Pre GE2025 Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kuanza mchakato wa kugawa na kubadili Majina ya Majimbo kuanzia Februari 27, 2025

Pre GE2025 Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kuanza mchakato wa kugawa na kubadili Majina ya Majimbo kuanzia Februari 27, 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Yale majimbo yanayoitwa mashariki, magharibi, kaskazini na kusini ni bora yakaitwa kwa jina la mji mkuu wa kata au wilaya. Mfano majimbo ya mkoa wa Singida ya Manyoni mashariki na manyoni magharibi, lile la mashariki liitwe Manyoni na lile la magharibi liitwe Itigi kama halitagawanywa na kupata jimbo jingine la Mgandu/Mitundu. Jimbo la Singida mashariki na Singida magharibi, lile la mashariki liitwe Ikungi na lile la magharibi liitwe Sepuka. Jimbo la Singida Kaskazini liitwe Ilongero. Jimbo la Iramba Magharibi na Iramba Mashariki, lile la magharibi liitwe Kiomboi kama halitagawanywa na kupata Jimbo la Misigiri na lile la mashariki liitwe Mkalama endapo wilaya ya mkalama itakuwa na jimbo moja. Kuna wilaya zina majimbo mawili tu ya uchaguzi ambapo kijiografia ni kubwa
 
Vipi kuhusu Majimbo yenye wapigakura wachache kama kule nchi jirani ya Zanzibar, YATAUNGANISHWA?..
 
Nje ya mada japo siyo sana. Mufindi district igawanywe iwe na wilaya mbili. Yaani wilaya Ina square kilomita 6,960. Hii syo sawa kabisa
 
Tunaufuatilia kwa makini mchakato

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi INEC , Jaji wa Rufani, Jacobs Mwambegele anasema makatibu tawala, wale wale waliosikiliza rufani za uchaguzi uliopita wa Serikali za Mitaa na Vijiji 2024 TAMISEMI ndiyo watakaoratibu mipaka mipya na majimbo mapya.

Gerrymandering:
UGAWAJI WA MAJIMBO KWA MINAJILI YA KUJIHAKIKISHIA KURA

Mwanahistoria nguli Mohamed Said wa JamiiForums anatukumbusha - ''Zanzibar chini ya utawala Waingereza hapakuwa na wizi wa kura. ASP walikuwa wanashindwa kupitia gerrymandering. Huu ni ujanja katika kukata majimbo ya uchaguzi. gerund or present participle: gerrymandering manipulate the boundaries of (an electoral constituency) so as to favour one party or class "


Ramani ikionesha mikoa mipya ya Simiyu, Geita, Katavi, Njombe, Songwe na ule mpya unaopigiwa chapuo mkoa wa Chato uanzishwe.
1740592364089.png

Picha maktaba: mfano kuonesha michezo ya kugawa majimbo kwa kuangalia CCM ijikusanyie wabunge wengi kupitia idadi kubwa ya majimbo bunge yenye idadi ndogo ya wapiga kura.




Ni kweli kwa ajili ya kupeleka huduma karibu na wananchi au ni kwa ajili ya kujiongezea viti vya ubunge na nafasi zingine za kuendelea kutawala?

1740592273511.png

Ramani ya mikoa, iliyogawiwa kwa ustadi wa kuzingatia ushindi


Gerrymandering ni kutengeneza mipaka ya majimbo bunge mengi lengo ili kuhakikishia kupata wabunge wengi na kushinda uchaguzi.

Gerrymandering is to manipulate district boundaries, for political advantage.

gerrymandering
  1. manipulate the boundaries of (an electoral constituency) so as to favour one party or class.
    • achieve (a result) by gerrymandering.
      "an attempt to gerrymander the election result
 
Naona No reform No Election ya Lissu inaanza ku sound masikioni mwa viziwi!
 
TANZANIA INAWEZA KUPATA MIPAKA YA MAJIMBO YA UBUNGE / MAJIMBO BUNGE MAPYA KABLA YA OCTOBER 2025 ?

Tuangalie nchi jirani yenye Tume Huru ya uchaguzi IEBC yenye mamlaka ya kukata mipaka mipya au kiunda majimbo bunge ya uchaguzu mapya, wakielezea uzoefu wao

FUNZO KUTOKA KENYA KUHUSU MUDA MUAFAKA WA KUPATA MIPAKA YA MAENEO BUNGE. JE


MUUNGANO wa mashirika ya kijamii umesisitiza kuwa uainishaji wa mipaka unaweza kufanywa kabla ya uchaguzi mkuu wa 2027.


IEBC-CHAIR-MAKANDA-1320x792.jpg

Dkt Nelson Makanda akila kiapo cha Jopo la Kuunda IEBC katika Mahakama ya Juu, Januari 27, 2025. Ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa jopo hilo. Picha|Dennis Onsongo.

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ilifaa kuratibu upya mipaka ya ndani ya nchi kufikia Machi 2024 lakini hakukuwezekana kwa sababu ya kukosa tume kamili baada ya muhula wa baadhi ya makamishna kupita, wengine kujiuzulu ama kutimuliwa.

View: https://m.youtube.com/watch?v=XHm6JTZ4c3g
Kwenye kikao na wanahabari jijini Nairobi mwishoni mwa wiki, viongozi wa muungano huo kwa jina “Uchaguzi Platform” walipuuzilia mbali hofu ya Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang’ula kwamba zoezi hilo haliwezi kukamilishwa kutokana na kukosekana kwa muda wa kutosha.


Akiongea mjini Naivasha, Bw Wetang’ula alielezea hofu kuhusu uwezekano wa kuundwa kwa maeneo bunge mapya kabla ya uchaguzi ujao, kutokana na kucheleweshwa kwa uteuzi wa makamishna wapya wa IEBC.

Alieleza kwa kuwa muda wa makataa wa kukamilishwa kwa zoezi ulipita, itakuwa vigumu kwa makamishina wapya kukamilisha shughuli hiyo haraka ili maeneobunge mapya yatumike katika uchaguzi mkuu wa 2027.

“Kutokana na kucheleweshwa kwa shughuli ya uteuzi wa makamishna wapya, haitawezekana kuundwa kwa maeneobunge mapya kuongezea idadi ya sasa ya 290,” Bw Wetang’ula akasema Jumatano alipohutubu katika mkutano wa kukadiria utendakazi wa wabunge kufikia katikati mwa muhula.


Lakini Mshirikishi wa Kitaifa wa Waangalizi wa Uchaguzi (ELOG) Mulle Musau na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuchanganua Sheria za Uchaguzi na Utawala Afrika (ELGIA) Felix Odhiambo wanashikilia kuwa IEBC bado inaweza kuunda maeneobunge mapya.

vlcsnap-2025-02-02-16h31m08s934.png
Mshirikishi wa Kitaifa wa ELOG Mulle Musau akizungumza na wanahabari Jumatano Februari 29, 2025. Picha|Charles Wasonga
“Hili ni suala la kikatiba na Spika Wetang’ula hana mamlaka ya kutoa ufasiri wake kulihusu. Makamishina wapya watakaoteuliwa na jopo ambalo sasa limeanza kazi wanaweza kutekeleza zoezi la uainishaji wa mipaka wakipata ushauri kutoka kwa Mahakama ya Juu. Spika akome kabisa kupoteza matumaini ya Wakenya ambao wangetaka maeneobunge yao yagawanywe ili wapate uwakilishi mzuri,” Bw Mulle akasema.

Kwa upande wake, Bw Odhiambo alielezea imani kuwa makamishina wapya wanaweza kukamilisha zoezi hili akifichua kuwa tayari sekritariati ya IEBC imekamilisha asilimia 60 ya shughuli hiyo.

“Ni asilimia 40 pekee ya kazi ya uainishaji mipaka ya maeneo wakilishi imesalia na makamishina wapya wanaweza kuikamilisha ndani ya muda wa miezi sita baada ya wao kuingia afisini. Kwa hivyo, kiongozi wa hadhi ya Spika Wetang’ula asiibue hofu kwamba huenda baadhi ya Wakenya wakakosa haki yao ya uwakilishi sawa katika uchaguzi mkuu wa 2027,” akaeleza kwenye kikao jijini Nairobi.

Wawili hao, waliandamana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kupambana na Ufisadi Transparency International, tawi la Kenya, Sheila Masinde na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kutetea Demokrasia ya Vyama Vingi (CMD) Frankline Mukwanja.

vlcsnap-2025-02-02-16h30m50s134.png
Mkurugenzi Mtendaji wa Transparency International Kenya Sheila Masinde akizungumza na wanahabari kuhusu uundaji wa IEBC kabla ya uchaguzi wa 2027. Picha|Charles Wasonga
Kulingana na kipengele cha 89 cha Katiba, shughuli ya uainishaji upya wa mipaka ya maeneo wakilishi inapaswa kufanywa baada ya muda usiopungua miaka minane au kuzidi miaka 12.

Shughuli hiyo ilifanyika mwisho mnamo Machi 2012 ambapo idadi ya maeneo bunge iliongezwa kutoka 210 hadi 290. Idadi ya wadi pia iliongezwa hadi 1, 450.

Kwa hivyo, muda wa mwisho wa kukamilishwa kwa awamu nyingine ya shughuli hiyo ulikuwa Machi 2024.

Lakini, wakati huo IEBC haikuwa na makamishina baada ya kukamilika kwa muhula wa aliyekuwa mwenyekiti Wafula Chebukati na makamishna Boya Molu na Abdi Guliye mnamo Januari 17, 2023.



Viongozi wa vuguvugu la Uchaguzi Platform pia wameitaka serikali kuu na wabunge kuliunga mkono jopo jipya la uteuzi wa makamishna wa IEBC ili liweze kukamilisha kibarua hicho kwa wakati.

“Tunaamini kuwa kupitia ufadhili mzuri kutoka kwa serikali, kutoingiliwa na viongozi wa serikali na wanasiasa, jopo hilo linaweza kukamilisha kazi yake hata ndani ya miezi miwili,” akasema Bi Masinde.

“Kile ambacho jopo hili linahitaji sasa ni mazingira mazuri na nia nzuri kutoka kwa viongozi wa taifa hili,” Bw Mukwanja akaongeza.

Aidha, walitoa wito kwa serikali kurahisisha taratibu za kupatikana kwa vitambulisho vya kitaifa ili vijana waliofikisha miaka 18 wapate hati hizo kwa urahisi ili wajiandikishe kuwa wapiga kura
 
Yale majimbo yanayoitwa mashariki, magharibi, kaskazini na kusini ni bora yakaitwa kwa jina la mji mkuu wa kata au wilaya. Mfano majimbo ya mkoa wa Singida ya Manyoni mashariki na manyoni magharibi, lile la mashariki liitwe Manyoni na lile la magharibi liitwe Itigi kama halitagawanywa na kupata jimbo jingine la Mgandu/Mitundu. Jimbo la Singida mashariki na Singida magharibi, lile la mashariki liitwe Ikungi na lile la magharibi liitwe Sepuka. Jimbo la Singida Kaskazini liitwe Ilongero. Jimbo la Iramba Magharibi na Iramba Mashariki, lile la magharibi liitwe Kiomboi kama halitagawanywa na kupata Jimbo la Misigiri na lile la mashariki liitwe Mkalama endapo wilaya ya mkalama itakuwa na jimbo moja. Kuna wilaya zina majimbo mawili tu ya uchaguzi ambapo kijiografia ni kubwa
Naunga Mkono hoja yako kwa asilimia zote
 
Mbeya mjini igawaywe Sugu na Tulia washirikiane kuwaletea maendeleo wana mbeya.

Anaepiga kelele za no election Tanzanians wamempuuza.
Kutakuwa na Jimbo la Sisimba na Iyunga...kwa sasa ndio Tarafa mbili zinazounda Mbeya jiji.
 
Maputo , Mozambique

Kigogo wa Tume ya Uchaguzi Mozambique ktk mahojiano exclusive - Mchakato na Uchaguzi uligubikwa na uchafuzi kwa kuingilia Tume Huru ya Uchaguzi ya Mozambique


View: https://m.youtube.com/watch?v=2B_xQtuZLW8

Naibu mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Bw. Fernando Mazanga asema uchafuzi wa uchaguzi na uchafuzi wa chakato wa uchaguzi, Tume haiwezi kusema nani alishinda..

Kwanza kiukweli kulikuwa na Tume mbili zinazosimamia mchakato, moja ni Tume ya Uchaguzi halisi isiyo na meno, na nyingine ni Tume Kificho ya Watu Wachache wa Frelimo waliokuwa na meno, rasilimali fedha na maamuzi ya kupika matokeo asema Fernando Mazanga

Alipoulizwa kuhusu Tume Kificho ya Watu wachache wa Frelimo ikifanyaje kufanya uchachuzi wa mchakato wa mzima wa matayarisho ya uchaguzi, uandikishaji na upigaji kura siku ya uchaguzi tarehe 9 Oktoba 2024 kigogo Fernado Mazanga alifunguka ...

Tume ya Ukweli ya uchaguzi ilinyimwa fedha na wizara ya fedha ya Mozambique na hata pesa zikipotolewa kidogo zote zikitumika makao makuu ya tume huku mikoani, wilayani na mitaani wasimamizi na wasimamizi uchaguzi walikuwa hoi si kifedha bali hata kimafunzo ya kuwapa uwezo wa kuandikisha wapiga kura, uteuzi na rufaa za mapingamizi.

Wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi walikuwa hawaelewi kanuni, sheria na miongozo ya kufanikisha uchaguzi ulio wa kiwango cha kukubalika ni huru, usiopendelea upande wowote na wakuweza kutoa matokeo sahihi ya kura zilizopigwa na mgombea yupi kazoa kura halali.

Fernando Mazanga anaongeza kuwa kutokana na Tume halisi kunyimwa uwezo wa kila aina, Tume kificho ya FRELIMO iliingia kazi kutangaza idadi ya watu waliojiandikisha ambayo haiwiani na takwimu za sensa ya taifa ya Mozambique ikiyofanyika 2023.

Wasimamizi wakuu na wasimamizi wasaidizi katika majimbo na wilaya walikosa kuwa na idadi za kulinganisha idadi ya watu katika maeneo yao ya majimbo, wilaya, kata na mitaa hivyo kura za ziada ya kuongezwa na FRELIMO ziliweza kutangazwa.

Huku wananchi hawafahamu idadi ya watu rasmo ktk maeneo yao kama sensa ya taifa ilivyokuwa ikionesha eneo kwa eneo, kijiji kwa kijiji, mtaa na kata.

Ingawa vyama makini vya upinzani zilipiga kelele kuwa idadi ya kuandikishwa watu katika sensa hailingani idadi ya wapiga kura watarajiwa na kura za matokeo yaliyotangazwa zimezidi kwa mbali idadi ya watu katika ripoti za sensa za taifa .

Wananchi baada ya kustuliwa kuhusu wafanye rejea za idadi ya watu na idadi ya wapiga kura wakabaini uchafuzi uliofanyika na kupelekea maandamano nchini Msumbiji kupinga matokeo yaliyotangazwa.

Mahakama ya Kikatiba iliyopewa mamlaka kusikiliza mapingamizi ya matokeo, imeomba tume ya uchaguzi ya taifa iwasilishe nyaraka ili ukaguzi ufanyike. Tume ilipewa siku 8 iwe imewasilisha nyaraka zote za uchaguzi uliofanyika 9 Oktoba 2024 zipitiwe na kufanyiwa ukaguzi wa kina.

Bw. Fernando Mazanga Naibu mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Mozambique anasema siku 8 zimepita na zinaonesha kuwasilishwa nyaraka zote zilizohifadhiwa katika Ofisi za Majimbo na Wilaya.

Lakini pamoja na nyaraka hizo kukusanywa sehemu, Mahakama ya Kikatiba hawajapewa makaratasi hayo ya kura na rejister za wapiga kura leo.

Inasemekana serikali inalaumu kutofika makaratasi hayo kutokana na vurugu za maandamano, lakini kigogo huyo Fernando Maganza anatillia shaka sababu hiyo kuwa vurugu zimezuia katatasi hizo kufika mji mkuu wa Mozambique Maputo.

Pengine Tume fiche ya Uchaguzi ya FRELIMO imeshikilia makaratasi hayo katika kituo salama (safe house) ikiyapitia matokeo hayo ya uchafuzi wa uchaguzi na kujiuliza wayawasilishe au la. Pia wanatafuta njia nyingine ya kuingilia mchakato wa Mahakama ya Kikatiba n.k n.k kujiokoa kutoka skandali hilo zito.

Fernando Mazanga alipoulizwa kama matokeo yanaweza kufutwa kutokana na uchafuzi wa wazi wa mchakato na uchaguzi sawia, kigogo huyo mzalendo wa Tume Halisi ya Uchaguzi anasema hawezi kutoa mawazo yake sasa kwa kuwa yeye ni mtu wa ndani kabisa katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mozambique.

Hivyo anaiachie Mahakama ya Kikatiba ibebe majukumu yake kuhakiki na kutoa hukumu sahihi baada ya kujiridhisha na ushahidi wote anahitimisha naibu mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa nchi Mozambique Bw. Fernado Mazanga.

Muito Abrigado kwa kutusikiliza
Source : DW Português para África : DW Kireno Africa

More info :
Maputo, Mozambique
Mahakama ya Katiba Mozambique yataka wasimamizi wa uchafuzi wa uchaguzi kujitetea madudu ya wazi yaliyojitokeza katika uchaguzi wa 9 Oktoba 2024 nchini Mozambique
1740593930956.jpeg

Picha : Waheshimiwa majaji wa Mahakama ya Kikatiba Mozambique


Kiongozi wa Upinzani nchini Mozambique Bw. Venancio Mondlane:

25 February 2025
Venâncio Mondlane Atoa Hotuba Yenye Nzito iliyogusa Inhambane - Afichua mambo kibao ..



View: https://m.youtube.com/watch?v=9TBk1ZfbaqQ
 
A
Yale majimbo yanayoitwa mashariki, magharibi, kaskazini na kusini ni bora yakaitwa kwa jina la mji mkuu wa kata au wilaya. Mfano majimbo ya mkoa wa Singida ya Manyoni mashariki na manyoni magharibi, lile la mashariki liitwe Manyoni na lile la magharibi liitwe Itigi kama halitagawanywa na kupata jimbo jingine la Mgandu/Mitundu. Jimbo la Singida mashariki na Singida magharibi, lile la mashariki liitwe Ikungi na lile la magharibi liitwe Sepuka. Jimbo la Singida Kaskazini liitwe Ilongero. Jimbo la Iramba Magharibi na Iramba Mashariki, lile la magharibi liitwe Kiomboi kama halitagawanywa na kupata Jimbo la Misigiri na lile la mashariki liitwe Mkalama endapo wilaya ya mkalama itakuwa na jimbo moja. Kuna wilaya zina majimbo mawili tu ya uchaguzi ambapo kijiografia ni kubwa
sawa kabisa majina yaweza kamili mfano ,IDODI, Saramka, kitwilu nk
 

Vijana Kenya wadai wanastahili kiti katika Tume Mpya ya IEBC - Angel Mbuthia



View: https://m.youtube.com/watch?v=5k7IHXeho9Q

IEBC siyo ya wazee tu, hata vijana nao wanatakiwa kupewa kiti katika jopo la wajumbe IEBC washiriki katika maamuzi mazito ya mustakhabali wa uchaguzi mkuu

N.B
Je vijana Tanzania sisi ni taifa la kesho tungoje hadi tumezeeka ili kuingia kama vijana katika INEC kuamua mipaka na majimbo mapya ?

1740595258666.jpeg

1740595335167.jpeg
 
Tanzania inatarajia kuingia kwenye historia mpya ya kisiasa ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu baada ya Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania (INEC) kuweka wazi utaratibu wa kuwashirikisha wafungwa kwenye upigaji wa kura kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mbali ya kujumuishwa kwa kipengele hicho pia INEC imetoa utaratibu wa wagombea Urais kuandika barua kwa tume hiyo iwapo wataamua kujitoa kwenye uchaguzi.
 
Ni bora Wafungwa kupiga kura kuliko Majini ya Bakwata.
 
Tanzania inatarajia kuingia kwenye historia mpya ya kisiasa ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu baada ya Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania (INEC) kuweka wazi utaratibu wa kuwashirikisha wafungwa kwenye upigaji wa kura kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Mbali ya kujumuishwa kwa kipengele hicho pia INEC imetoa utaratibu wa wagombea Urais kuandika barua kwa tume hiyo iwapo wataamua kujitoa kwenye uchaguzi.
chimbo jipya la kuibia kura
 
Tanzania inatarajia kuingia kwenye historia mpya ya kisiasa ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu baada ya Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania (INEC) kuweka wazi utaratibu wa kuwashirikisha wafungwa kwenye upigaji wa kura kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Mbali ya kujumuishwa kwa kipengele hicho pia INEC imetoa utaratibu wa wagombea Urais kuandika barua kwa tume hiyo iwapo wataamua kujitoa kwenye uchaguzi.
Aloleta hiyo Hoja ni Mpuuzi Mkuu.

Na Hilo haliifanyi Tume kua Huru.

Serikali iwajibikie Hoja za LISSU
 
Huko ndio wizi utakuwa mkubwa maana hakuna mawakala
 
Nashauri siku ya kupiga kura wafungwe walishwe chakula kizuri na soda ,maji plus magodoro safi ya kulallia!ole wenu nasema msitekeleze!
 
Back
Top Bottom