Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 1,194
- 911
Na Mwandishi maalum
Kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kuhusu kuundwa kwa Tume ya Uchunguzi itakayochunguza kwa kina yale yaliyobainishwa kwenye ripoti ya Tume ya Rais ya iliyoundwa kuchunguza matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea Oktoba 29, 2025 imeungwa mkono na Watanzania walio wengi, hongera Mhe Rais kwa uamuzi huu.
Ni wazi kuwa, Kiongozi wetu ana maono makubwa yanayolenga kuendelea kuliunganisha Taifa la Tanzania ambalo limeendelea kuwa moja na lenye misingi imara iliyojengwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Waswahili wanasema mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, Watanzania tunaungana na Kiongozi wetu katika kuhakikisha kuwa Tume itakayoundwa inatekeleza majukumu yake ya uchunguzi kwa ufanisi ili nchi yetu iendelee mbele zaidi katika Nyanja zote katika kujenga umoja wa kitaifa ulio imara zaidi.
Akizungumza na moja ya Chombo cha habari Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge ambaye pia ni nguli wa Sheria ameonesha kuwa jambo hili limekuja wakati muafa na litasaidia Taifa kupiga hatua katika kuleta maridhiano na kuimarisha zaidi umoja wa kitaifa.
“Tume imesema kuna watu wamepanga, kutekeleza na kufadhili matukio ya Oktoba 29, 2026,” anaeleza Prof. Kabudi, hivyo ni muhimu Tume itakayoundwa kufanya uchunguzi wa masuala yote ya jinai yaliyobainishwa ikapewa nafasi na ikaaminiwa katika kutekeleza jukumu hili la kiuchunguzi kuhusu masuala yote yaliyoainishwa na ripoti ya Jaji Chande.
Serikali ya Awamu ya Sita ina utashi wa kisiasa katika kujenga umoja wa kitaifa na imekuwa nyakati zote ikifanya kazi kwa kuweka maslahi ya Watanzania mbele nyakati zote. Jukumu letu kama watanzania ni kuangalia tulipotoka, tulipo na tunapotaka kwenda kwa maslahi ya Taifa letu, heko watanzania kwa kuweka mbele maslahi ya Taifa.
“Amani, Umoja na Mshikamano ndio msingi wa maendeleo yetu” Mwl Nyerere alisisitiza kuwa bila amani hakuna maendeleo yoyote yanayoweza kupatikana. Dhamira ya kufanyika kwa uchunguzi wa kina inatuelekeza kwenye kuendelea kutibu tatizo na kuepuka masuala kama haya kujirudia.
Hivi Karibuni, Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Dkt Fredrick Shoo ameonesha wazi kuwa Ripoti ya Tume ya Rais ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani ya Oktoba 29, 2025 imekuja kuliponya Taifa. Jukumu la Kila Mtanzania ni kulinda amani na kuungana na viongozi wetu katika kuwezesha Tume ya uchunguzi itakayoundwa kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. #NeverAgain