PreGE2025 Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) yaongeza siku mbili uboreshaji daftari la wapigakura Dar

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Hizi nchi zetu kupiga kura sometimes hakuna maana .niko leo kituoni foleni watu wengi ,yaani maswali mengi yakanijia ,hivi nafanya ujinga gani nko hapa? maana mwaka ule uchaguzi uliopita mawakala walinunuliwa na kura zikaibwa..
 
🤣🤣🤣 Mwisho ukala kona
 
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imeongeza siku mbili (Machi 24 na 25) za uboreshaji wa daftari la mpigakura kwa Mkoa wa Dar es Salaam kutokana na mwitikio mkubwa wa wananchi.

Taarifa ya INEC imetolewa leo Machi 23, 2025 na Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Jacobs Mwambegele ikiwa ni siku moja tangu Mwananchi iripoti wingi wa watu vituoni na malalamiko ya baadhi kushindwa kuboresha taarifa zao.

Soma: Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura Dar es Salaam Kufanyika Machi 17-23, 2025. Wapiga Kura wapya 643,420 kuandishwa

Uboreshaji wa taarifa huo awali mkoani Dar es Salaam ulianza Machi 17 na ulitakiwa kumalizika leo Jumapili Machi 23, 2025.

"Kama mnavyofahamu Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi inaendelea na hatua ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapigakura kwa Mkoa wa Dar es Salaam, hatua ambayo kwa mujibu wa ratiba ilianza Machi 17, 2025 na ilitarajiwa kukamilika Machi 23, 2025."

"Kutokana na mwitiko mkubwa Tume ilichukua hatua za kuongeza mashine za bvr kits pamoja na watumishi katika maeneo yote yaliyoonekana kuwa na watu wengi na hatua hii imewezesha shughuli hiyo kuendelea kwa utulivu katika maeneo yote. Hatua hiyo imewezesha kuongeza kasi ya kuwahudumia wananchi na kupunguza kwa kiasi kikubwa misongamano kwenye baadhi ya maeneo,"
imeeleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa: "Licha ya hatua zilizochukuliwa na Tume, bado katika maeneo kadhaa kuna mwitikio mkubwa wa wananchi. Hivyo basi, napenda kuwatangazia wananchi wote wa mkoa wa Dar es Salaam kuwa Tume imeongeza siku mbili za uboreshaji wa daftari kwa Machi 24 na 25, 2025."

Halafu kuna wajinga fulani eti "No Reform, No Election"! Nyambafu!!
 
Una uhakika gani kura yako itatumika kuwapata hao wabunge wapinzani....kwa sasa wabunge ni kama kupeana tu...kilichofanyika 2024 ndicho kitafanyika 2025....wait and see
Sasa nini kifanyike? wananchi hawana imani na bunge hili fake, ninaamini upinzani utapata wabunge wengi sn
 
Tume ya CCM sio tume huru,maana imewekwa na CCM
 
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imeongeza siku mbili (Machi 24 na 25) za uboreshaji wa daftari la mpigakura kwa Mkoa wa Dar es Salaam kutokana na mwitikio mkubwa wa wananchi.

Taarifa ya INEC imetolewa leo Machi 23, 2025 na Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Jacobs Mwambegele ikiwa ni siku moja tangu Mwananchi iripoti wingi wa watu vituoni na malalamiko ya baadhi kushindwa kuboresha taarifa zao.

Soma: Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura Dar es Salaam Kufanyika Machi 17-23, 2025. Wapiga Kura wapya 643,420 kuandishwa

Uboreshaji wa taarifa huo awali mkoani Dar es Salaam ulianza Machi 17 na ulitakiwa kumalizika leo Jumapili Machi 23, 2025.

"Kama mnavyofahamu Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi inaendelea na hatua ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapigakura kwa Mkoa wa Dar es Salaam, hatua ambayo kwa mujibu wa ratiba ilianza Machi 17, 2025 na ilitarajiwa kukamilika Machi 23, 2025."

"Kutokana na mwitiko mkubwa Tume ilichukua hatua za kuongeza mashine za bvr kits pamoja na watumishi katika maeneo yote yaliyoonekana kuwa na watu wengi na hatua hii imewezesha shughuli hiyo kuendelea kwa utulivu katika maeneo yote. Hatua hiyo imewezesha kuongeza kasi ya kuwahudumia wananchi na kupunguza kwa kiasi kikubwa misongamano kwenye baadhi ya maeneo,"
imeeleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa: "Licha ya hatua zilizochukuliwa na Tume, bado katika maeneo kadhaa kuna mwitikio mkubwa wa wananchi. Hivyo basi, napenda kuwatangazia wananchi wote wa mkoa wa Dar es Salaam kuwa Tume imeongeza siku mbili za uboreshaji wa daftari kwa Machi 24 na 25, 2025."

Kwa mujibu wa Ibara ya 74 ya Katiba ya JMT, inatambua uwepo wa Tume ya Uchaguzi, yaani NEC LAKINI siyo Tume Huru ya Uchaguzi (INEC). INEC kwa mujibu wa Ibara hiyo ya Katiba ni Kitu BATILI kwani haitambuliki na Katiba. Marekebisho ya jina la Tume ya Uchaguzi kutoka NEC kwenda INEC yalipaswa kutanguliwa na Marekebisho ya Katiba iliyopo kwanza, hususani Ibara hiyo ya 74.

Katiba inasema kwamba kutakuwa na Tume ya Uchaguzi wala siyo Tume Huru ya Uchaguzi. Mabadiliko haya ya Sheria ya Uchaguzi yaliyosababisha kubadilisha jina la Tume ya Uchaguzi kutoka NEC kwenda INEC ni BATILI kwa mujibu wa Ibara hiyo ya 74 kwani Mabadiliko haya yanakinzana na matakwa ya Katiba ya nchi.

Kwa maana hiyo, Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania (INEC) ni Taasisi au kitu ambacho hakitambuliki na Katiba ya nchi hivyo ni BATILI KWA UJUMLA WAKE. Taasisi hiyo haitambuliki kisheria kwa mujibu wa Ibara ya 74 ya Katiba ya JMT
 
Back
Top Bottom