitwa omeprazole kidonge(capsule) 1×1 kwa siku30.

Dawa hiyo inashusha kabisa na kuponesha kabisa 'kilungulila' pamoja na vidonda vya tumbo.

Unatakiwa uimeze nusu saa kabla ya kula, kila siku muda huo huo, pia punguza kiwango chako cha ulaji pamoja na kuacha kula vyakula flani flani utakavyoshauriwa na dk.

Hilo nimekupa kama angalizo tu, fika hospitali upesi kacheki Bp, kipimo kinaitwa proton pump(kuangalia ufanyaji kazi wa viungo vyako vya ndani tumboni) pamoja na ushauri sahihi wa daktari
 
Back
Top Bottom