SIku zote mwovu huwa ni muoga wa uovu wake, hasa ukijulikana kwa wengi.
Toka mwanzo, Tume ile iliyoundwa na mtuhumiwa namba 1 wa Mauaji ya 29 Oktoba, wengi waliistukia na kusema ni tume bandia inayotaka kuwapumbaza wananchi na jamii ya kimataifa, lakini lengo lake kubwa likiwa kutafuta namna ya kumsafisha kiongozi mkuu wa mauaji. Wengi waliipuuza na kuamua kitoipatia ushirikiano wowote ule.
Lakini tupo ambao tulibakia katikati, tukiwa hatuna uhakika wa moja kwa moja kama hao wajumbe wa tume walioteuliwa na mtuhumiwa watakubali kuharibu majina yao, na kuungana na mtuhumiwa wa mauaji kumtetea kupitia hiyo tume bandia.
Lakini yanayoendelea sasa, hakuna shaka tena kuwa Tume hiyo ni sehemu ya wauaji, haina dhamira yoyote ya kutaka kupata ushahidi wa uhakika jinsi mauaji ya maelfu ya watu yalivyofanyika.
NB: Mahali popote, watu waovu wakitaka kutekeleza uovu wao, kitu cha kwanza ambacho huwa wanafanya, ni kuzuia au kuzima mawasiliano, ili wanapofanya uchafu au uharamia wao, usijulikane.
Wote tu mashahidi, yule muuaji kabla hajatekeleza mauaji, aliminya uhuru wa vyombo vya habari, kisha alifungia mitandao ya kijamii, alipoona haitoshi, akaamua kuzima internet moja kwa moja, kisha akafanya mauaji ya maelfu ya watu.
Na tume aliyoichagua nayo imeanza kufuata njia hiyo hiyo. Ilipoona watu wamesusia, ilijifanya inataka kupata habari toka kwa watu wengi, wakawa wanawaalika na wanahabari. Baada ya kuona wananchi walioshuhudia ushetani mkubwa uliofanywa na yule bibi na watu wake, wakizidi kuongezeka, na kuweka wazi jinsi mashetani yale yaliyoletwa toka Zenji na mengine ya huko huko Tanganyika yalivyotekeleza ushetani wao, mara moja ile Tume bandia ya mtuhumiwa wa mauaji imepiga marufuku vyombo vya habari kushuhudia maelezo ya mashuhuda, na kuyatangaza, sawa na alichofanya yule muuaji aliyewatuma. Kuzuia vyombo vya habari, itakuwa ni hatua ya mwanzo kuelekea kutekeleza uovu wao.