Uchaguzi 2020 Tume ya Taifa ya Uchaguzi, yatoa ratiba ya Uchaguzi 2020

Uchaguzi 2020 Tume ya Taifa ya Uchaguzi, yatoa ratiba ya Uchaguzi 2020

wanahesabu kura au wanafanya tallying ya matokeo ya vituoni?
yani tunarudi zile zama za kulinda masandaku halmashhuri ndio yahesabiwe ?
 
Nimepitia hiyo Ratiba na kuona mapungufu 8 ya haraka katika vipengere vifuatavyo:

12. Kuhusu Kupokea Pingamizi dhidi ya Uteuzi wa Wagombea Ubunge na Udiwani : Hivi ni Madiwani na wabunge pekee waopingwa au hata uteuzi wa Raisi pia waweza kupingwa ?
14: Kushughulikia pingamizi dhidi ya Uteuzi wa Wagombea Ubunge na Udiwani : Pingamizi dhidi ya wagombea uraisi ni lini?
29. Kuchambua na kupanga vifaa vya kupigia kura kwa kila kituo :Hili ndilo linatakiwa kuwa la kwanza au la pili at maximum.
33. Vyama vya siasa kupatiwa Orodha ya Vituo vya Kupigia Kura: Hili liwe la pili baada ya number 29.
37. Mawakala wa Vyama vya Siasa pamoja na Mawakala mbadala kula kiapo cha kutunza siri mbele ya Wasimamizi wa Uchaguzi/ Wasimamizi Wasaidizi kwenye Kata siku 7 kabla ya Siku ya Uchaguzi : Ni siri gani inayozungumziwa hapa? kificho cha matokeo au kiapo cha siri cha mambo mengine. ni yapi hayo?
42. Kuvitaarifu vyama vya Siasa mahali pa kujumlishia kura : de facto, Kwa nini isiwe katika kituo cha kupigia kura? au wanataka kuchakachua
47. Kusafirisha masanduku ya Kura, Fomu na vifaa vya Uchaguzi wa Rais, na Wabunge kutoka vituoni kwenda Makao Makuu ya Halmashauri.  Kusafirisha masanduku ya Kura, Fomu na vifaa vya Uchaguzi wa Madiwani hadi Makao Makuu ya Kata : hapa ndio uchakachuaji wenyewe unafanyika ... matokeo yatangazwe vituoni na majibu yatolewe pale pale kama uchaguzi wa ccm kuwapata wagombea ulivyofanyika
48. Kujumlisha Kura za Uchaguzi wa Rais na Wabunge – Makuu ya Halmashauri  Kujumlisha Kura za Uchaguzi wa Madiwani Makao Makuu ya Kata : Huu ni Mushkeri mwingine huu... kura zihesabiwe mahala zilipo pigiwa full stop , hakuna njia nyingine zaidi ya hii. Tume iyakusanye majibu kutoka kila kituo na kuyajumlisha kwa wazi kama walivyofanya kenya.. short of that ni uchakachuaji.. full stop .

Ni hayo tu kwa leo, maboresha yanaruhusiwa bila mkwaruzo....

Upo sahihi nilimsikia Mnyika akilalamika kuw amwaka huu hakuna kuhesdabu kura vituoni na hata zikihesabiwa hakuna kupewa fomu ya matokeo vituoni, kwahiyo hatutayajua matokeo mpaka wakachakachue halmashahuri.
 
Upo sahihi nilimsikia Mnyika akilalamika kuw amwaka huu hakuna kuhesdabu kura vituoni na hata zikihesabiwa hakuna kupewa fomu ya matokeo vituoni, kwahiyo hatutayajua matokeo mpaka wakachakachue halmashahuri.
Na cha ajabu zaidi ni kwamba hivi vyama vya upinzani vimekubali tu kupelekeshwa pelekeshwa na tume ya uchaguzi, sijui wapinzani wanakubali vipi kufanya mtihani ambao hawakuusomea, ina maana tayari wanayajua matokeo au wamekubalina nayo kabla hata ya mtihani wenyewe kutoka...
 
Sasa kwa mfano urais nani huko upinzani anakubalika zaidi ya Magufuli?

Tundu Lisu dhambi ya kumkejeli Nyerere inampotezea ushawishi kabisa!
60% vijana hata hawakuwahi kumuona Nyerere...umeona msiba wa Mkapa vijana wakiulizwa mnamzungumziaje hawana cha kujibu..nyie vikongwe ni 10% ya Watanzania mnaomjua mwalimu
 
Hiyo namba 7, wagombea kuweka fedha za dhamana ni kinyume cha katiba. Itawanyima fursa baadhi ya wagombea, hela ya fomu tu inatosha. Dhamana tena ya kazi gani??
 
Back
Top Bottom