GE2025 Tume Uhuru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC): Polepole hana uelewa na ufahamu kuhusu mfumo wa Uchaguzi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imekanusha taarifa zinazodai kuwa mfumo wa uchaguzi unaotumika na Tume hiyo umeunganishwa na mfumo wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na chama cha siasa, hususan Chama Cha Mapinduzi (CCM), pamoja na madai kwamba zoezi la upigaji kura tayari limefanyika.

Mkurugenzi Mkuu wa INEC, Ramadhan Kailima kupitia taarifa ya INEC ya Agosti 23, 2025, amesema taarifa hizo zinazozunguka kwenye mitandao ya kijamii ni za uongo na upotoshaji zenye lengo la kupotosha umma na kuibua taharuki.

“Taarifa hizo za uongo na upotoshaji zinaenezwa na mtu ambaye hana uelewa na ufahamu kuhusu mfumo wa uchaguzi. Daftari la Kudumu la Wapiga Kura halijaunganishwa na mfumo wowote wa Serikali au wa Taasisi binafsi kwa madhumuni ya upigaji kura”, amesema Kailima na kuongeza,

“Taarifa hizo za uongo na upotoshaji zinaenezwa na mtu ambaye hana uelewa na ufahamu kuhusu mfumo wa uchaguzi”.

Kailima amebainisha kuwa Tanzania haitumii mfumo wa kielektroniki katika kupiga kura, kuhesabu kura, au kutangaza matokeo. Badala yake, zoezi hilo hufanyika kwa kutumia utaratibu wa kawaida (manual).

“Ifahamike kuwa, Kitambulisho cha Taifa hakitumiki kupigia kura, bali Kadi ya mpiga kura pekee iliyotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na kuhakikiwa ndiyo inayotumika wakati wa upigaji kura katika vituo vya kupigia kura”, amesisitiza.

Ameongeza kuwa vyama vya siasa vilishapewa Daftari la Wapiga Kura baada ya zoezi la uboreshaji kukamilika, na mawakala wa vyama watatumia daftari hilo kutambua wapiga kura siku ya uchaguzi.

Tume imewataka wananchi kupuuza taarifa hizo, ikisisitiza kuwa zinasambazwa na watu wasiokuwa na uelewa wa mfumo wa uchaguzi nchini.

Tume imewasihi wananchi na wadau wote wa uchaguzi kuupuza uongo na upotoshaji huo, na anayesambaza ana lengo la kuzua taharuki na upuuzwe kama wapotoshaji wengine.

Taarifa hii imetolewa kutokana na madai yaliyotolewa na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, usiku wa tarehe 22 Agosti 2025, ambapo alidai kuwa mifumo ya CCM imeunganishwa na ya INEC na NIDA kwa madhumuni ya kudhibiti matokeo ya uchaguzi.

View attachment 3450171

View attachment 3450172
Wewe Kailima ni muongo mkubwa, Hao viongozi wanaotembelea wafanyakazi kurekodi namba zao za NIDA na vitambulisho vya kura wanafanya kwa minajili gani? Unajua unaongea uongo wewe kada wa CCM kwa sababu mmezoea kuongea uongo ninyi wizi, mafisadi, watekaji na wauaji wakubwa. Wewe Kailima upo kwenye tume huru? Unajua kabisa kuwa unadanganya, Kila kitu mnachofanya ni cha uongo. Huo uchaguzi gani mnaoufanya wa kupingana na vyama mlivyovianzisha na vinavyopokea fedha kutoka kwenu? Mpinzani ni mmoja tu, yule aliyeko gerezani, mmeshindwa kumrubuni, wengine wote including Mbowe mmewalipa na hawaongei lolote. WAONGO NINYI WOTE.
 
INEC ni uwongo ,katiba ya Tanzania haitambuiiiii hiii tume
 
Attachments

  • 20250823_154242.jpg
    20250823_154242.jpg
    29.3 KB · Views: 25
Huyo mkurugenzi Inawezekana akawa na uelewa na mfumo wa uchaguzi na asiye na uelewa na mfumo wa technology ambao mfumo wa uchaguzi uko ndani yake🤣🤣🤣
Kabisa yaani
 
Kama nia ya tume ni nzuri wangekubali reform ili kujenga imani na watu.sahv watz weng hawana imani na tume na tume wanalielewa hilo.pole pole ndyo kawasha MOTO.
Siyo kazi ya Tume kufanya mabadiliko ya Katiba na sheria.
 
Huo upumbavu wawadanganye wajinga waliopo hapo ofisini kwao .

Eti mfumo wa NIDA umeunganishwa na chama kimoja cha siasa[hicho chama hakina jina?]

Eti mtu huyo hana uelewa wa mifumo[hana jina huyo mtu?]
 
1) Kwa nini ameishia namba 8 tu kwenye huo mtiririko wake wa majibu?

2) Matokeo ya mwisho hupatikanaje hasa katika suala la majumuisho na ujumlishaji?

3) Hivi kweli NIDA-card haina uhusiano wowote na INEC-card ya mpiga kura?
 
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imekanusha taarifa zinazodai kuwa mfumo wa uchaguzi unaotumika na Tume hiyo umeunganishwa na mfumo wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na chama cha siasa, hususan Chama Cha Mapinduzi (CCM), pamoja na madai kwamba zoezi la upigaji kura tayari limefanyika.

Mkurugenzi Mkuu wa INEC, Ramadhan Kailima kupitia taarifa ya INEC ya Agosti 23, 2025, amesema taarifa hizo zinazozunguka kwenye mitandao ya kijamii ni za uongo na upotoshaji zenye lengo la kupotosha umma na kuibua taharuki.

“Taarifa hizo za uongo na upotoshaji zinaenezwa na mtu ambaye hana uelewa na ufahamu kuhusu mfumo wa uchaguzi. Daftari la Kudumu la Wapiga Kura halijaunganishwa na mfumo wowote wa Serikali au wa Taasisi binafsi kwa madhumuni ya upigaji kura”, amesema Kailima na kuongeza,

“Taarifa hizo za uongo na upotoshaji zinaenezwa na mtu ambaye hana uelewa na ufahamu kuhusu mfumo wa uchaguzi”.

Kailima amebainisha kuwa Tanzania haitumii mfumo wa kielektroniki katika kupiga kura, kuhesabu kura, au kutangaza matokeo. Badala yake, zoezi hilo hufanyika kwa kutumia utaratibu wa kawaida (manual).

“Ifahamike kuwa, Kitambulisho cha Taifa hakitumiki kupigia kura, bali Kadi ya mpiga kura pekee iliyotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na kuhakikiwa ndiyo inayotumika wakati wa upigaji kura katika vituo vya kupigia kura”, amesisitiza.

Ameongeza kuwa vyama vya siasa vilishapewa Daftari la Wapiga Kura baada ya zoezi la uboreshaji kukamilika, na mawakala wa vyama watatumia daftari hilo kutambua wapiga kura siku ya uchaguzi.

Tume imewataka wananchi kupuuza taarifa hizo, ikisisitiza kuwa zinasambazwa na watu wasiokuwa na uelewa wa mfumo wa uchaguzi nchini.

Tume imewasihi wananchi na wadau wote wa uchaguzi kuupuza uongo na upotoshaji huo, na anayesambaza ana lengo la kuzua taharuki na upuuzwe kama wapotoshaji wengine.

Taarifa hii imetolewa kutokana na madai yaliyotolewa na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, usiku wa tarehe 22 Agosti 2025, ambapo alidai kuwa mifumo ya CCM imeunganishwa na ya INEC na NIDA kwa madhumuni ya kudhibiti matokeo ya uchaguzi.

View attachment 3450171

View attachment 3450172
Hatudanganyiki
nidaNecCCM.jpg
 
Alihusika kwenye instqllation ya mfumo, kwa hiyo wewe kicheche ndio tukuamini?
 
Back
Top Bottom