William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,400
Tume ya Mabadiliko ya Katiba imeomba kuongezewa muda wa mwezi mmoja kutokana na ugumu wa kazi ya uchambuzi wa maoni yaliyotolewa na wananchi na asasi mbalimbali.![]()
Tume hiyo inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba ilitakiwa kufanya kazi kwa miezi 18 kwa mujibu wa Sura ya 83 ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.
Maana yake ni kuwa Tume hiyo iliyoanza kazi Mei 1, mwaka jana ilitakiwa kukamilisha kazi yake Novemba 1, mwaka huu.
Ikiwa maombi hayo ya Tume yatakubaliwa ina maana watatakiwa kukabidhi ripoti yake Desemba 1, mwaka huu.
- Big nah! hawa tume ya Katiba wamegeuka kuwa opposition Institution ndani ya Serikali, wasiongezewe muda ni muhimu sana wakaondolewa hata leo kwa sababu tayari walishaamua mapema sana matokeo kabla hata ya kukusanya maoni kama walivyotakiwa na Sheria iliyowaunda. Nimeshuhudia kwa macho na masikio yangu nikiwa Moshi kwenye mkutano wa Tume hii na wananchi, Mjumbe wa Tume hii Butiku akiwakaripia wananchi kwamba Serikali tatu haina mjadala tena imeshapita, wananchi walipomjia juu akasema kwamba hana muda wa kusikiliza tena maana hiyo hoja tayari imeshapita, hivi hii tume ni kweli iliundwa kulazimisha wananchi hoja au maoni yao?
- Tume imejitwika madaraka makubwa mno ya kutengeneza maoni ya wananchi badala ya kusikiliza maoni ya wananchi, kama tume ina tatizo na maoni ya wananchi kuwa sio yao basi ingeandika kwenye majumuisho kwamba ina wasi wasi maoni mengi ya wananchi hayakuwa yao yalikuwa ni ya vyama vya siasa kwa sababu vyama vyote vya siasa nchini vinahusika na kuwapiga msasa wananchama wake kuhusu interest za vyama vyao kwenye katiba mpya wala sio siri. I mean kwa wajumbe wa Tume kuwakaripia wananchi wakitoa maoni yao kama nilivyoona Moshi na Singida, ni very clear kwamba Tume ilishapoteza uhalali wake kisheria siku nyingi sana.
- sijawahi kuona Tume ya kukusanya maoni tu, ipo kwenye media kila siku wajumbe wa tume wanaongea na media almost kila wakati WHY? Kazi yao ni kukusanya maoni tu sasa kwenye media wanatafuta nini? Wajumbe wa Tume wameingia mpaka kwenye malumbano na wanasiasa WHY? Kazi yao si ilikuwa kukusanya maoni tu ya wananchi, mbone tume zingine zilizopita hatukuwasikia kwenye media mpaka walipofikia kutoa ripoti tu, hii tume ya Katiba imepata wapi haya mamlaka mazito ya mpaka kukemea wananchi kuhusu maoni yao binafsi kwenye mikutano yake?
- The more wanavyozidi kuwepo ni more wanavyozidi kutuchanganya na kutugawa wananchi kwa sababu wanapenda sana media, nilijua muda hautawatosha maana kila wakati wapo kwenye malumbano na wanasiasa kwenye media sasa muda wa kuchambua maoni watautoa wapi? Nasema hivi Ikulu isiwape muda zaidi maana hii tume ni useless na ni waste, I mean katika kutembelea Dunia nzima as I have done except nchi 10 tu sijawahi kusikia tume inayokusanya maoni ya wananchi inalumbana na na walioituma kabla ya kuwasilisha ripoti yake, kwa kawaida huwa kunakuwa na malumbano baada ya kuwasilisha sio in the process ya kukusanya maoni, ndio ninasema hii ni tume iondolewe now inapotesa muda bure na mapesa ya wananchi, haifai kwa sababu ina wajumbe waliokwisha amua mapema sana maamuzi yao yawe ya wananchi na huku wakijua wazi kwamba ni against the law!
- HII TUME WANATUVURUGA VICHWA BURE WANANCHI IONDOLEWE NOW NA ISIONGEZEWE MUDA KABISA KWA SABABU TAYARI MWANANCHI KAMA MIMI NAJUA MATOKEO YA UCHAMBUZI WAO UTAKUWA NI NINI KUTOKANA NA MANENO YAO MENGI SANA KWENYE MEDIA NA MIKUTANO YAO, SO WAPO COMPROMISE HAWAFAI! NA NASHAURI IN THE FUTURE TUME KAMA HIZI WAPIGWE MARUFUKU KUONGEA NA MEDIA AU KUWEKA MAONI YAO KWA WANANCHI!!
- KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!!
Le Big Shoow - The King Of All Bongo Network Social Media@ Blogu ya Wananchi.