Uchaguzi 2020 Tume imekataza Viongozi wa Dini kuwa waangalizi wa Uchaguzi Mkuu 2020. Chaguzi zote tangu 1995 viongozi wa Dini walishirikishwa

..labda hii hatua ya kuweka msisitizo kwamba serikali yetu ni secular.
Serikali yetu si secular, rais haishi kumtaja Mungu kwenye mambo ya serikali. Mpaka bunge linafunguliwa kwa dua.

Hawajakataza hili kwa sababu wanataka kuwa secular.

Hawataki viongozi wa dini wapate cha kusema ikiwa kuna figisu kwenye kuiba kura huko.
 

..asante sana kwa kuliona hili.

..umelisema kwa usahihi, na ufasaha, kuliko ambavyo ningelisema mimi.
 
Huku wanasmbiwa Wauombee Uchaguzi kule Hawaruhusiwi kuwa Waangalizi nini Kinaogopwa?
 
TEC NA BAKWATA ni wanachama wa TEMCO (TANZANIA ELECTION MONITORING COMMITTEE) ambayo iko chini ya chuo kikuu cha Dar es Salaam ( UDSM) ambayo kipindi cha nyuma ilikuwa ikisimamiwa na Dr. Bana. Wakati wa chaguzi,kwenye zoezi la uangalizi wa uchaguzi,TEC NA BAKWATA kama wanachama huwa wanatuma nguvu kazi kuja kusaidiana na watu ambao huwa wanatokea hapohapo UDSM kwenye shughuli hizi. Kwa maana hiyo huwa wanashiriki ila si lazima wawe wamevaa kanzu za kuonyesha kuwa huyu ni padre ama ni askofu ama shekhe.
 
Sasa kama mwaka huu kama watakuwa wamezuiwa kama mleta mada anavyosema basi ni tatizo.
 
Wako sahihi ni uamuzi wa busara kwani viongozi wengi wa dini wamejiingiza kwenye ushabiki wa siasa ikiwemo kugombea uongozi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…