Tume ya Madini, tuambieni CPA ni nini kwenye initial za majina ya watumishi wenu

Tume ya Madini, tuambieni CPA ni nini kwenye initial za majina ya watumishi wenu

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
14,255
Reaction score
23,949
Kila kukicha TANZANIA haikosi vituko.

Tume ya madini tuambieni mtumishi jina kuanza na neno CPA, ni nini maana yake na kirefu chake ni nini.

Mfano ni huu hapa👇wa watumishi wa Tume ya Madini.

1. CPA. William E. Mtinya
Director, Corporate Services Department.

2. CPA. Elikana P. Buremo
Director, Internal Audit Unit.

3. CPA. Mwagule D. Ikunga
Manager, Finance and Accounts Section.

Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere , Huwa haitumii hizo initial, kwenu huko tume ya madini ni mabosi wa CAG?

Hii imetupa watanzania taharuki, na mambo ya kienda hivi , Kuna siku utumishi wa umma ,utakuwa ni kijiamulia kuchagua cheo cha kujiita.
 
CPA - Certified Public Accountant. Au nimekosea soulimeti? Ni title tu sawa na Mhandisi, Dr, Prof....

Screenshot_20240415_160604_Samsung Internet.jpg
 
Kila kukicha TANZANIA haikosi vituko.

Tume ya madini tuambieni mtumishi jina kuanza na neno CPA, ni nini maana yake na kirefu chake ni nini.

Mfano ni huu hapa👇

1. CPA. William E. Mtinya
Director, Corporate Services Department.

2. CPA. Elikana P. Buremo
Director, Internal Audit Unit.

3. CPA. Mwagule D. Ikunga
Manager, Finance and Accounts Section.

Hii imetupa taharuki, na mambo yakienda hivi , Kuna siku utumishi wa umma ,utakuwa ni kijiamulia kuchagua cheo cha kujiita.
Mbona ni kawaida Mzee Kuanza na Initial Ya CPA ni kama walivyo DR, Mr na zingine
 
Nenda Marekani au UK, haya mavyeo mbele ya majina ni kwa watu kama medical doctors, Dentists na Veterinary Doctors.Tanzania kuna mambo ya ajabu sana, kama Adv., Arch. Eng. CPA, Dr (za mchongo kama za wabonge baadhi)

Elimu ya vyeti ingeanzia huku, kila taaluma ingekuwa unatoa vyeti na watu wote wangeamua kuweka titles za walichosomea.
 
Hao ni watu waliothibitishwa kusomea kiwango cha juu kabisa cha taaluma ya uhasibu na ukaguzi wa mahesabu yaani Certified Public Account.

Kwa sheria za tanzania ni lazima uwe na CPA au related qualification kana ACCA ili kusimamia kitengo cha uhasibu au fedha au kufunga hesabu za mwaka za kampuni au taasisi au kufanya shughuli za ukaguzi wa mahesabu

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Nenda Marekani au UK, haya mavyeo mbele ya majina ni kwa watu kama medical doctors, Dentists na Veterinary Doctors.
Tanzania kuna mambo ya ajabu sana, kama Adv., Arch. Eng. CPA, Dr (za mchongo kama za wabonge baadhi)

Elimu ya vyeti ingeanzia huku, kila taaluma ingekuwa unatoa vyeti na watu wote wangeamua kuweka titles za walichosomea.
Ni mara chache au kama sio zote kumkuta wakili anaanza kujiita Adv. ABCD, ila hao watu wa CPA na wahandisi, wanapenda sana. Lakini sio kesi, wamepambania taaluma hizo acha wajiite watakavyo
 
Nenda Marekani au UK, haya mavyeo mbele ya majina ni kwa watu kama medical doctors, Dentists na Veterinary Doctors.
Tanzania kuna mambo ya ajabu sana, kama Adv., Arch. Eng. CPA, Dr (za mchongo kama za wabonge baadhi)

Elimu ya vyeti ingeanzia huku, kila taaluma ingekuwa unatoa vyeti na watu wote wangeamua kuweka titles za walichosomea.
Marekani Gani unayozungumzia Dunia Nzima CPA..Lazma watambulishwe Kwa Initial Aidha kwa kuandikwa mwanzo mwa Jina au Mwisho wa Jina..

Marekani wanatumia Mfumo wa Kuandika mwisho wa Jina kama Daktari anavyoandikwa..

Freddie matuja,CPA
Freddie matuja, MD

Ila sio mwanzo kama Uandishi wa Bristish
Dr Freddie Matuja
CPA freddie Matuja.

Tanzania Inafuata Mfumo wa British..
 
Mkuu wakati mwingine ukisema hizo title ni za mchongo unatakiwa uoneshe ulizo nazo kati ya hizo ulizotaja. Sawa Mkuu.

Alafu unakuta mtu kama wewe unamwambia mwanao asome aitwe wakili msomi kama Kibatala.

Karma anakuangalia tu anasubiri akupige tukio.
 
Marekani Gani unayozungumzia Dunia Nzima CPA..Lazma watambulishwe Kwa Initial Aidha kwa kuandikwa mwanzo mwa Jina au Mwisho wa Jina..

Marekani wanatumia Mfumo wa Kuandika mwisho wa Jina kama Daktari anavyoandikwa..

Freddie matuja,CPA
Freddie matuja, MD

Ila sio mwanzo kama Uandishi wa Bristish
Dr Freddie Matuja
CPA freddie Matuja.

Tanzania Inafuata Mfumo wa British..
Wala sio case mkuu.
Nipe Makala au jarida lolote linalomtambulisha mtaalam wa uhasibu iwe USA au UK (kwenye ACCA) ambapo utambulisho wa mhusika unakuwa sawia na maelezo yako.
 
Ni Tanzania tu ndio kuna huo upumbavu wa kuitana CPA. Tanzania sasa kila mtu anataka ajiite kwa fani yake, CPA, sijui bodi ua manunuzi, sijui bodi ya masekretari, bodi ya records management, bodi ya sukari, bodi ya nyama mtu ajiite Meat Expert John Okelo na ujinga mwingine.
 
Kila kukicha TANZANIA haikosi vituko.

Tume ya madini tuambieni mtumishi jina kuanza na neno CPA, ni nini maana yake na kirefu chake ni nini.

Mfano ni huu hapa👇

1. CPA. William E. Mtinya
Director, Corporate Services Department.

2. CPA. Elikana P. Buremo
Director, Internal Audit Unit.

3. CPA. Mwagule D. Ikunga
Manager, Finance and Accounts Section.

Hii imetupa taharuki, na mambo yakienda hivi , Kuna siku utumishi wa umma ,utakuwa ni kijiamulia kuchagua cheo cha kujiita.
Watu wamekujibu hapo juu lakini binafsi uwa naamini watu wanaohangaika kuonyesha shule yao mara nyingi hawapo vizuri kitaaluma sababu shule ya mtu ni utendaji, ubunifu na uzoefu wako unatakiwa ukutofautishe na wasiokuwa na taaluma husika, hivyo vyeti umuhimu wake upo kwenye resume au linkedin unapokuwa unatafuta kazi au network kwa ajili ya career yako lakini siyo kila mahali. Ni kama vile hamna kitu kinasikitisha kama nikienda kwenye misiba halafu mfu aliyesoma anazungumziwa kwa shule yake kuliko mchango aliofanya hapa dunia kwa akili au elimu yake. Kwanini nimeandika haya, ukiangalia changamoto zetu hapa Tanzania ndani ya sekta zote iwe Uchumi, elimu, afya, maji,umeme,media, sheria,siasa nakadhalika inashangaza kuona kuna watu wanajiita wasomi na wameshika madaraka ya kufanya maamuzi wakati Nchi inaenda kombo lakini wamejaa na mavyeti kama wazee wa CPA.
 
Kila kukicha TANZANIA haikosi vituko.

Tume ya madini tuambieni mtumishi jina kuanza na neno CPA, ni nini maana yake na kirefu chake ni nini.

Mfano ni huu hapa👇

1. CPA. William E. Mtinya
Director, Corporate Services Department.

2. CPA. Elikana P. Buremo
Director, Internal Audit Unit.

3. CPA. Mwagule D. Ikunga
Manager, Finance and Accounts Section.

Hii imetupa taharuki, na mambo yakienda hivi , Kuna siku utumishi wa umma ,utakuwa ni kijiamulia kuchagua cheo cha kujiita.
CPA zimeweza kuisaidiaje Tume ya madini, kutatua changamoto za Tume? Mapato ya Tume ya koje?
 
Back
Top Bottom