GE2025 Tume Uhuru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC): Polepole hana uelewa na ufahamu kuhusu mfumo wa Uchaguzi

GE2025 Tume Uhuru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC): Polepole hana uelewa na ufahamu kuhusu mfumo wa Uchaguzi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Inategemea:
1) ustadi wa mdukuzi
2) ubora wa mfumo
3) ujuzi wa mtu (au custodian) aliyedukuliwa
Okay...sasa vipi kuhusu wale waajiriwa wa Serikali na taasisi zake ambao wengi wao wamejifunza IT wakiwa kazini na uperekwa tuu kozi fupi za kufundishwa jinsi ya kutumia mfumo unaotumika..unadhani wanaweza kuwa na utundu/creativity waliyonayo hawa vijana walio kua na laptops kama Toys?! na most probably ndio wanatumiwa na ma-consultants wa Serikali katika kufanya marekebisho au updates za mifumo..?
 
20250823_213811.jpg


Watazunguka wewe lakini mwisho wa siku ni kwamba wote ni zao la ccm.
WaTanganyika wanachotaka ni hiyo mifumo iwe na watu huru ili iwe huru!
 
Nyooo! Hakuna anayewaamini ninyi manyang'au wa tume
 
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imekanusha taarifa zinazodai kuwa mfumo wa uchaguzi unaotumika na Tume hiyo umeunganishwa na mfumo wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na chama cha siasa, hususan Chama Cha Mapinduzi (CCM), pamoja na madai kwamba zoezi la upigaji kura tayari limefanyika.

Mkurugenzi Mkuu wa INEC, Ramadhan Kailima kupitia taarifa ya INEC ya Agosti 23, 2025, amesema taarifa hizo zinazozunguka kwenye mitandao ya kijamii ni za uongo na upotoshaji zenye lengo la kupotosha umma na kuibua taharuki.

“Taarifa hizo za uongo na upotoshaji zinaenezwa na mtu ambaye hana uelewa na ufahamu kuhusu mfumo wa uchaguzi. Daftari la Kudumu la Wapiga Kura halijaunganishwa na mfumo wowote wa Serikali au wa Taasisi binafsi kwa madhumuni ya upigaji kura”, amesema Kailima na kuongeza,

“Taarifa hizo za uongo na upotoshaji zinaenezwa na mtu ambaye hana uelewa na ufahamu kuhusu mfumo wa uchaguzi”.

Kailima amebainisha kuwa Tanzania haitumii mfumo wa kielektroniki katika kupiga kura, kuhesabu kura, au kutangaza matokeo. Badala yake, zoezi hilo hufanyika kwa kutumia utaratibu wa kawaida (manual).

“Ifahamike kuwa, Kitambulisho cha Taifa hakitumiki kupigia kura, bali Kadi ya mpiga kura pekee iliyotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na kuhakikiwa ndiyo inayotumika wakati wa upigaji kura katika vituo vya kupigia kura”, amesisitiza.

Ameongeza kuwa vyama vya siasa vilishapewa Daftari la Wapiga Kura baada ya zoezi la uboreshaji kukamilika, na mawakala wa vyama watatumia daftari hilo kutambua wapiga kura siku ya uchaguzi.

Tume imewataka wananchi kupuuza taarifa hizo, ikisisitiza kuwa zinasambazwa na watu wasiokuwa na uelewa wa mfumo wa uchaguzi nchini.

Tume imewasihi wananchi na wadau wote wa uchaguzi kuupuza uongo na upotoshaji huo, na anayesambaza ana lengo la kuzua taharuki na upuuzwe kama wapotoshaji wengine.

Taarifa hii imetolewa kutokana na madai yaliyotolewa na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, usiku wa tarehe 22 Agosti 2025, ambapo alidai kuwa mifumo ya CCM imeunganishwa na ya INEC na NIDA kwa madhumuni ya kudhibiti matokeo ya uchaguzi.

View attachment 3450171

View attachment 3450172
Kama si KAMBALE huwezi jua mchezo huu utaishia kuingia kwenye mfumo
 
Back
Top Bottom