Tume ya Madini, tuambieni CPA ni nini kwenye initial za majina ya watumishi wenu

Haina Shida hao ni Wahasibu ,kutanguliza 'CPA' mbele ya Jina ipo kisheria ndani ya Sheria na Kanuni za Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu(NBAA)na siyo fatal,labda kama una hoja nyingine kuhusu uwepo wao hapo..
 
Tena wengi unakuta ni graduate cpa
Sio lazima awe graduate. Wanaweza kua ni wakongwe zaidi ila hawajazi mafomu ya kubadili graduate kwenda associate na hawahuzurii semina.

Nina ndugu yangu ni kiongozi mkubwa wa serikali alipata cpa toka 1998 hadi sasa ni graduate cpa kwa sababu hajawahi kujaza form za kuomba kuhama.
 
Hata aliekua Rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad ni profesa wa Physics. Hakuna mahala amewahi kujiita professor. Hata hata alipomaliza urais amerudi chuo kikuu kufundisha ana vipindi vyake kama mwalimu wa kawaida.

Aliekuwa kansela wa Ujerumani mama Angela Markel alikua na Phd ya Physics lakini hakuna mahala alikua anajiita Doctor.

Nyerere alikataaa kuitwa Dokta, Mugabe alikataa kuitwa Dokta na alikua na degree zake mwenyewe za kusoma 7 acha za kupewa.

Ujinga huu wa kujisifia kielimu umeanza wakati wa Kikwete mara ajiite professa, mara dokta mambo ya hovyo.

Sasa hivi Tanzania kila mtu anajiita cpa, cpa. Ila ujinga huu uko kwenye baadhi ya taasisi za umma, sio zote. Mfano CAG hajiiti CPA na hata Assad hakua anajiita CPA.
 
Haina Shida hao ni Wahasibu ,kutanguliza 'CPA' mbele ya Jina ipo kisheria ndani ya Sheria na Kanuni za Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu(NBAA)na siyo fatal,labda kama una hoja nyingine kuhusu uwepo wao hapo..
Nendeni mkabadili sheria mnatia aibu. Kama kuna members wa NBAA humu chukueni thread hii kama maoni ya wadau wenu.

Mtu kama Makalla ajitambulishe hivi; Amos Makalla, CPA, Siyo CPA Amos Makalla.

Hata kama ni sheria yenu tambueni tu kuwa ina bowa
 
Sio kweli, nilikuwa na Boss foreigner ni Chartered Accountant lakini hana huo ushuzi, ni kaushamba tunako tuu.
 
Nendeni mkabadili sheria mnatia aibu. Kama kuna members wa NBAA humu chukueni thread hii kama maoni ya wadau wenu.

Mtu kama Makalla ajitambulishe hivi; Amos Makalla, CPA, Siyo CPA Amos Makalla.

Hata kama ni sheria yenu tambueni tu kuwa ina bowa
Jenga hoja yenye element za legislative legal Drafting kwanini Sheria ibadilishwe na siyo hisia tu Kwa sababu ya generalization na possible chuki zako binafsi Kwa Makala.Nini athari za ku- maintain status quo na nini faida ya Hilo badiliko unalopendekeza?
 
Tume ya Madini, mkiandikwa na kupewa machungu yenu humu Jf ,Huwa mnaziba masikio yenu na kufunga macho, mkijifanya hasikii na hamuelewi.

Fanyieni Uzi huu kazi na mtambue kuwa , Katibu mkuu Ofisi ya Rais utumishi yumo Jf, anawaangalia tu.

Atachukua hatua!
 
Hizi ni za kuombea kazi mkuu. Yaani umeingia kwenye platforms za ajira au company portfolio. Wenzetu hawana sana haya mambo ya kuitana wakili msomi au CPA. Ila si tatizo tukiitana huku ni sawa tu pia, sioni ulazima ila ni sawa tu.
Wakili msomi ni swala la kidunia, kwani huangalii hata movie za wenzetu Mkuu?
 
Hapo tume ya madini unataka wafanye Nini?
 
Kwa hio kila mtu awe kama Mugabe,Nyerere?
 
Hapo tume ya madini unataka wafanye Nini?
1. IT wa Tume ya madini ,Angie kwenye mfumo wao,afute hayo ma CPA kwenye majina ya watumishi walio tajwa.
2. Tume ya madini ,ijikite kutatua kero za wachimbaji na kuepuka kutumia wataalamu ambao VYEO ni vikubwa utendaji ni mdogo.
3. Hao wanajiita CPA wawe field zaidi badala ya kukakaa maofisini .
 
Kwa wao kuandika hizo Cpa mbele ya majina yao,naomba unitajie sheria waliyovunja?
 
Huu sasa ni wakati wa kila msomi kutafta initial yake lazma tuheshimiane mjini
 
CPA. Elikana P. Buremo
Director, Internal Audit Unit.

3. CPA. Mwagule D. Ikunga
Manager, Finance and Accounts Section.
acheni wivu wakuu someni na nyie mpate hizo cpa.. na hapo wanafanya kazi zao kwa vyeti vyao namba mbili na tatu sio ajabu kuanza na cpa kama anayo...... cpa sio matako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…