Uchaguzi 2020 Tume ya taifa ya uchaguzi (NEC), nawasihi, kupitisha jina la Lissu kugombea Urais, ni kuweka rehani Amani na Usalama wa Taifa

Do not exaggerate. Hakuna matamshi mabaya aliyotoa. Ila anaitahadharisha tume ya uchaguzi na vyombo vya dola kutoharibu uchaguzi. Anataka uchaguzi uwe wa huru na haki. Swala la kumhusisa JPM na kupigwa kwake risasi ni la kisheria na vyombo husika vinatakiwa kufanya kazi zake. Sisi wananchi na wapiga kura halituhusu.
 
Huu ujinga ndio mnalishwa kisha mkitumika mnatelekezwa ,majuto mjukuu
Amani itavunjwa na CCM kwa matendo yake ya hovyo hovyo kuwaonea kuwahujumu kuwabambikia kesi kuwapiga risasi kuwapora ushindi wapinzani
 
Mimi na yule mwenyekiti wako wa maisha alievunjika mguu kwa ulevi yupi smart?
Wewe ni Lijuakali aliyevaa max usiku akampiga mbowe akatokomea nyumba ya jirani usifikiri watu hawajui ni nani alimpiga mbowe, uovu wa CCM wote upo wazi hakuna baya la CCM lisilojulikana
 
Hivi mbona makada wa CCM mmeingiwa na hofu kuhusiana na Tundu Lissu kutia nia ktk kinyang'anyiro cha nafasi ya uraisi? Hivi ilikuwa ni njama kwa kuvipiga marufuku visitangaze matukio yake ya kusaka wadhamini, ili kitafutwe kisingizio kuwa alitukana matusi ama kufanya uchochezi!

Hivi yale matukio ya kuchoma ofisi za CDM kule Arusha na Mbeya yalikuwa na nia ya kuwachochea wananchi wapandwe na jazba na kufanya fujo ili zitafutwe sababu za kumuengua siyo? Ile njama ya kuupopoa msafara wake kule Hai ilikuwa ni mtego mwingine siyo?

Ikiwa kama miradi mikubwa ya kimkakati inakibeba chama tawala hofu ni ya nini sasa? Ikiwa kama ujenzi wa SGR, bwawa la umeme la Mwl. Nyerere, barabara, hospitali na madaraja, na pia ikiwa kama serikali inatoa elimu ya msingi bure na kuboresha huduma za afya ikiwemo kulisambalatisha gonjwa hatari la COVID-19 hapa nchini kwa muda mfupi, hofu ya nini sasa?

Hukumu na hakimu ni wananchi. Mbona makada wa CCM wanaogopa kushtakiwa mbele ya wapigakura? Mbona wanaziogopa hoja za mashtaka zinazotolewa na Lissu kiasi kwamba wanaziita ni matusi na uchochezi? Orodhesheni nanyi mashtaka yenu kwa lugha rahisi ili kila mtu akapate kuelewa.
 
UOGA HAUWEZI KULETA MAENDELEO EWE KIRUS CHA FARAO
 
Ofisi mlichoma wenyewe na imekua jadi kwenu
 
NEC haiwezi kusikiliza maoni ya mtu mlevi asiye na akili.
Mkurugenzi wa NEC anachunguzwa na taasisi za haku za binadamu Duniani mahakama ya uhalifu The Hague, FBI, Scotland yard na vyombo vingine vya kimataifa kuanzia Nchi jirani na kwingineko kote Duniani akijichanganya akafanya ujinga atambue kuwa Duniani kote watajua ushetani wake.
 
Ushetani wote wa CCM unafuatiliwa Duniani kote kwani wameshajua chama shetani kipo Tanzania
 

Kwanza nani kakuuliza kama umetumwa au la? Yes, tunajua umetumwa, ndiyo maana umetanguliza kujitetea.

Hilo kundi lenu la "usalama uchwara" mnaozunguka humu mitandaaoni kueneza propaganda na kuwaingizia hofu watawala ili wavunje sheria za uchaguzi makusudi kwa lengo la kubaki madarakani hamuisaidii nchi bali mnaiandaa for disaster.

Kama kweli Tume ya Uchaguzi imejipanga kutenda haki, na serikali na CCM yao hawajipangi kuiba au kudhulumu haki ya wananchi, hii hofu yote kwa Lissu ya nini? Msidhani mnawazi akili mamilioni ya watanzania mliowaziba midomo kwa miaka 5. Hamtaweza, hamjajipanga, wala hamna mbinu sahihi za kuzuwia wananchokitaka wananchi kupitia sanduku la kura.

Amani ya nchi itabaki kwa kutenda mambo mawili tu:

1. Kuacha haki itendeke katika process nzima ya uchaguzi. Msilogwe wala kuchochewa na shetani yeyote kuleta mizengwe kwenye uteuzi wa Lissu. Kufanya janja yoyote kuzuwia Lissu asigombee kwa sababu ya visingizio vyovyote ni kuamua moto uanze kuwaka mapema kabla ya uchaguzi, na hivyo kupelekea uchaguzi usiwepo kabisa. Msijaribu.!

2. Kuweka mfumo wa wazi wa kutangaza matokeo halali mwanzo mwisho na kuviruhusu vyama vyote vya siasa vikusanye matokeo yake na kulinganisha na ya Tume ili kila upande uridhike na mshindi halali. Mnaogopa nini kuweka wazi kama mnaheshimu matakwa ya wananchi?

Kinyume cha hapo, mjiandae kupambana na wananchi wenye hasira kali na waliochoka na upuuzi wenu wa kila uchaguzi. Hasira zote za watanzania zilizofunikwa kwa miaka mingi mtaziona mwaka huu mkifanya ujinga. Na nyie mnaojiita usalama mtaikimbia nchi na kuliachia jeshi la wananchi kuokota vipande vya mabaki ya upuuzi wenu.

Lissu sio tatizo. Lissu ni kikwazo cha uonevu, wizi, vurugu, na dhuluma yenu dhidi ya wananchi. Mnamwogopa kwa sababu mnajua, huyu si kama Lowassa 2015. Hana damu ya CCM ya unafiki na uoga. Ana maanisha kweli. Kajitoa sadaka ili Tanzania ipone. Kuna nini ambacho hamjafanya dhidi yake mpaka awaogope? Kama hata ishara za Mungu hamziogopi subiri mkutane na kisasi chake dhidi ya uovu mkubwa mnaoitendea hii nchi.
 
Akili yako ina utapiamlo sio bure
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…