Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kufumuliwa

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kufumuliwa

NEC Ili iweze kutenda haki na kulaumiwa kama haijatenda haki ni lazima kuondoa watumishi wa serikali hasa wakurugenzi na watendaji.wa kata na watumishi wengine. Tume lazima iajiri watumishi wake.
Yaani watumishi wakiwa wa kuajiriwa itakuwa rahisi kula rushwa popote pale penye mnofu,

Yaani chama kitakacho honga sana ndicho kitakachopata upendeleo kwa muhusika yule.

Bado CCM itakuwa mstari wa mbele kuhonga ,kwa vile hazina ya nchi iko mikononi mwao.

Naona iwe Tume huru ili ikiburunga iweze kushtakiwa Mahakamani. Iwe hivyo hata kwa kura za Raisi
 
Mwalimu anatakiwa awe mfano mzuri kwa wanafunzi wake !!
Mkuu ni kweli...lakini usisahau hawa wasomi wetu wakipewa teuzi hasa kipindi cha awamu iliyopita walikuwa wanajitoa ufahamu..mfano mzuri ni Prof Kabudi, na hata Kitila (ukiangalia michango ya Kitila sasa hivi huko Twitter utadhani sio Kitila yule aliyekwenda kuzindua trela kule Ruvu JKT)!
 
View attachment 2183424
  • Kuajiri watumishi wake hadi ngazi ya Wilaya, kata
  • Sasa rasmi kusimamia uchaguzi Serikali za Mitaa
  • Mapendekezo ya muundo wake yasubiri wadau
===
Kwa mujibu wa Gazeti la Raia Mwema la Aprili 11, 2022 ni kuwa kuna uwezekano mkubwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuundwa upya kabla ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2025 na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024.

Aidha, gazeti hilo linaelezwa kuwa taarifa za ndani ya Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na kikosi kazi zinaeleza kuwa tayari mapendekezo ya kuunda upya kwa NEC yameshawasilishwa kwa Rais Samia na ndani ya muda mfupi chombo hicho kitaundwa upya.

Zaidi ya hayo, inaelezwa kuwa kiongozi Mwandamizi ndani ya CCM alieleza kuwa Tume ya Uchaguzi iliyopo sasa imeonekana machoni mwa watu kuwa imeshindwa kusimamia uchaguzi hasa kutokana na muundo wake uliopo kwa sasa, hivyo kikosi kazi kimependekeza Tume hiyo iwekewe Muundo mpya ikiwamo watendaji wake.

Taarifa juu ya kufumuliwa kwa Tume ya Uchaguzi zinakuja baada kuwapo malalamiko kutoka kwa wadau mbalimbali juu ya Muundo wa NEC pamoja na Mamlaka ya Tume hiyo kushindwa kusimamia Uchaguzi Huru na Haki.

Zaidi kuhusu taarifa hizi soma hapa chini

View attachment 2183528

View attachment 2183541
View attachment 2183542
View attachment 2183543

Chanzo: Raia Mwema
Namkumbuka huyo bwana Mahera hapo pichani, wakati huo alikuwa na nguvu kama rais wa nchi, ni muuaji mkuu wa demokrasia ya nchi yetu.
 
Hujaelewa, kufumuliwa ifumuliwe lakini sio kwa utaratibu wa kuajiri kuanzia mtaa, we unategemea ni watumishi wangapi wataajiriwa nchi nzima. Hapo ndio nnapokataa. Ni Kama leo TRA iajiri kuanzia mtaa. Yaani kuwe na ofisi ya mtaa, kata,
Jambo la muhimu ni kuwa NEC iwe na watumishi wake. Itakuwa na watumishi waje kwa muundo gani, ni suala jingine.

Nadhani NEC itakuwa na watumishi wake wa kudumu, na wengine wa mkataba wa muda mfupi, ikiwezekana kwa miezi 6 tu.
 
Dk. Charles Wilson Mahera ( aliyekuwa Mtu wa Hayati Rais Dkt. Magufuli Kiukaribu na Kiutii ) hatakiwi tena hapo, ila huenda bado wanatafakari ni wapi wampeleke Kiuteuzi kama akiondolewa katika hiyo Nafasi Muhimu na Nyeti katika Maamuzi ya Afya ya Kisiasa, Kiusalama na Kidemokrasia nchini.
Mhalifu kama Mahera hastahili kuumiza vichwa, wapi kwa kumpeleka. Ni kumrydisha kwenye ukurugenzi wa Halmashauri. Anaweza kupelrkwa huko Uvinza au Namanyere. Akileta upuuzi wake, atashughulikiwa huko huko.
 
  • Kuajiri watumishi wake hadi ngazi ya Wilaya, kata
  • Sasa rasmi kusimamia uchaguzi Serikali za Mitaa
  • Mapendekezo ya muundo wake yasubiri wadau
Je hawatakuwa na bei ya kuwanunua!?
 
Huo ufumuaji hautakuwa na maana kama mamlaka ya uteuzi wa mwenyekiti wa tume itabaki ile ile.
Hautakuwa na maana kabisa kama MAMLAKA YA UTEUZI WA MWENYEKITI WA TUME IABAKI ILE ILE.
Tunaposema madarakani ya rais yapunguzwe, (na ni kwa kupitia KATIBA MPYA) watu hawaelewi kabisa.
 
View attachment 2183424
  • Kuajiri watumishi wake hadi ngazi ya Wilaya, kata
  • Sasa rasmi kusimamia uchaguzi Serikali za Mitaa
  • Mapendekezo ya muundo wake yasubiri wadau
===
Kwa mujibu wa Gazeti la Raia Mwema la Aprili 11, 2022 ni kuwa kuna uwezekano mkubwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuundwa upya kabla ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2025 na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024.

Aidha, gazeti hilo linaelezwa kuwa taarifa za ndani ya Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na kikosi kazi zinaeleza kuwa tayari mapendekezo ya kuunda upya kwa NEC yameshawasilishwa kwa Rais Samia na ndani ya muda mfupi chombo hicho kitaundwa upya.

Zaidi ya hayo, inaelezwa kuwa kiongozi Mwandamizi ndani ya CCM alieleza kuwa Tume ya Uchaguzi iliyopo sasa imeonekana machoni mwa watu kuwa imeshindwa kusimamia uchaguzi hasa kutokana na muundo wake uliopo kwa sasa, hivyo kikosi kazi kimependekeza Tume hiyo iwekewe Muundo mpya ikiwamo watendaji wake.

Taarifa juu ya kufumuliwa kwa Tume ya Uchaguzi zinakuja baada kuwapo malalamiko kutoka kwa wadau mbalimbali juu ya Muundo wa NEC pamoja na Mamlaka ya Tume hiyo kushindwa kusimamia Uchaguzi Huru na Haki.

Zaidi kuhusu taarifa hizi soma hapa chini

View attachment 2183528

View attachment 2183541
View attachment 2183542
View attachment 2183543

Chanzo: Raia Mwema
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ipo kikatiba kwa mujibu wa Ibara ya 74(1-5 na mjukumu yake Ibara ya 74 (6) (a-e), kifungu cha 4c cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343 na Tume kuwa chombo huru kwa mujibu wa Ibara 7 na 11. Tume pia ipo kwenye katiba pendekezwa. Kama ni mabadiliko lazima Katiba ibadilishwe na Bunge litunge sheria pia
 
Hoja siyo kufumuliwa na kuundwa upya! Hoja ni je itakuwa huru wakati wa kumtangaza mshindi halali? Si kwamba pamoja na kufumuliwa bado matokeo ya kura yatasimamiwa na JWTZ,TISS na Polisi?
 
Mfumo mzima wa tume kusiwe na mtu anayeteuliwa na President....

Hapo tunaweza kuanza kujadili mengine
 
Kwasababu ya upumbavu wako hujui gharama sio kitu mbele ya amani. Tume ya taifa inge au itasababisha vita siku moja gharama sio kitu.
Wewe ni mjinga mmoja mkubwa sana- sasa unamatukana mwenzako sababu ikiwa ni ipi- mjinga sana wewe. HUNA UNALOELEWA NA HIYO NI HULKA ZA UANAHARAKATI
 
CCM haiwezi kutengeneza mazingira ya CCM kushindwa. Ukiona wanatengeneza kitu ujue wanajua namna ya kukitumia kuendelea kukaa madarakani.
 
NEC Ili iweze kutenda haki na kulaumiwa kama haijatenda haki ni lazima kuondoa watumishi wa serikali hasa wakurugenzi na watendaji.wa kata na watumishi wengine. Tume lazima iajiri watumishi wake.
Haitasaidia kitu kama watumishi wake wataendelea kuona wajibu wao ni kwa Chama Tawala na sio Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tume iliyopo ilikuwa na mamlaka ya kuwaadabisha wasimamizi wa uchaguzi ambao walionekana dhahiri kuegemea upande fulanilakinini hawakufanya hivyo kwa sababu na wao waliegemea upande ule ule. Tume ilikuwa na haki ya kubatilisha maamuzi ya kuwaondoa wagombea kwa sababu za kijinga lakini hawakufanya hivyo kwa sababu waliunga mkono vitendo hivyo.

Hivi Tume walishindwaje kuhakikisha kuwa wasimamizi wa uchaguzi wanakuwepo katika vituo vyao katika muda wote wa kupokea fomu za kugombea uchaguzi kutoka kwa wagombea wote? Kuna uchaguzi mmoja, Mkurugenzi alifunga ofisi yake akajificha mahali. Wagombea wasio wa Chama Tawala walimpigia simu Mkurugenzi wa Uchaguzi aliyepita, kumueleza kuhusu hali hiyo na aliwaahidi atachukua hatua. Hakufanya lolote na aliidhinisha taarifa ya Mkurugenzi kuwa mgombea wa Chama Tawala alipita bila kupingwa kwa sababu hamna mgombea mwingine aliyewasilisha fomu zake katika wakati muafaka. Aidha, hata nje yautumishi wa uma kuna makada ambao wataweza kuajiriwa ili wasimamie uchaguzi. Bila Katiba Mpya itakayobadilisha upatikanaji wa viongozi wa Tume, yote haya hayataleta mabadiliko yeyote ya maana isipokuwa kuturudisha kwenye aina ya uchaguzi tuliokuwa nao kabla ya 2015.

Amandla...
 
Back
Top Bottom