Pre GE2025 Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kuanza mchakato wa kugawa na kubadili Majina ya Majimbo kuanzia Februari 27, 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Nimeona watu wa Tume ya Uchaguzi eti wamefungua mchakato wa kuongeza na kugawa majimbo mengine.

Kwanza hakuna sababu za msingi za kuongeza idadi ya majimbo ya uwakilishi ikiwa tayari tuna Wabunge wa Viti Maalumu karibu 1/3 ya Wabunge Wote.Aisha Tanzania ni Kati ya Nchi yenye Wabunge wengi.

Kuongeza Majimbo ni kielelezo Cha ubinfsi wa Hali ya Juu wa Wanasiasa ambao wanajali matumbo Yao.

Kama Rais amekuwa anakataa kuongeza maeneo ya Utawala iweje Tume ya Uchaguzi itake kuongeza Wabunge wengine?

Mbunge ana kazi gani hiyo inayomtagiza Kuwafikia Wananchi? Haya ni matumizi mabaya ya Rasilimali za Nchi katika mazingira ambayo Vijana wanahangaika na Ajira,ongezeko kubwa la watu wanahitaji Huduma za jamii na kiuchumi sanjali na Changamoto zingine za Nchi kimiundombinu.

View: https://www.instagram.com/p/DGiMOcXt_wB/?igsh=a2pzZ205ZW1oNnZr

My Take
Kuongeza Majimbo ya Uchaguzi ni kumuongezea mzigo wa Kodi mwananchi.

Napinga hili Kwa Nguvu zote,Naomba Serikali ilitazame upya jambo hili.
 
Hili halikubaliki kabisa na ni ibinafsi wa Hali ya Juu ndio maana nawachukia Wanasiasa na siasa kasoro SSH.

Nita mtag akatae jambo hili.Wabunge wanatosha.
Dunia ya Sayansi na Teknolojia Kila mkoa ungetoa Wabunge wawili tu 😂

Pale DOGE USA Watumishi ni 20 tu wanafuatilia utendaji wa Majimbo yote na kutoa Ripoti Kila Wiki
 
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza kuanza kwa mchakato wa kuchunguza na kugawa au kubadili majina ya majimbo ya uchaguzi ambapo itapokea mapendekezo kuanzia tarehe 27 Februari, 2025 hadi tarehe 26 Machi, 2025.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufani, Jacobs Mwambegele leo tarehe 26 Februari, 2025 muda mfupi baada ya kumaliza kuongoza kikao cha Tume kilichofanyika mkoani Morogoro.

“Kwa kuzingatia masharti ya Kanuni ya 18(1) ya Kanuni za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi za mwaka 2024, napenda kutoa taarifa kwa umma kwamba, kuanzia kesho siku ya Alhamis tarehe 27 Februari, 2025 Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi itaanza mchakato wa kuchunguza na kugawa au kubadili majina ya majimbo ya uchaguzi,” amesema Jaji Mwambegele.

Akifafaunua kuhusu muda wa kupokea maombi, Jaji Mwambegele amesema “maombi yote ya kugawa au kubadilisha jina la jimbo yawasilishwe Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kuanzia tarehe 27 Februari, 2025 hadi tarehe 26 Machi, 2025”.

Jaji Mwambegele amesema Tume inatekeleza jukumu hilo kwa mujibu wa ibara ya 74(6)(c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na kifungu cha 10(1)(d) cha Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Na. 2 ya Mwaka 2024, ambapo Tume imepewa jukumu la kuchunguza mipaka na kuigawa Jamhuri ya Muungano katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya uchaguzi wa Wabunge.

Ameeleza kuwa kwa mujibu wa ibara ya 75(4) ya Katiba, jukumu hilo la kuchunguza mipaka na kugawa Jamhuri ya Muungano katika majimbo ya uchaguzi linaweza kufanywa na Tume mara kwa mara na angalau kila baada ya miaka kumi.

“Kwa kuzingatia masharti hayo ya Katiba, kwa mara ya mwisho Tume ilichunguza mipaka na kugawa majimbo ya uchaguzi katika Jamhuri ya Muungano mwaka 2015, ambapo majimbo mapya 26 yalianzishwa,” amesema.

Jaji Mwambegele amewakumbusha wadau wote wenye maombi wahakikishe kuwa mapendekezo yanajadiliwa katika Kamati ya Ushauri ya Wilaya, kisha yawasilishwe kwa Katibu Tawala wa Mkoa kwa ajili ya kujadiliwa katika Kamati ya Ushauri ya Mkoa na Katibu Tawala wa Mkoa awasilishe Tume mapendekezo yaliyopitishwa na kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa pamoja na viambatisho vyote.

Kupata taarifa na matukio ya kimkoa kuhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

===
Ndugu zangu Watanzania,

Mchakato wa Kugawa na kubadili Majina ya Majimbo kuanza Kesho.Ambapo maoni ya wadau yataanza kupokelewa.

Ambapo wadau Mnakaribishwa kwa ajili ya kutoa maoni yenu. Hapa bila shaka itaangaliwa na kuzingatiwa ukubwa wa jimbo na idadi ya watu na jiografia ya eneo. Ambapo kuna majimbo Yamekuwa makubwa sana na idadi kubwa ya watu imeongezeka na inaendelea kuongezeka siku hadi siku..

Ambapo kuhudumiwa na kuwakilishwa na mbunge mmoja tu pekee inakuwa ni changamoto kubwa sana katika kutoa uwakilishi mzuri.

Japo mbunge mmoja au gharama za kumuhudumia Mbunge mmoja ni kubwa sana .ambapo inakadiliwa Kuwa kuanzia posho,misharaha mpaka kiinua mgongo chake kwa miaka mitano ya Mbunge inakadiliwa kufikia Billion Moja.

Lakini ni lazima tukubaliane na ukweli kuwa hiyo ndio demokrasia na ndio gharama pia ya demokrasia ambayo haikwepeki. Maana mwingine anaweza kusema hakuna sababu ya kuongeza majimbo ilihali huko chini kuna Mkurugenzi wa halmashauri,DC,DAS, Mwenyekiti wa halmashauri na viongozi wengine wengi.

Hivyo hakuna haja ya kuongezwa kwa Majimbo na mbunge ambaye anakwenda kuongeza gharama za malipo yake kama stahiki zake za halali na zilizo kisheria kabisa.. lakini ni ukweli kuwa ni muhimu wananchi kupata uwakilishi wenye tija na wenye kuwakilisha vyema Sauti zao kwa kila mmoja wao kusikika kupitia Mbunge wao.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

Napinga huu upuuzi Kwa Nguvu zote
 
Hiyo inaitwa tume huru ya ccm ya Uchaguzi.
 
Hakuna jipya majimbo ya uchaguzi yanatakiwa kuwa ya kimikoa tu, mbona wakuu wa mikoa wanafika kona zote za mikoa yao, hao wabunge wananshindwa nini?
Wabunge wabaki wawili tu kila mkoa, inatosha mno.
 
Back
Top Bottom