Tume ya ajira na sharti la kuthibitisha vyeti kwa mawakili na mahakimu

Tume ya ajira na sharti la kuthibitisha vyeti kwa mawakili na mahakimu

wa2 acheni kukalili!we fuata maelekezo yaliyomo kwenye tangazo husika,ila kwa ajira za serikalini,barua lazima iandikwe kwa mkono(sio typing)na ndilo huwa hawasemi!lakini mengine yote husemwa.

hiyo ya kuandika kwa mkono mnaitoa wapi? Mbona mnaendekeza ujima?
 
kiukweli uo ni ufisadi tu wa kutengenezeana ela na mawakili kupitia mgongo wa wabongo wenye shida, ata kitendo cha kusema utume kwa njia ya posta wakati zamani tulikua tunapeleka pale pale direct kwann leo tutumie posta uo pia ni ufisadi ili buku buku za watu mzile bure kazi zenyewe mmeshaweka watoto zenu kiukweli haipendezi ata kidogo.
 
huo ulazima unautoa wapi? Nimewahi pata kazi mbili, pasipo kucertify wala kupeleka vyeti original

Mkuu wewe unasema Vyeti, Kuna Mashirika kibao tena haya ya Nje wao huwa wanataka CV pekee hata barua hawataki, na kinacho kuajiri ni CV na kama ukidanganya kwenye CV inakula kwako kwenye probation period, Vyeti vinatengenezwa sana hujasikia yule mwalimu wa MUCOS aliyekamatwa na matambo wa kutengeneza vyeti?

Kuna shirika Moja la kimataifa lenye kufanya kazi huku Tanzania na nchi zingine, waliwahi kusema sababu ya kuto taka vyeti ni kwa sababu WALIWAHI KUJIRI MTU WA IT mwenye first class lakini alicho fanya kazina hawatakaa wasahau na tangia siku hiyo MABOSI WA HILI SHIRIKA AMBAO NI WAZUNGU HAWATAKI KUSIKIA KITU VYETI, WANATAKA CV PEKEE

 
Sijaambiwa ni certify, wamenambia nitoe nakala za kopi za vyeti, achen longo longo, tatizo le2 wabongo sehem ya kujamba tunataka kuarisha, tufateni masharti ya matangazo husika na si kugeneralise basing on our old schematas.

Wasiwasi ndio akili
mkuu. Mifano ya kujamba na kuharisha inaweza kukupa ushindi kwenye mabishano ya JF lkn umeshajiuliza kama inao uwezo wa kuku-short list kwenye secretariat ikiwa mdau aliyeko kule akili zake zinamtosha mwenyewe?

Wote twajua kuwa Tangazo la tarehe 25 halikutoa maagizo hayo, lkn kwa kutumia busara unaweza kujiuliza kama wanaweza kukuondoa kwa kuwa umecertify au wanaweza kukuondoa ikiwa haukucertify. Jiulize hivi, kama tangazo lao lilikuwa limekosewa kwa kusahau kuweka sharti hilo, halafu lawama wakaziamishia kwako kwamba haukuwa makini kujua kuwa serikalini lazima ucertfy vyeti, Je wewe utajua kwa nini huitwi au utashangaa tu kuona wenzio wameitwa wewe hujaitwa?

Tafakari, chukua hatua!


Shinda ubishi kwenye jamvi au jiwekee tahadhari in case atakayepewa kazi ya kushortlist ni mwehu
 
bumpkin ur ver smart na umejibu vizuri, ila pia naona nimekufuraisha na neno jamba na harisha, kiukwel nimeshatuma na wala sijacertify na hela pia ckua nayo so wasiponishort list mungu atanishortlist, though nimeulza watu wa wizara hucka wamenambia hakuna tatizo kwakua tangazo liko plain.
 
ndugu yangu uko sawa kabisa. Naona matajiri na watoto wao ndio wenye nafasi katika nchi hii na si masikini elfu 25 ya kucertify nakala 10 ama elfu 10 ni pesa nyingi sana kwa m2 aliyemaliza chuo na yuko mtaani. mimi mwenyewe kuna wakati hata ile 2600 ya kutuma barua za maombi ya kazi kwa njia ya register huwa naikosa na kushindwa kuomba kazi sasa haya ya kucertify ndio kabisaa yatanishinda.mimi nafikiri lile la kwenda na original certificate siku ya usaili ndilo lenye tija ambalo serikali ingeliendeleza kwenye kucertify kuna changa la macho sana kwani karani hupeleka copy bila kuona original na kuzigonnga muhuri kwa hakim.
ni heri kuamini kwamba Mungu yupo japo hatumuoni kuliko kuamini kwamba Mungu hayupo halafu siku ya mwisho tukamuona.

ukiwa na pesa certify ukiwa huna tuma bila kucertify
 
Naunga mkono hoja. Wanachpaswa ni kumweka afisa ambaye atapokea vyeti na kukagua originals, then afisa huyo apige muhuri - originals seen. Watanzania ni lazima tujifunze kuadjust taratibu mbalimbali ziendane na uhalisia wa mambo. Vijana wamefanya jitihada ya kusoma, sasa bado tunawawekea vizingiti kwenye jitihada ya kutafuta kazi!!!
 
katangeneze mhuri pale posta acha kuwa mvivu wa kufikiri .hujawahi kusikia huko dodoma wizara ya nishati kwenye elfu 20 waliongeza sifuri moja mbele wakalamba dume.
 
katangeneze mhuri pale posta acha kuwa mvivu wa kufikiri .hujawahi kusikia huko dodoma wizara ya nishati kwenye elfu 20 waliongeza sifuri moja mbele wakalamba dume.
nafikiri litakuwa jambo la busara sana,hakuna jinsi hapa zaidi ya kujitafutia muhuri wako.thanks mkuu!
 
tangazo la tarehe 25 mei ni la kiswahili na halijaandika mambo ya kusetifai,sasa hilo jingine wanalitoa after sisi wengine kutuma bila kusetifai ili iwe nija rahisi ya kutumwaga kua hatukusetifai. na wanaosema kusetifai ni lazima, sio kweli kwani unapoenda kwenye interview si unapeleka original copies sasa why lazima usetifai?anyway wao wana mpini mimi nimeshika makali wacha wafanye watakavyo!
 
Siwashangai vijana! Kwani mmekariri toka shule za msingi hadi vyuo vikuu!!!
 
Swala sio kuchonga mihuri au ukosefu wa fedha! hebu tujiulize,anayeweza kutambua kuwa cheti changu ni halali au batili ni chuo/baraza au wakili? Kama ni mawakili basi hata mitihani ya taifa/chuo wanatakiwa waisajili wao
 
Nilichokisema na ambacho bado nakisema ni kuwaomba tume ya ajira iondoe sharti la ku-certify vyeti kwa vile linaongeza ghalama zisizo za msingi waombaji kazi ambao wengi bado wanakuwa wako katika msoto.
Mbadala wa ku-certify vyeti uwe ni kwenda na vyeti halisi katika usaili iwapo utaitwa.
 
Back
Top Bottom