Pre GE2025 Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kuanza mchakato wa kugawa na kubadili Majina ya Majimbo kuanzia Februari 27, 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Aloleta hiyo Hoja ni Mpuuzi Mkuu.

Na Hilo haliifanyi Tume kua Huru.

Serikali iwajibikie Hoja za LISSU
Alieleta si mpuuzi iwapo tume itakuwa huru kweli kweli bali ni mpuuzi kama amemdanganya Rais Samia kuwa wafungwa wanampenda.
 
Tuangalie nchi jirani yenye Tume Huru ya uchaguzi IEBC yenye mamlaka ya kukata mipaka mipya au kiunda majimbo bunge ya uchaguzu mapya, wakielezea uzoefu wao

FUNZO KUTOKA KENYA KUHUSU MUDA MUAFAKA WA KUPATA MIPAKA YA MAENEO BUNGE. JE

31 January 2025
Nairobi, Kenya

Jaji mkuu wa Kenya akiapisha jopo, bila kumungunya wala kupepesa macho adai ucheleweshaji wa kupatikana wajumbe ni mbinu za wanasiasa / vyama vya siasa kujinufaisha kupata ushindi


View: https://m.youtube.com/watch?v=lJMsgZC-rF4
Shughuli ya kuwatafuta Wajumbe 7 watakaohudumu katika Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka itaanza Jumamosi wakati jopo la mchujo litapoketi kupitia maombi kutoka kwa wawaniaji wanaotaka nafasi 7 za kuwa Wajumbe wa Tume ya Uchaguzi na Mipaka ya Majimbo ya Uchaguzi ya Kenya . Jopo hilo katika kikao chake cha kwanza Ijumaa lilitangaza kuwa mchakato wa kuwachagua makamishna wapya utachukua takriban miezi mitatu na kisha watatuma majina waliofaulu usaili kwa Rais ili kuteuliwa.

More info :


Jopo la kuunda tume mpya ya uchaguzi IEBC likiongozwa na Dkt Nelson Makanda. Picha|Boniface Mwangi

JOPO la kuteua mwenyekiti na makamishna wapya wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) leo Jumatatu inaanza kuchambua jumla ya maombi 1, 848 kutoka kwa watu wanaotaka kujaza nafasi hizo.

Katika taarifa, mwenyekiti wa jopo hilo Nelson Makanda alisema kuwa baada ya shughuli hiyo kukamilika mwishoni mwa juma hilo, watachapisha majina ya wale walioorodheshwa kwa mahojiano.

“Kufikia mwisho wa muda wa kupokea maombi, Jumamosi Februari 15, 2024, tulikuwa tumepokea jumla ya maombi 1,848 kutoka kwa Wakenya wanaotaka kujaza nafasi saba za mwenyekiti na makamishna wa IEBC,” akasema.

“Kwa hivyo, kuanzia Jumatano, Februari 17, 2025 tutachambua maombi hayo kubaini ufaafu wa wanaotaka kujaza nafasi hizo kisha kuchapisha majina ya waliorodheshwa kwa usaili,” Dkt Makanda akaongeza.

Mwenyekiti huyo hata hivyo, hakubaini idadi ya watu waliotuma maombi ya kujaza nafasi ya mwenyekiti na idadi ya wale wanaotaka kujaza nafasi sita za makamishna wa IEBC, akieleza kuwa hilo litabainika baada ya zoezi la uchambuzi wa maombi kukamilika.

Dkt Makanda, kwa mara nyingine, aliwahakikishia Wakenya kuwa jopo hilo litazingatia haki, uwazi na uhitimu katika utekelezaji wa kibarua hicho.

Wiki jana, jopo hilo lilitangaza kuwa kufikia Aprili 25, 2025 litawasilisha kwa Rais William Ruto majina ya watu bora kwa nafasi za mwenyekiti na makamishna wa IEBC.


“Tukiwasilisha majina kufikia Aprili 25, mwenyekiti mpya na makamishna sita wa IEBC watakuwa wemeingia afisini kufikia mwezi Mei mwaka huu,” naibu mwenyekiti wa jopo hilo Lindah Kiome akasema kwenye kikao na wanahabari Februari 7, baada ya mkutano wao mjini Naivasha.

Kulingana na Sheria ya IEBC ya 2024, jopo hilo litawasilisha, kwa rais, majina ya watu watatu bora kwa wadhifa wa mwenyekiti, kisha ateue mmoja wao.

Vile vile, Dkt Makanda na wenzake watawasilisha majina ya watu 14 kwa wadhifa wa makamishina ambapo Rais Ruto atateua sita kati yao.

Saba hao wataingia afisi kujaza nafasi iliyosalia wazi baada ya muda wa kuhudumu kwa aliyekuwa mwenyekiti Wafula Chebukati na makamishana watatu kutamatika mnamo Januari 17, 2023.

Nafasi nyingine nne zilisalia wazi Desemba 2022 baada ya kutimuliwa kwa aliyekuwa naibu mwenyekiti Juliana Cherera na makamishna Wilfred Wanderi, Irene Masit na Justus Nyang’aya
 
TOKA MAKTABA :

27 December 2021


Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali akiwamo Jaji Jacob Casthom Mwambegele.

Rais Samia ateau wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi INEC



Wajumbe wa Tume​


Wajumbe wa Tume

Mhe. Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele

Mwenyekiti wa Tume

Mhe. Jaji wa Rufaa (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk

Makamu Mwenyekiti

Mhe. Jaji wa Mahakama Kuu Asina A. Omari

Mjumbe

Mhe. Balozi Omar Ramadhani Mapuri

Mjumbe wa Tume

Mhe. Magdalena Kamugisha Rwebangira

Mjumbe wa Tume

Mhe. Dkt. Zakia Mohamed Abubakar

Mjumbe wa Tume


Source : INEC | Mhe. Magdalena Kamugisha Rwebangira
 

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele atembelea mafunzo ya Maafisa Waandikishaji Wasaidizi katika Halmashauri ya Morogoro Vijijini


Imewekwa: 24 Feb, 2025

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele leo Februari 23, 2025 ametembelea mafunzo ya Maafisa Waandikishaji wasaidizi ngazi ya Kata katika halmashauri katika Halmashauri ya Morogoro Vijijini, mkoani Morogoro na kujionea washiriki wakifanya mafunzo.

Mhe. Mwambegele alipata fursa ya kuzungumza na washiriki hao wa mafunzo ambapo aliwasisitiza kuwahamasisha wananchi katika maeneo yao kujitokeza kwenye zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linalotarajiwa kuanza Machi Mosi hadi Machi 07, mwaka huu Mkoani Morogoro.

Tume yatoa wito wananchi kujitokeza uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura​


View: https://m.youtube.com/watch?v=2806ZCaSUM4Pia alipata fursa ya kuzungumza nao ambapo aliwasisitiza kuhamasisha wananchi katika maeneo yao kijitokeza katika zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linalotaraji kuanza Machi Mosi hadi Machi 07, mwaka huu 2025 mkoani Morogoro.
 
25 February 2025
Morogoro, Tanzania

Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi wakiongea mkoani Morogoro


View: https://m.youtube.com/watch?v=wY5eOIvMud8Wajumbe hao wakiwemo balozi Omar Ramadhani Mapuri, jaji mstaafu Mbarouk Salim Mbarouk, Jaji Asina A. Omari waliongozana na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele,

Watoa wasia mzito kwa Maafisa Waandikishaji wasaidizi wanaohudhuria mafunzo ya siku mbili wanaotoka mikoa ya Morogoro na Tanga
 
27 February 2025
Dar es Salaam, Tanzania
DR. SLAA BAADA YA KUACHIWA KUTOKA MAHABUSU ALIKOWEKWA SIKU 49, ASISITIZA NO REFORMS NO ELECTION


View: https://m.youtube.com/watch?v=JeDlc_sMxXk
Dr. Slaa mara baada ya kuachiwa huru kutokana na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali kutoa hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi, katibu mkuu huyo wa zamani Dr. Slaa afunguka kuwa anaunga mkono No Reforms No Election
 

27 February 2025
WAKILI wa DK SLAA AFICHUA HAYA BAADA ya MTEJA WAKE KUACHIWA HURU - "MASHITAKA YALIKUWA ya UONGO"...


View: https://m.youtube.com/watch?v=T07byQOUg7w
 
Dkt slaa anapoteza muda tu . Maana haaminiki kwa watanzania na ndio maana hata alivyokuwa ndani hakuna aliyekuwa anahangaika naye.
 
Dr. W. P Slaa awaonya waandishi wa habari ambao ni mhimili wa dola namba 4, kuacha kuwahurumia CCM na vyombo vya dola vya serikali, Mahakama, Tume ya Uchaguzi kwa kutowauliza maswali magumu


View: https://m.youtube.com/watch?v=4WRQXxwBM1Q
Dr. Slaa ni afoka ni kana kwamba Tanzania hakuna chochote kinachoashiria uchafuzi wa uchaguzi, matumizi mabaya ya mfumo haki jinai. Waandishi wanashindwa kuwabana Tume ya Uchaguzi, Bunge, Serikali n.k

Dr. Slaa awataka waandishi kuanza kuvibana vyombo husika , kwa namna ile ile wanavyowabana wapinzani na wanaharakati...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…